Haya ya kufanyiwa kazi haraka Simba SC kabla ya kuanza Ligi Kuu na michuano ya CAF

Haya ya kufanyiwa kazi haraka Simba SC kabla ya kuanza Ligi Kuu na michuano ya CAF

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Akizungumza kwenye Pre-Meeting ya Watani wa Jadi Simba SC na Yanga SC, Kocha Zaron Maki alisema kuwa amekutana na derby nyingi, huku akiamini kuwa ubora wa wachezaji ndo unaamua mechi kushinda na sio ubora wa mbinu ndani ya uwanja, kwani game kubwa huamuliwa na mambo kama Kona au Free Kick.

Kwangu Ghazwat, hili lilikuwa kosa kubwa sana alifanya Zaron Maki, kwani hapa ni dhahiri ameshindwa kumuheshimu mpinzani wake, ameleta dharau na ndo maana aliamua kuingia na kikosi cha kawaida mno na kufanya Sub yake ambayo imegharimu timu hali iliyosababisha kufungwa kizembe na ndo kilikuwa Kiini hasa cha matokeo.

Kwahivyo ili kuweza kufikia malengo ya timu, Viongozi wa Simba wamwambie Kocha abadilike kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF kuanza, aache dharau na kukariri na mambo ya Morocco, Sudan na Angola, na kwa game dhidi ya Yanga, Nabi ndo ameonekana kuzijua zaidi game za Derby, na amekumbushwa la kufanya.

April 30 2022, niliandika Uzi kuhusu Kocha Pablo Flanco Martin kuwa ni Kocha nzuri sana ila anahitaji wachezaji Quality, hapa ni wachache sana walielewa hii Nukta akiwepo Pettymagambo na Goguryeo asanteni sana nyie Wanamsimbazi

Pablo Flanco ni kocha aliyemsumbua sana Nabi kimbinu ingawa alikuwa na wachezaji wa kawaida, tofauti na sasa, Kocha Nabi ili aweze kumfunga Pablo ilikuwa lazima baadhi ya wachezaji katika kikosi cha Simba kuwa majeruhi, na pia alifanya vizuri Kimataifa kwa matokeo ya ndani na nje hasa game dhidi ya Orlando Pirates.

Kuelekea msimu wa Ligi Kuu na michuano CAF, Simba SC wanahitaji Defensive Midfielder, (DM) na siku zote hakuna mabeki wazuri kama hakuna Defensive Midfielder, Simba SC inahitaji Proper Replacement ya Prime Kanoute.

Haya ndo mambo yakufanya kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF, ili kubaki na mwendo wa ngiri tu meno nje, naona baadhi wengine wamesusa na wakafika mbali zaidi kwamba viongozi waache ngazi, mashabiki waache kwenda uwanjani haya yote sidhani kama ni sahihi kwa sasa, na si afya kwenye medani ya soka, hii ni Simba yetu Nguvu Moja.[emoji881]

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
 
Taratibu mnaanza kuelewa maana ya ushabiki. Nimeandika mara nyingi Simba tatizo ni DM nikawa naitwa Utopolo. Labda akiongea mwanasimba atasikilizwa.

Magoli yote mawili juzi si ubovu wa beki Bali ukosefu wa DM kutimiza majukumu yake. Ni yeye aliyeruhusu long distance delivery ya Job, na free role ya Aziz Ki.
 
Hii pointi ya kusema kocha aliingia na kikosi dhaifu sio kweli, wale wote ni wachezaji wa Simba SC na lazima waungwe mkono, na wao ndio waliocheza mpira mwingi kipindi cha kwanza tukaenda mapumziko tunaongoza 1-0.

Kipindi cha pili ndio mambo yakabadilika, mbinu alizokuja nazo kocha wa Yanga ndio ziliiua Simba hasa sehemu ya kiungo cha chini Mkude akapotezwa, na sub alizokuja kuzifanya kocha wa Simba SC ndio zikaiua kabisa timu, hapa sioni kama kocha wa Simba aliwadharau Yanga.

Kwangu mimi ile mechi tulipoteza kwa kuzidiwa na mbinu za wapinzani pamoja na uwezo wa wachezaji walionao kutimiza maelekezo wanayopewa na kocha wao, sisi kocha wetu alifanya mabadiliko ambayo hayakuisaidia timu.

Kocha wa Simba SC simlaumu sana, bado namuona ni mpya, hajawafahamu vizuri wachezaji alionao na ajue ni vipi awatumie ili kupata matokeo, hii ni tofauti na Nabi ambaye amekaa na kikosi cha Yanga karibia mwaka wa pili sasa, kocha apewe muda atengeneze timu. Mtu kama Phiri nataka apewe nafasi ya kutosha arudishe match fitness yake bado naamini ubora anao.
 
Hii pointi ya kusema kocha aliingia na kikosi dhaifu sio kweli, wale wote ni wachezaji wa Simba SC na lazima waungwe mkono, na wao ndio waliocheza mpira mwingi kipindi cha kwanza tukaenda mapumziko tunaongoza 1-0...
Paragraph yako ya mwisho ndo inarejea yote niliyoandika hapo kwenye Uzi, ndo mambo yote mkuu denooJ
 
Wakati wa uchebe tulicheza mpira mzuri sana. Kumiliki mpira wakati wote. Sasa hivi hilo limebaki kuwa ni suala la vipindi. Mara tunakuwa tunamiliki,Mara pasi fupi,Mara pasi ndefu,Mara mpira wa kasi,Mara taratibu,wakati mwengine tunabutuatua n.k Hatuna formation kamili.
 
