Haya Wakenya kubadilisha Katiba tena, mpaka kieleweke, Rais Magufuli tafadhali usiguse Katiba yetu!

Nchi za kijinga kijinga ndizo zinazokurupuka na kutuhumu katiba. Watu wanaojielewa wanashugulikia matatizo ya msingi ya nchi yao. Katiba will never solve the problems kama hakuna utashi wa kweli kwa viongozi.
Matatizo ya msingi yanatatuliwa kupitia sheria ambazo zinatekelezwa chini ya katiba ambayo inaheshimika na wote. Acha nikupe mifano kadhaa ya hayo unayoyaita matatizo ya msingi ambayo yametatuliwa chini ya katiba mpya ya Kenya. Ubaguzi dhidi ya wanawake likija kwenye suala la kumiliki mali. Haki za wananchi likija kwenye suala la huduma bora bila ubabaishaji wala ubaguzi kwenye taasisi za umma. Kujumuishwa kwa mwananchi wa kawaida kwenye maamuzi yanayomhusu kupitia bunge za mashinani na pia kwenye kura za maamuzi. Wananchi mashinani kuwezeshwa kujiamulia wenyewe maendeleo wanayoyataka kwenye county zao kupitia 'public participation', hili limewekwa wazi kwenye sheria. Mhimili wa mahakama kuwa na nguvu za kubatilisha maamuzi hata yawe ya nani. N.K.
 
Kwa wale mnaokejeli katiba ya Kenya ni wazi hamna lolote mnalolijua kuihusu. Manufaa ambayo yamekuja na hii katiba hamyajui pia. Kama hauniamini nenda ukaulize mkaazi yeyote mkaazi wa sehemu kame za Kenya. Mbona mambo ya pwani si Kenya hayasikiki tena?. Mapungufu ya katiba yalitambuliwa mapema mno lakini cha msingi ikawa ni kupitisha halafu marekebisho baadaye. Wengine wanadai sii kwa manufaa ya mwananchi, nani kakudanganya? Ngoja uone vile hii game inachezwa. Nyinyi toshekeni na yenyu nzee, haituhusu ndewe wala sikio!.
 
Tribalism has increased, Court orders are disobeyed by gvt, Joblessness is at its peak.Corruption is now institutionalised.
You dont need Constitutional changes but ethics in governance...As long as criminals like uhuru and ruto are leaders forget about good governance
 
Tumia kura yako kupinga marekebisho kwenye katiba, ni haki yako. Pia kwenye uchaguzi mkuu tumia kura yako kuwachagua viongozi ambao unawataka wewe. La sivyo hata baada ya uchaguzi wa 2022 utabaki kulialia kuhusu yule atakaye kuwa madarakani kwa miaka mingine mitano hadi itakapofika 2027. Alafu tena uanze upya.
 
Asante Dkt.Peter Mselewa kwa maelezo ya kiutaalamu.
 
Wewe ni mtu mwerevu sana
 
Raisi , makamu wa raisi , waziri mkuu . Kwa nchi masikini unaonaje ?
 
Hivi wewe jamaa una matatizo gani kichwani mwako?, wewe unapelekeshwa kama nguruwe wala hujitambui nini unafanya hapa duniani. Juzi tu mlikua mkisifia kwamba katiba ya Kenya is the best, leo mnasema imelibebesha mzigo mkubwa kwa wananchi kwahiyo irekebishwe kupunguza mzigo, inamaana wakati mnaipitisha haumkuliona hilo?, hao MCA kuwa wengi na wabunge walipitishwa na katiba ipi na watu wa nchi gani?, sasa unataka kutuaminisha kwamba watu haohao waliofanya makosa ya wazi kabisa leo hii wanapochukua maamuzi mengine wasitiliwe mashaka kwamba ni muendelezo uleule wa maamuzi ya ovyo?
 
Acha kupiga domo, matatizo ya msingi na ya muda mrefu Kenya ni
1)Tribalism
2)Corruption
3)Land ownership
4)Nepotism
5)Unemployment
6)Big gap between richer and poorer
7)Insecurity

Msipopata ufumbuzi wa hayo matatizo, mtaendelea kuandika katiba hadi Yesu atashuka na kuwakuta bado hamjamaliza.
 

Kijana unaelewa maana ya katiba ingine (new constition) na kubadilisha vipengee (ammendement).
Constitional amendments are constant.
Ata kama sikubali mwenyewe, every country holds constitional ammendements.

Alafu, ile katiba ya kitambo ingefanywa ammendements bila kuhitaji referendum. Mfano tulipo ondoa section 2A ya one-party state.
Lakini mabadiliko kwenye hii katiba lazima irudi kwa wananchi.
 
