Haya yote aliyofeli Rais Magufuli ni madogo sana, mradi wa Stiglers Gorge ndiyo utakuwa tsunami kwenye kushindwa!

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Sijui ilianza sukari, uhakiki, kodi za hovyo, makinikia, mbaazi, korosho, ndege vyote hivyo Rais wetu anashindwa vibaya sana na hii ni kutokana na one man show.

Ngoja niwapeni kuhusu mbaazi. Aliyekuwa msambazaji mkuu wa zao hilo kule kwa wahindi alikuwa Yusuph Manji. Serikali ikampiga stop kisha waziri wa kilimo akaenda huko kudai kuwa sasa atakayekuwa msambazaji mkuu wa mbaazi kwao ni serikali ya Tanzania badala ya Yusuph Manji. Akajibiwa kama ni hivyo basi hata hizo mbaazi zenu hatuzitaki tena. Soko likaenda shimoni.

Kaenda kwenye makinikia kisha sasa wanatoa kinyemela kupeleka Japan kusafisha. Matokeo yake mategemeo yao yamekuwa sifuri na imekuja hasara ya kufa mtu.

Rais Magufuli amefeli kila jambo. Sasa kuna mradi mmoja huko nyanda za juu wa umeme unaojulikana kama Stiglers Gorge. Huu mradi kwanza huo umeme tunaoambiwa kuwa tutapata hautofikia hata nusu yake. Mradi ukikamilika pamoja na kutumia fedha nyingi sana za ndani (maana nje tumenyimwa) utaenda kuwa msiba kwa mazingira, hasara ya mradi husika na hatimaye utatuletea umeme wa kusuasua. Tusubiri tuone! Wapi amewahi kufanikiwa? Mbona wenzake wote hawakuthubutu kuugusa? Si ulikuwepo? Haya tuone ila hajawahi kufanikiwa.

Ngoja niishie hapo maana mtu unaweza kula kifungo cha maisha jela kutokana na uhochezi na hakimu akapewa "promosheni" mchana peupeeee! Mambo ni vululu vululu ukiugusa utawala na dola ni kifungo cha kufa mtu.
 
Kuna watu wanauliza ukweli wa gharama au umeme utakaozalishwa na mradi huu kwa kuutazama mradi wa Rusumo ambapo.$468million zitazalisha megawatts 80 tu
 
yaani wamisri watoke makwao waache wake zao waje kujenga mradi utakaofeli...


chadema hamjui mnachotaka.. mmeishia kupinga kila kitu..

reliii ilee imeshaaamka.... haya umeme nao huooooo unakujaaaaa
 
JPM amebakiza miaka 7 ya kutawala Tz.
Muhimu jitahidini thread za JPM ziwe fupifupi maana miaka 7 ni mingi mnaweza pumzi ikakata

Sent using Jamii Forums mobile app
Waliambiwa hii ni nguvu ya gongo sio ya mirinda wala pepsi, wakabisha. Sasa walichobakiwa nacho ndio huu uwezo wa kuanzisha threads zisizo na kichwa wala miguu.

Huyu Ngosha tunae mpaka 2025 iwapo Mungu atatupa uhai.
 
yaani wamisri watoke makwao waache wake zao waje kujenga mradi utakaofeli...


chadema hamjui mnachotaka.. mmeishia kupinga kila kitu..

reliii ilee imeshaaamka.... haya umeme nao huooooo unakujaaaaa
Hawa wanapoteza muda, wanabakia kuwadanganya watu ambao hawawezi kufikiria mambo kwa kina.
 
First US$340 million project under the Great Lakes Regional Initiative

WASHINGTON, August 6, 2013 – The World Bank’s Board of Executive Directors today approved US$340 million for the Regional Rusumo Falls Hydroelectric Project which aims to benefit people in Burundi, Rwanda and Tanzania. This project is the first operation under the World Bank Group Great Lakes Regional Initiative inaugurated by World Bank Group President Jim Yong Kim during his historic joint visit with UN Secretary General Ban Ki-moon in May 2013.

The overall project cost is US$468.60 million and its eventual 80 megawatt generation capacity will boost reliable power supply to the electricity grids of Burundi, Rwanda and Tanzania, reduce electricity costs, promote renewable power, spur job-led economic development and pave the way for more dynamic regional cooperation, peace and stability among the countries of the Nile Equatorial Lakes (NEL) sub-region in east Africa.

Hii ilikuwa ni press release ya World Bank
Mkuu hii taarifa una Uhakika nayo?
Maana $468= 900 Billion Tsh hivi, Au Zaidi au Trillion 1.
Duuu...Let's wait kwanza Mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…