Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Kwamba Waziri anaitia serikali hasara kubwa, na nchi uzorotaji wa kimaendeleo ya teknolojia na ya watu... anaoteshwa, anabadilisha, na anaendelea na kazi!
Kabla ya tozo, sekta ya 'fedha mtandaoni' (mobile money) ilikadiriwa kuwa dola bilioni 4 (Shilingi Trilioni 9.5), kiasi ambacho kwa mwaka kilikadiriwa kufikia dola bilioni 45! Tanzania ilikuwa katika 10 bora Afrika katika sekta hii ya 'Mobile money' hata kuipita Kenya.
Kiasi hicho (ikiwa bado twangojea takwimu) kinakadiriwa kushuka kwa asilimia 70 baada ya tozo, na chaji za kutoa pesa benki; kiasi kwamba watu wengi waliamua kuweka pesa chini ya mto, kuzichimbia au ndani ya mitungi, na wale wa kutuma walitumia mabasi, boda boda au baiskeli kuwatumia ndugu zao vijijini!
Vijana wengi walikosa ajira kwa kitendo hicho cha 'kibahau'. Kumbuka asilimia 30% takriban ya Watanzania huishi chini ya kiwango cha ufukara yaani chini ya sh. 2300 kwa siku (dola moja). Tanzania ikaachwa nyuma katika vuguvugu la huduma za 'bila sarafu' (paperless money).
Katika nchi kadhaa za Afrika si lazima tena kulipia huduma kama kununua nyama bucha, au chai mgahawani, nguo sokoni....kwa kutoa pesa taslimu, inatosha kutumia simu tu. Siyo kwetu!
Tozo pia zimeathiri vibaya biashara ya mtandaoni kiasi kwamba wataalamu wanasema, Jibuti na Somalia zinafanya biashara ya mtandaoni zaidi kuliko Tanzania!
Si kuwa serikali haikuwa inapata pesa kupitia simu kabla ya tozo, la, bado kuna VAT 18% na malipo ya kutoa pesa 10% Ni kutojali tu na kuona binafsi hahusiki!
Fast forward: Waziri aoteshwa! Kwamba tozo zina madhara makubwa kwa uchumi, na kwamba watu wameanza kukasirika, na hapo anaamua kuziondoa, na anabaki na kazi yake!
Wapi kwengine duniani katika karne ya 21 Waziri kama huyo anaweza kuendelea na kazi yake? Moja ya masuala kipaumbele kabisa kwa kiongozi yeyote kabla ya kufanya uamuzi anapima athari zake kiuchumi, kijamii na hata ki-jina, sifa, utajo (reputation).
Ndiyo maana hata mimi nadai Katiba mpya haraka, maana hii itaondoa madaraka ya rais kumchagua amtakaye kwa sababu ima za kichama, kujikomba au sura! Bunge litakuwa ndilo lenye kauli ya mwisho baada ya uchambuzi wa kina wa elimu, uzoefu na rekodi zake huko nyuma.
Ni hapo tu ndipo tutakuwa na sera mustakim za uchumi.
Ili niwe mwadilifu, hapa naomba wale wenye taarifa zaidi za performance ya Waziri wa Fedha wataje mazuri aliyoyafanya katika kipindi chake fauka ya blunder hii ya tozo.