Haya ya kufanyiwa kazi haraka Simba SC kabla ya kuanza Ligi Kuu na michuano ya CAF

Haya ya kufanyiwa kazi haraka Simba SC kabla ya kuanza Ligi Kuu na michuano ya CAF

Akizungumza kwenye Pre-Meeting ya Watani wa Jadi Simba SC na Yanga SC, Kocha Zaron Maki alisema kuwa amekutana na derby nyingi, huku akiamini kuwa ubora wa wachezaji ndo unaamua mechi kushinda na sio ubora wa mbinu ndani ya uwanja, kwani game kubwa huamuliwa na mambo kama Kona au Free Kick.

Kwangu Ghazwat, hili lilikuwa kosa kubwa sana alifanya Zaron Maki, kwani hapa ni dhahiri ameshindwa kumuheshimu mpinzani wake, ameleta dharau na ndo maana aliamua kuingia na kikosi cha kawaida mno hali iliyosababisha kufungwa kizembe na ndo kilikuwa Kiini hasa cha matokeo.

Kwahivyo ili kuweza kufikia malengo ya timu, Viongozi wa Simba wamwambie Kocha abadilike kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF kuanza, aache dharau na kukariri na mambo ya Morocco, Sudan na Angola, na kwa game dhidi ya Yanga, Nabi ndo ameonekana kuzijua zaidi game za Derby, na amekumbushwa la kufanya.

April 30 2022, niliandika Uzi kuhusu Kocha Pablo Flanco Martin kuwa ni Kocha nzuri sana ila anahitaji wachezaji Quality, hapa ni wachache sana walielewa hii Nukta akiwepo Pettymagambo na Goguryeo asanteni sana nyie Wanamsimbazi

Pablo Flanco ni kocha aliyemsumbua sana Nabi kimbinu ingawa alikuwa na wachezaji wa kawaida, tofauti na sasa, Kocha Nabi ili aweze kumfunga Pablo ilikuwa lazima baadhi ya wachezaji katika kikosi cha Simba kuwa majeruhi, na pia alifanya vizuri Kimataifa kwa matokeo ya ndani na nje hasa game dhidi ya Orlando Pirates.

Kuelekea msimu wa Ligi Kuu na michuano CAF, Simba SC wanahitaji Defensive Midfielder, (DM) na siku zote hakuna mabeki wazuri kama hakuna Defensive Midfielder, Simba SC inahitaji Proper Replacement ya Prime Kanoute.

Haya ndo mambo yakufanya kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF, ili kubaki na mwendo wa ngiri tu meno nje, naona baadhi wengine wamesusa na wakafika mbali zaidi kwamba viongozi waache ngazi, mashabiki waache kwenda uwanjani haya yote sidhani kama ni sahihi kwa sasa, na si afya kwenye medani ya soka, hii ni Simba yetu Nguvu Moja.[emoji881]

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Kwanza mimi napingana na hoja zako zote.

1. Unasema kocha abadilike kwa kufungwa mechi moja tu na Yanga ? Si kweli Zoran aliaproach vizuri sana mechi ya Yanga first half na asingefanya mabadiliko kwenye second half wakati kikosi chake kilicheza vizuri kipindi cha kwanza.
Subs zake alifanya kwa nia njema kabisa ya kwenda kutunza mpira kwa kumuingiza Okwa na Okra alichokosea ni kumtoa Chama akamuacha Sakho, alitakiwa kumtoa Sakho amuache Chama.

2. Unasema Simba wanahitaji DM simba DM wanao zaidi ya watatu kikosini na wote wana quality kuliko timu yoyote ya ligi kuu. Akpan, Kanoute, Mkude na Mzamiru.

3. Unasema Simba wanahitaji replacement ya Prime Kanoute lini Kanoute alikuwa kwenye Prime yake ?

4. Mnataka mashabiki waachie ngazi kwa lipi? Kufungwa na Yanga mechi mbili mfululizo ? Are you serious shabiki wa namna hiyo ni shabiki maandazi and probably ni shabiki mamluki.

5. Anyway umesuggest Simba wamsajili DM wamwache nani waende wakamchukue nani ?
 
Taratibu mnaanza kuelewa maana ya ushabiki. Nimeandika mara nyingi Simba tatizo ni DM nikawa naitwa Utopolo. Labda akiongea mwanasimba atasikilizwa.

Magoli yote mawili juzi si ubovu wa beki Bali ukosefu wa DM kutimiza majukumu yake. Ni yeye aliyeruhusu long distance delivery ya Job, na free role ya Aziz Ki.
Goli la kwanza la Mayele ndiyo kosa la DM ila goli la pili lilikuwa kosa la timu nzima.