Wakati wa uchebe tulicheza mpira mzuri sana. Kumiliki mpira wakati wote. Sasa hivi hilo limebaki kuwa ni suala la vipindi. Mara tunakuwa tunamiliki,Mara pasi fupi,Mara pasi ndefu,Mara mpira wa kasi,Mara taratibu,wakati mwengine tunabutuatua n.k Hatuna formation kamili.
Ule uamuzi wa kumfukuza uchebe kwangu bado naona ndio chanzo cha haya majanga yote yanayotukuta kwa sasa.

Kila mara kubadilisha makocha kabla hawajatengeneza timu, matokeo yake ndio haya ni vipigo mfululizo toka kwa wale tuliokuwa tumewaweka mfuko wa nyuma enzi za uchebe.
 
tuache kumlaumu kocha kwa makosa ya viongozi,

kocha alijitahidi sana kulingana na aina ya wachezaji alionao, kosa lake kubwa ni kumtoa chama tu,

huwezi kuwa na malengo makubwa huku umejaza wachezaji aina ya boko, dejan na mkude pale mbele na katikati,

huwezi kuwa na malengo ya kufika nusu final ya caf champions league halafu unashindwa kumchukua striker mkali kwa tsh 400mls, viongozi hawako siriazi,

wakati Uchebe anaondoka alituambia namnukuu "ili simba ipige hatua inahitaji kuwaondoa viongozi wasio na elimu katika bodi" mwisho wa kunukuu.
 
Nimeongeza nyingine ya mwisho kabisa inayotoa majibu kwa yote niliyoandika pale juu.
Kwa vyovyote vile Kocha alizingua kuanzia Kikosi cha mwanzo mpaka Sub yake, sijui kwa nini Kocha alimuacha Phiri na hata Akpan hakucheza, naendelea kufanya utafiti na nitakuja na majibu soon.

Kuhusu Kocha Nabi kukaa miaka 2 na kikosi ndo maana nikasema kwa Simba wakati ule tulihitaji wachezaji wa kusupport kikosi kilichopo.

Sina maana nadharau baadhi ya wachezaji la hasha, ila mabadiliko kwa wachezaji kuingia na kutoka ni jambo la kawaida.
 
tuache kumlaumu kocha kwa makosa ya viongozi,

kocha alijitahidi sana kulingana na aina ya wachezaji alionao, kosa lake kubwa ni kumtoa chama tu...
Kocha Zaron anapaswa kubadilika, kama umeona ni kosa kumtoa Chama, halafu Timu ikapwaya ndo vile vile amekosea kuanza na kikosi chake cha kawaida mno na kuwaacha akina Kapombe na Phiri na Akpan.

Kuna baadhi ya game hupaswi kujaribu Wachezaji mkuu.
 
tuache kumlaumu kocha kwa makosa ya viongozi,

kocha alijitahidi sana kulingana na aina ya wachezaji alionao, kosa lake kubwa ni kumtoa chama tu...
Tumefungwa derby mara mbili mfululizo viongozi hawashituki, wanatujazia wachezaji wasio na msaada huyo kapama alisajiliwa Kwa akili ya nini, gadiel aliongezwa mkataba Kwa ajili ya nini
 
Tumefungwa derby mara mbili mfululizo viongozi hawashituki, wanatujazia wachezaji wasio na msaada huyo kapama alisajiliwa Kwa akili ya nini, gadiel aliongezwa mkataba Kwa ajili ya nini
inaumiza sana, halafu haitoshi kiongozi huyohuyo anayetusajilia kapama na dejan ndio huyo huyo anataka kumuuza sakho!

na huyohuyo anataka timu ifike nusu final ya caf champions league,

daah! salaaale.
 
Kwa upande wako viongozi hawana tatizo?
Viongozi wametimiza wajibu wao kuleta wachezaji wazuri, kama walifanya kosa kumfukuza Pablo lakini kwenye usajili wanajitahidi kadri ya uwezo wao.

Kocha Zaron Maki abadilike, sijasema Kocha mbaya, bali mbinu yake dhidi ya wapinzani haikuwa na athari yoyote Uwanjani.
 
Kama kikosi kilichoanza kilikuwa dhaifu, ilikuwaje sasa kikapata goli la kuongoza dakika ya 16 tu! Na pia kuumiliki mchezo kwa kipindi chote cha kwanza?
Kwani kupata goli dakika ya 16 ndo nini, mbona unaweza kumiliki mchezo na ukapoteza vile vile, na kwanini halijadumu hadi kumalizika kwa mchezo.

Mpira ni dakika 90, na pale haikuwa game dhidi Lipuli ya Iringa kwamba unaweza kutanguliwa na wasisawazishe.
 
unapiga gitaa kwa mbuzi, la kuzuia mashabiki na wachawi tu kuhudhuria mazoezi na kuyarekodi kwa simu kule bunju wamelishindwa sembuse hayo unayosema
Acheni hizi imani zenu potofu, kama kweli walituibia mbinu mbona kipindi cha kwanza tulicheza Simba SC na goli tukapata?

Tujifunze kukubali matokeo, hata wakifanyia mazoezi mwezini ukizidiwa mbinu na mwenzako utapigwa tu.
 
Back
Top Bottom