Haya yanayotokea st Joseph College sio uvunjaji wa haki za wanafunzi?

muhogomchungu

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2011
Posts
375
Reaction score
3
Hichi chuo kilichopo Mbezi, st joseph

1)Uchaguzi wa wanafunzi kuchagua rais wao, mawakala, wenyeviti wa tume ya uchaguzi walikuwa walimu wa chuo (wahindi) na sio wanafunzi.
2) Huruhusiwi kwenda Kujisaidia ukiwa ktk Chumba cha EXAM, japo ukotoke hapa hapo.
3) Ada kubwa sana kupita kiasi inawalazimu wanafunzi kutoa pesa mifukoni kukamilisha ada baada ya 100% ya bodi ya mikopo kutokamilisha ada
4)Pesa ya Stationary uitumie Chuoni, vitabu na madafatari gali sana vyenginevyo utakuwa umekiuka Sheria
5)Hamna mapumziko, akitoka lecture kaingia mwengine. kama hayupo basi anaingia Lecture mwengine kusimamia eti pasitokee zogo. hadi saa za kula.
 
Poleni vijana hii ndo bongo!Naamin mkiamua kudai haki zenu mtapata!msiogo hao wahindi!they hav nothng 2do wth xul govt.!!nyie ndo mnahaki kuchagua viongozi wenu!!komaeni ndugu huku mkisali sana si chuo cha dini hicho!!?GOD wil help u!
 
Mimi napendekeza ingeundwa ewura ya ku- control tuition fees. Thanks to the open university. Tuition fees ni 360,000 tu
 
Poleni jamani.
Haki haiombwi inadaiwa. STUKA.
 
Duhh! inategemea unasoma kozi gani mdau. Nakumbuka nilipokuwa UDSM - (FOE kwa wakati huo) kila jioni nilikuwa nameza vidonge vya kupunguza maumivu hasa ya kichwa. Mwaka wa kwanza ulikuwa umebana sana. Ilikuwa ni bandika bandua. Ndo system ya elimu duniani kwa upande wa Engineering.

Ukitaka elimu bora ni lazima ukubari gharama kubwa. Ebu angalia vyuo vikuu vya maana duniani kisha uone karo zao!! Ukitaka ukombozi wa kielimu na uwe na uwezo wa uelewa wa unachokifanya basi kubali kulipia gharama kubwa. Mzee, ukiona vyaelea vimeundwa.... Hakuna kizuri kisicho na gharama!! Ukitaka elimu ya bora liende basi jaribu vyuo vingine huko India, OUT n.k

Nasikitika kuwa unaweza usinielewe ninachosema ila mimi kama mdau na mwalimu katika chuo kikuu nje ya Tanzania ninauzoefu mkubwa sana na gharama za masomo. Ebu jaribu kufanya publication moja tu kwenye international journals... itakugharimu si chini ya dola 50,000 kwa utafiti na uandaaji. Mwalimu anatakiwa atoe angalau article 2 kila mwaka ...... piga mahesabu ni kiasi gani chuo kinatakiwa kugharamia!! Well, sijui system za Chuo chenu ila kizuri kinagharama!
 
  • Thanks
Reactions: mka
Hiyo ya kutokupumzika naipinga kwa nguvu zote,nipo chuo mwaka wa pili nachukua computing(UK not bongo),lecture ni masaa mawili,baada ya dakika 50 au lisaa limoja lazima mpate break ya dakika 10 mpaka 15.na ikitokea lecturer akaunganisha bila ya kuwapa break,ujue hatomaliza masaa mawili,lazima atafanya kwasaa moja na nusu,zimezidi sana 45.na kama ikatokea lecturer hayupo basi kila mtu anashika hamsini zake,wanaokwenda library wanakwenda, wanao kwenda nyumbani wanakwenda. na kama ikatokea vipindi vikafuatana basi si zaidi ya vipindi viwili, kwahiyo kipindi cha tatu lazima kuwe na gap la masaa mawili mpaka manne.
 