Hakuna aliyetrace back kwa strikers kumsumbua Dikson Job,

Kwenye midfield hakuna aliyefanya zone marking.

Defenders hakuna aliyenusa hatari ya mpira ule na kufanya interception in fact the whole team was in shambles.
 
Hii pointi ya kusema kocha aliingia na kikosi dhaifu sio kweli, wale wote ni wachezaji wa Simba SC na lazima waungwe mkono, na wao ndio waliocheza mpira mwingi kipindi cha kwanza tukaenda mapumziko tunaongoza 1-0.

Kipindi cha pili ndio mambo yakabadilika, mbinu alizokuja nazo kocha wa Yanga ndio ziliiua Simba hasa sehemu ya kiungo cha chini Mkude akapotezwa, na sub alizokuja kuzifanya kocha wa Simba SC ndio zikaiua kabisa timu, hapa sioni kama kocha wa Simba aliwadharau Yanga.

Kwangu mimi ile mechi tulipoteza kwa kuzidiwa na mbinu za wapinzani pamoja na uwezo wa wachezaji walionao kutimiza maelekezo wanayopewa na kocha wao, sisi kocha wetu alifanya mabadiliko ambayo hayakuisaidia timu.

Kocha wa Simba SC simlaumu sana, bado namuona ni mpya, hajawafahamu vizuri wachezaji alionao na ajue ni vipi awatumie ili kupata matokeo, hii ni tofauti na Nabi ambaye amekaa na kikosi cha Yanga karibia mwaka wa pili sasa, kocha apewe muda atengeneze timu. Mtu kama Phiri nataka apewe nafasi ya kutosha arudishe match fitness yake bado naamini ubora anao.
Spot on
 
tuache kumlaumu kocha kwa makosa ya viongozi,

kocha alijitahidi sana kulingana na aina ya wachezaji alionao, kosa lake kubwa ni kumtoa chama tu,

huwezi kuwa na malengo makubwa huku umejaza wachezaji aina ya boko, dejan na mkude pale mbele na katikati,

huwezi kuwa na malengo ya kufika nusu final ya caf champions league halafu unashindwa kumchukua striker mkali kwa tsh 400mls, viongozi hawako siriazi,

wakati Uchebe anaondoka alituambia namnukuu "ili simba ipige hatua inahitaji kuwaondoa viongozi wasio na elimu katika bodi" mwisho wa kunukuu.
Ukali wa huyo striker wa Tsh 400 umeujua vipi ?

Kwenye ligi nyepesi kama Uganda alikuwa na 18 goals tu.

Kwenye kikosi cha As Vita hakuwa na maajabu yoyote wewe huo ukali umeuona wapi ?

Simba ina kikosi cha kufunga magoli mengi kuliko hata hitaji la huyo striker.
 
tuache kumlaumu kocha kwa makosa ya viongozi,

kocha alijitahidi sana kulingana na aina ya wachezaji alionao, kosa lake kubwa ni kumtoa chama tu,

huwezi kuwa na malengo makubwa huku umejaza wachezaji aina ya boko, dejan na mkude pale mbele na katikati,

huwezi kuwa na malengo ya kufika nusu final ya caf champions league halafu unashindwa kumchukua striker mkali kwa tsh 400mls, viongozi hawako siriazi,

wakati Uchebe anaondoka alituambia namnukuu "ili simba ipige hatua inahitaji kuwaondoa viongozi wasio na elimu katika bodi" mwisho wa kunukuu.
Viongozi wasio na elimu kwenye bodi aliwalenga kina nani ?

Je mpaka sasa wapo ?
 
Kwa vyovyote vile Kocha alizingua kuanzia Kikosi cha mwanzo mpaka Sub yake, sijui kwa nini Kocha alimuacha Phiri na hata Akpan hakucheza, naendelea kufanya utafiti na nitakuja na majibu soon.

Kuhusu Kocha Nabi kukaa miaka 2 na kikosi ndo maana nikasema kwa Simba wakati ule tulihitaji wachezaji wa kusupport kikosi kilichopo.

Sina maana nadharau baadhi ya wachezaji la hasha, ila mabadiliko kwa wachezaji kuingia na kutoka ni jambo la kawaida.
Kikosi cha mwanzo kilikuwa sawa ndiyo maana kilitawala sehemu kubwa ya mchezo.
 
Kuna kiungo gani pale wa kumfikia sadio kanoute box to box hunter na alivyotoka yeye kati kati palikuwa wazi maana alikuwa anafika katika kwenye hatari kabla yanga hawajaanzisha mashambulizi kawapoteza aucho sure boy na feisal first half sadio kanoute ndio midfielder bora simba kwa sasa sio lazima ukubali.
Nafikiri ile yellow kadi ilipunguza sana ufanisi wake kwa asilimia kubwa.
 
