Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 21,237
- 31,811
Kwanza mimi napingana na hoja zako zote.Akizungumza kwenye Pre-Meeting ya Watani wa Jadi Simba SC na Yanga SC, Kocha Zaron Maki alisema kuwa amekutana na derby nyingi, huku akiamini kuwa ubora wa wachezaji ndo unaamua mechi kushinda na sio ubora wa mbinu ndani ya uwanja, kwani game kubwa huamuliwa na mambo kama Kona au Free Kick.
Kwangu Ghazwat, hili lilikuwa kosa kubwa sana alifanya Zaron Maki, kwani hapa ni dhahiri ameshindwa kumuheshimu mpinzani wake, ameleta dharau na ndo maana aliamua kuingia na kikosi cha kawaida mno hali iliyosababisha kufungwa kizembe na ndo kilikuwa Kiini hasa cha matokeo.
Kwahivyo ili kuweza kufikia malengo ya timu, Viongozi wa Simba wamwambie Kocha abadilike kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF kuanza, aache dharau na kukariri na mambo ya Morocco, Sudan na Angola, na kwa game dhidi ya Yanga, Nabi ndo ameonekana kuzijua zaidi game za Derby, na amekumbushwa la kufanya.
April 30 2022, niliandika Uzi kuhusu Kocha Pablo Flanco Martin kuwa ni Kocha nzuri sana ila anahitaji wachezaji Quality, hapa ni wachache sana walielewa hii Nukta akiwepo Pettymagambo na Goguryeo asanteni sana nyie Wanamsimbazi
Pablo Flanco ni kocha aliyemsumbua sana Nabi kimbinu ingawa alikuwa na wachezaji wa kawaida, tofauti na sasa, Kocha Nabi ili aweze kumfunga Pablo ilikuwa lazima baadhi ya wachezaji katika kikosi cha Simba kuwa majeruhi, na pia alifanya vizuri Kimataifa kwa matokeo ya ndani na nje hasa game dhidi ya Orlando Pirates.
Kuelekea msimu wa Ligi Kuu na michuano CAF, Simba SC wanahitaji Defensive Midfielder, (DM) na siku zote hakuna mabeki wazuri kama hakuna Defensive Midfielder, Simba SC inahitaji Proper Replacement ya Prime Kanoute.
Haya ndo mambo yakufanya kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF, ili kubaki na mwendo wa ngiri tu meno nje, naona baadhi wengine wamesusa na wakafika mbali zaidi kwamba viongozi waache ngazi, mashabiki waache kwenda uwanjani haya yote sidhani kama ni sahihi kwa sasa, na si afya kwenye medani ya soka, hii ni Simba yetu Nguvu Moja.[emoji881]
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
1. Unasema kocha abadilike kwa kufungwa mechi moja tu na Yanga ? Si kweli Zoran aliaproach vizuri sana mechi ya Yanga first half na asingefanya mabadiliko kwenye second half wakati kikosi chake kilicheza vizuri kipindi cha kwanza.
Subs zake alifanya kwa nia njema kabisa ya kwenda kutunza mpira kwa kumuingiza Okwa na Okra alichokosea ni kumtoa Chama akamuacha Sakho, alitakiwa kumtoa Sakho amuache Chama.
2. Unasema Simba wanahitaji DM simba DM wanao zaidi ya watatu kikosini na wote wana quality kuliko timu yoyote ya ligi kuu. Akpan, Kanoute, Mkude na Mzamiru.
3. Unasema Simba wanahitaji replacement ya Prime Kanoute lini Kanoute alikuwa kwenye Prime yake ?
4. Mnataka mashabiki waachie ngazi kwa lipi? Kufungwa na Yanga mechi mbili mfululizo ? Are you serious shabiki wa namna hiyo ni shabiki maandazi and probably ni shabiki mamluki.
5. Anyway umesuggest Simba wamsajili DM wamwache nani waende wakamchukue nani ?