Sioni cha kulalamika, nivema uchukulie kama changamoto, kutoa mafunzo ya sayansi ni garama huwezi linganisha na fani nyingine, swala la hampumziki badala ya kufurahia unalalamika? Kwa taifa changa kama Tanganyika vijana mnatakiwa mjitahidi, kulalamika kumepitwa na wakati.Naamini kwa hiyo hali ukiweza kumaliza utaweza kufanya kazi sehemu yeyote duniani,,,,,,,nikijaribu kulinganisha shule tulizopitia sisi na unachokilalamikia naona kama unafanya mchezo kabisa,, shukuru Mungu hao walimu wapo na wanajituma kufundisha, nivema ukakaa bila simu hakiksiha unanunua vitabu, laptop hizo ni kama jembe kwa mwanafunzi,,

wakati unalalamika ni vema ungejiuliza India ilipata Uhuru 1940 wamewezaje au walifanya nini mpaka wakaweza kufikia maendelea waliyonayo sasa mpaka wakaweza kuja kuwajengea chuo, Waliwekeza katika elimu, na watu wanajituma wanawajibika,,kijana its better to think big badala ya kulalamika
 
Duhh!

Ukitaka elimu bora ni lazima ukubari gharama kubwa. Ebu angalia vyuo vikuu vya maana duniani kisha uone karo zao!! Ukitaka ukombozi wa kielimu na uwe na uwezo wa uelewa wa unachokifanya basi kubali kulipia gharama kubwa. Mzee, ukiona vyaelea vimeundwa.... Hakuna kizuri kisicho na gharama!! Ukitaka elimu ya bora liende basi jaribu vyuo vingine huko India, OUT n.k

Naona unaiponda OUT kwa nguvu.
 
Hiyo ya kutokupumzika naipinga kwa nguvu zote,nipo chuo mwaka wa pili nachukua computing ...,lecture ni masaa mawili,baada ya dakika 50 au lisaa limoja lazima mpate break ya dakika 10 mpaka 15.
Yeah, computing, sio Engineering!
 
kwa upande wangu naona kama wamepunguza sheria sasa ivi. sisi tuliozindua ndo ilikuwa balaa
 
Hichi chuo kilichopo Mbezi, st joseph

1)Uchaguzi wa wanafunzi kuchagua rais wao, mawakala, wenyeviti wa tume ya uchaguzi walikuwa walimu wa chuo (wahindi) na sio wanafunzi.
2) Huruhusiwi kwenda Kujisaidia ukiwa ktk Chumba cha EXAM, japo ukotoke hapa hapo.
3) Ada kubwa sana kupita kiasi inawalazimu wanafunzi kutoa pesa mifukoni kukamilisha ada baada ya 100% ya bodi ya mikopo kutokamilisha ada
4)Pesa ya Stationary uitumie Chuoni, vitabu na madafatari gali sana vyenginevyo utakuwa umekiuka Sheria
5)Hamna mapumziko, akitoka lecture kaingia mwengine. kama hayupo basi anaingia Lecture mwengine kusimamia eti pasitokee zogo. hadi saa za kula.

Safi sana St. Joseph wanafunzi wa bongo wavivu sana wanataka kila muda wapige story za Man U, Arsenal na Barcelona. Pigeni hivyo hivyo bandika bandua. Hamna tatizo lolote ili wajue mafanikio ya elimu yaliyopo India hayakuja kwa kushuka toka mbinguni!
 
Duhh! inategemea unasoma kozi gani mdau. Nakumbuka nilipokuwa UDSM - (FOE kwa wakati huo) kila jioni nilikuwa nameza vidonge vya kupunguza maumivu hasa ya kichwa. Mwaka wa kwanza ulikuwa umebana sana. Ilikuwa ni bandika bandua. Ndo system ya elimu duniani kwa upande wa Engineering.

Ukitaka elimu bora ni lazima ukubari gharama kubwa. Ebu angalia vyuo vikuu vya maana duniani kisha uone karo zao!! Ukitaka ukombozi wa kielimu na uwe na uwezo wa uelewa wa unachokifanya basi kubali kulipia gharama kubwa. Mzee, ukiona vyaelea vimeundwa.... Hakuna kizuri kisicho na gharama!! Ukitaka elimu ya bora liende basi jaribu vyuo vingine huko India, OUT n.k