Tatizo huu uzi umeuleta kimahaba ukiwa na nia ya kuwakandamiza Watanzania wenzio na kuwatamausha wasidai katiba mpya, hutaki mjadala wa kitaalam, mwenye unaanzisha uzi halafu unatiririka kejeli za kitoto.
Unanikumbusha enzi zangu za utotoni, mtoto aliyekua anamiliki mpira ndiye alikua anachagua timu, akina nani wanaruhusiwa kuucheza na pia timu yake iwe na akina nani halafu upinzani washirikishwe nani, pia alikua anaamua mchezo unaanzia wapi, maana ameutia mpira kwapani hadi mashariti yake yazingatiwe, kisha hamna cha kipyenga wala nini, yeye atachagua wapi ataushushia na kupiga kiki, ikiwemo karibu na kipa wa upinzani, hivyo kiki lake la mwanzo linaweza kuwa goli.

Katiba yetu ni nzuri, tena bora sana zaidi ya karibia zote Afrika, lakini pia kama kitu chochote kingine kipya ambacho ndio cha kwanza tangu uhuru, lazima humo kuna kasoro za kiaina ambazo zinahitaji kuboreshwa zaidi. Hamna sehemu imetajwa kwamba tunaingiza wadhifa wa waziri mkuu, hayo yanaibuka kwenye majadiliano baina ya Wakenya kuhusu nchi yao, ni jambo la kawaida hoja za kila aina kuibuka, najua unapata tabu maana mumewakalia Watanzania hadi hawana uhuru wa kusema chochote, sasa unashangaa kuwaona Wakenya wakizungumza.

Marekani katiba yao ni ya miaka 200 na imarekebishwa mara 27, huo ni wastani wa mabadiliko kila baada ya miaka saba.
 
Nchi za kiafrika hazikutakiwa kufata hii demokrasia ya kimagharibi ni ghari sana,uchumi wa nchi nyingi hauwezi kumudu,
Jirani zetu,baada ya miaka kumi,wamegundua likabrasha walilojitayarishia linawatia gharama kubwa kulisimamia,mwananchi anataka huduma bora,elimu,chakula,makazi,Uhuru,sio utitiri wa viongozi,
 
Sasa wewe ulipigia kura mwizi uhuru kenyatta..leo unalialia ufisadi, Taxes etc. Kila siku mungiki wenzako wanalia Tano tena ni gùtee..Akili ama kamasi?
 

Soma nilivyomjibu mleta mada hapo juu, uongozi bora au hivyo vitu unavitaja haviji bila mwongozo mzuri wa katiba, hauwezi ukaendesha nchi kwa visasi na matamko bila kuzingatia katiba halafu utegemee kufaulu.
 
Tatizo sio kubadilisha katiba bali unabadilisha katiba kwa maslahi ya nani! Kama unabadilisha kwa maslahi ya wananchi/taifa; let it be. Tatizo ni pale wanaobadilisha katiba wanapokuwa ni wale wenye kariba ya akina Paul Kagame au Yoweri Museven ambao uzoefu unaonesha kwamba, mabadiliko wanayoyapigia chapuo ni yale yanayowahakikishia madaraka makubwa zaidi na kukaa madarakani muda mrefu zaidi!

Chemsha Bongo:

Je, huyu wa kwetu ana kariba ya nani kati ya ile aliyonayo Uhuru Kenyatta au waliyonayo Yoweri Museven na mwenzake Paul Kagame.
 
Sasa wewe ulipigia kura mwizi uhuru kenyatta..leo unalialia ufisadi, Taxes etc. Kila siku mungiki wenzako wanalia Tano tena ni gùtee..Akili ama kamasi?
Sasa ukitupa mitusi kwa wale wengi wa wakenya waliompigia kura rais Uhuru Kenyatta ndio unajiona mjanja? Mbona mliowaunga mkono nyinyi mlio wachache wamechanganyikiwa na hata majukumu yao rahisi kama upinzani wameshindwa kuyatekeleza? Sasa hao tuliowakataa ndio mlitaka tukawakabidhi nchi hii tukufu ya Kenya? Wakati hata hawajui mkono wao wa kushoto wala wa kulia ni upi?
 
Kati ya mimi na wewe nani ambaye kichwa chake kina matatizo? Ni wazi kwamba ni wewe, ulieunga mkono wito wa kuinajisi katiba 'yenu' mlioandikiwa na mjerumani 1897 ili Jiwe atawale milele. Katiba ya Kenya hairekebishwi ili kuwanufaisha miungu watu. Hata hakuna aliyeibuka na wazo la kilumumba lumumba kama hilo. Akili za kuazima na hisia za mzuka wa buku saba baki nazo huko huko Tandale.
 
Uwe na mazoea ya kujiongeza bana, unabishana kuhusu marekebisho yatakayofanywa kwenye katiba ya Kenya wakati ufahamu wako wote kuhusu mchakato wenyewe umeutoa kwenye uzi huu wa kiajabu ajabu. Hizo changamoto zote ulizozitaja zitapunguzwa kwa njia kubwa kupitia mapendekezo mengi ambayo wakenya wanataka yawe kwenye kura ya maamuzi. Maoni ya wananchi yatasikizwa kote kote nchini.
 
Mentality ya mwizi wetu, When the opposition was working to remove the corrupt Jubilee ,you voted for your beloved thief..When the opposition now joins the Jubilee to eat together you blame the opposition for supporting the oppressors that are raising taxes. Akili ama kinyesi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…