Fraga na Lwanga kazi yao moja tu, ni kukaba na kuharibu mashambulizi, Mkude si Defensive Midfielder ni Holding Midfielder.
Hao watu kina Fraga na Lwanga bado wako kwenye ubora ule ule wa miaka hiyo ?
 
Simba Ina matatizo makuu mawili.
1. Kamati ya usajili.
2. Tactics

1a.TATIZO la Simba sio DM
defensive midifilder.

TATIZO la Simba lipo kwenye kiungo wa kati wa UKABAJI. CDM.
Central defensive midifilder.
Aina ya Thadeo Lwanga,Mafisango Au Bangala,kidogo Kotei na Flaga.

1b. Kanute Akpan Mzamiru ni wakabaji wazuri Sana lakini sio CDM woteni 8. Box to box.
Mkude mkabaji mbovu Sana ni DM

2. KUSHINDWA KUMSAJILI MANZOKI NA KUSHINDWA KUMTUMIA MOSES PHILI.

NILIKUWA WA KWANZA KUANDIKA MZUNGU TUMEPIGWA.
Mafisango hakuwa DM
 
Kwenye game ya michuano ya Azam Sports Federation Cup Jijini Mwanza

Simba waliacha space kubwa sana kati Beki na Viungo kiasi kwamba Feisal alidrible mpira kama mara tatu akiwa free kisha akaachia fataki na hakutokea Kiungo kumkaba wala kuharibu mashambulizi.

Tukisema tunahitaji Kiungo Defensive Midfielder tumeangalia panavuja.
Kanoute hakuwepo ?
 
Kipindi cha Kwanza Yanga walikuwa tumewakamata, Kitendo cha kumtoa mbunifu wa pasi za Magoli yaani Chama na Mkabaji asiyepewa heshima yaani Kanoute ili mkosti Kocha, nafikiri suala la Kocha msaidizi lifikiliwe upya ikiwezekana aondolewe kama tulivyofanya kwa Djuma basi Matola naye amshe tu.
Matola amewakosea nini ?
 
Kwanza mimi napingana na hoja zako zote.

1. Unasema kocha abadilike kwa kufungwa mechi moja tu na Yanga ? Si kweli Zoran aliaproach vizuri sana mechi ya Yanga first half na asingefanya mabadiliko kwenye second half wakati kikosi chake kilicheza vizuri kipindi cha kwanza.
Subs zake alifanya kwa nia njema kabisa ya kwenda kutunza mpira kwa kumuingiza Okwa na Okra alichokosea ni kumtoa Chama akamuacha Sakho, alitakiwa kumtoa Sakho amuache Chama.

2. Unasema Simba wanahitaji DM simba DM wanao zaidi ya watatu kikosini na wote wana quality kuliko timu yoyote ya ligi kuu. Akpan, Kanoute, Mkude na Mzamiru.

3. Unasema Simba wanahitaji replacement ya Prime Kanoute lini Kanoute alikuwa kwenye Prime yake ?

4. Mnataka mashabiki waachie ngazi kwa lipi? Kufungwa na Yanga mechi mbili mfululizo ? Are you serious shabiki wa namna hiyo ni shabiki maandazi and probably ni shabiki mamluki.

5. Anyway umesuggest Simba wamsajili DM wamwache nani waende wakamchukue nani ?
Najibu hoja mbili 4 na 5 hapo kwenye Uzi

Kuhusu mashabiki nimesema kuwa kuna mashabiki wanasusia Timu na kutaka uongozi uachie ngazi, hapo sioni kosa la viongozi maadamu wametimiza wajibu wao kwenye usajili.

Kiungo Defensive Midfielder kwa kumtegemea Mkude na Mzamiru endapo Kanoute akiwa low ni kujidanganya.

Kuna mdau ametoa maoni yake kuwa ikiwa kusajili DM ni ngumu kama kuna Mchezaji anaweza kutengenezwa akawa DM imara, kutafuta mbadala si lazima kusajili, kama Kocha anaona Akpan hatoshi ni kiasi cha kumuweka sawa.
 
Goli la kwanza la Mayele ndiyo kosa la DM ila goli la pili lilikuwa kosa la timu nzima.

Hakuna aliyetrace back kwa strikers kumsumbua Dikson Job,

Kwenye midfield hakuna aliyefanya zone marking.

Defenders hakuna aliyenusa hatari ya mpira ule na kufanya interception in fact the whole team was in shambles.
Sasa si ndo yale tunayozungumza, sijaona unapinga nini kulingana na Comment yako hii.

Uliyosema ndo tumeyasema yaani
 
Back
Top Bottom