Nasikitika kuwa unaweza usinielewe ninachosema ila mimi kama mdau na mwalimu katika chuo kikuu nje ya Tanzania ninauzoefu mkubwa sana na gharama za masomo. Ebu jaribu kufanya publication moja tu kwenye international journals... itakugharimu si chini ya dola 50,000 kwa utafiti na uandaaji. Mwalimu anatakiwa atoe angalau article 2 kila mwaka ...... piga mahesabu ni kiasi gani chuo kinatakiwa kugharamia!! Well, sijui system za Chuo chenu ila kizuri kinagharama!
india wamepiga hatua kubwa sana kielimu dunia haswa ktk udaktari, uchumi,sayansi ya kompyuta na mawasiliano. Wangonjwa wengi toka ulaya na america wanaenda india kutibiwa kwa garama nafuu na matibabu ya hali ya juu. Wataalamu wengi wa kompyuta na uchumi toka india wanafanya kazi america na ulaya kwahiyo mkuu india sio ya kubeza hata kidogo. OUTsawa na kukubalia maana vyuo vya tanzania vinafundisha uwe na uwezo wa kukariri( kopi na kupesti) ili mradi umefaulu na kupata cheti basi yameisha. Havifundishi uwezo wa kuwa mbunifu kisayansi na kutumia elimu kuleta maendeleo kwa taifa.Miaka imepita 50 hakuna kitu nchi bado inatambaa kimaendeleo ndio maana nyinyi mumekwenda nje ya nchi kuongeza elimu ambayo ndio inadhamani kwa karne ya 21
 
5)Hamna mapumziko, akitoka lecture kaingia mwengine. kama hayupo basi anaingia Lecture mwengine kusimamia eti pasitokee zogo. hadi saa za kula.

Vipi jamani hata walimu wakiingia darasani mnalalamika?mimi nimezoea kusikia malalamiko ya walimu kutokuingia darasani,this is very strange to me!!
 
Bora dar, cha songea ndo uwozo kabisa. Kilifanya niwachukie wahindi kabisa. Mfano ukiwa mwanafunzi ktk hiki chuo hauruhusiwi kuwa mwanachama wa siasa. Mbwa kabisa hawa.
 
Hichi chuo kilichopo Mbezi, st joseph

1)Uchaguzi wa wanafunzi kuchagua rais wao, mawakala, wenyeviti wa tume ya uchaguzi walikuwa walimu wa chuo (wahindi) na sio wanafunzi.
2) Huruhusiwi kwenda Kujisaidia ukiwa ktk Chumba cha EXAM, japo ukotoke hapa hapo.
3) Ada kubwa sana kupita kiasi inawalazimu wanafunzi kutoa pesa mifukoni kukamilisha ada baada ya 100% ya bodi ya mikopo kutokamilisha ada
4)Pesa ya Stationary uitumie Chuoni, vitabu na madafatari gali sana vyenginevyo utakuwa umekiuka Sheria
5)Hamna mapumziko, akitoka lecture kaingia mwengine. kama hayupo basi anaingia Lecture mwengine kusimamia eti pasitokee zogo. hadi saa za kula.
Ukiona elimu ni ghari.........basi JARIBU UJINGA ................. na hapo ndo utaona how cheap the education is............
 
Bora dar, cha songea ndo uwozo kabisa. Kilifanya niwachukie wahindi kabisa. Mfano ukiwa mwanafunzi ktk hiki chuo hauruhusiwi kuwa mwanachama wa siasa. Mbwa kabisa hawa.
Waulize wenzio wa YU-DOMU............... walijifanya wana CCM sasa wanakoma........... ni bora hao wanaowaonyesheni njia mapema............
 
Safi sana St. Joseph wanafunzi wa bongo wavivu sana wanataka kila muda wapige story za Man U, Arsenal na Barcelona. Pigeni hivyo hivyo bandika bandua. Hamna tatizo lolote ili wajue mafanikio ya elimu yaliyopo India hayakuja kwa kushuka toka mbinguni!
You have said it all.................. Halafu ananishangaza huyu jamaa .....eti analalama bandika bandua.............. aende shule za kata akaone kusivyo na bandika bandua na jinsi walivyo nyuma kielimu.................. UMEAGA KWENU UNAKWENDA SHULE KUSOMA...........SOMA BANA.
 
Bora dar, cha songea ndo uwozo kabisa. Kilifanya niwachukie wahindi kabisa. Mfano ukiwa mwanafunzi ktk hiki chuo hauruhusiwi kuwa mwanachama wa siasa. Mbwa kabisa hawa.
....du mbwa tena!!!
 
Back
Top Bottom