Haya yote aliyofeli Rais Magufuli ni madogo sana, mradi wa Stiglers Gorge ndiyo utakuwa tsunami kwenye kushindwa!

Haya yote aliyofeli Rais Magufuli ni madogo sana, mradi wa Stiglers Gorge ndiyo utakuwa tsunami kwenye kushindwa!

Kilaza vipi,,Jiwe alferi kama ulivyoomba na chadema Yako au umebadili mawazo
Wewe mburula ngumbaru jifunze kuandika kwa herufi sahihi kabla ya kuninukuu.

Halafu ondoka katika Uushuzi wa one track mind ya kufikiri kwamba kila anayemsema Magufuli ni CHADEMA.

Jiwe hatuna muda wa kumsema, tumewaachia hiyo kazi CCM wenzake kina January Makamba
 
80MGW kwa gharama zote hizo mmmmmh kumbe sasa 2100MGW ni lundo la hela kwa sababu

80MGW~1tr
2100MGW~? crossmultplication

(2100MGW×1tr)÷80MGW=26.25trillions mmmh sio poa
Katumia 6 trillion
 
Wewe mburula ngumbaru jifunze kuandika kwa herufi sahihi kabla ya kuninukuu.

Halafu ondoka katika Uushuzi wa one track mind ya kufikiri kwamba kila anayemsema Magufuli ni CHADEMA.

Jiwe hatuna muda wa kumsema, tumewaachia hiyo kazi CCM wenzake kina January MakambaView attachment 2930483
Sasa huyo ndio source? What if Anamchafua?
 
Sasa huyo ndio source? What if Anamchafua?
Huyu ndiye aliyesema hivi karibuni tu, haya yalisemwa miaka mingi ila yalionekana maneno ya wapinzani tu, sasa hivi mpaka CCM wenyewe wanakubali.

Jiwe hahitaji mtu wa kumchafua, alikuwa anajichafua mwenyewe hata kwa kauli zake za waziwazi.

Tatizo Tanzania ni nchi ya low standards.
 
Humu watu hushabikia kama mazuzu tu.

Mradi unapeta kwa sasa wanataka maua apewe huyu at aliukuta upo 30% ila ungebuma hizi nyuzi ndiyo zingekuwa rejea.
Sifa za jiwe ni kuthubuthu na kuweka mipango ya fedha itakapopatikana kwa kushirikiana na Dr mpango by then alikiwa wazir wa fedha
 
STIGLERS GORGE ni Big Time Failure kwa Tanzania na qa

waathirika ni vizazi vijavyo katika kulipa deni. Shida ni kwamba anayefanya maamuzi ana uelewa finyu wa mambo halafu anafanya maamuzi ya mambo makubwa kiuchumi na kijamii. Imefika wakati hata wasaidizi wake wasomi na degrees zao wamebaki kusifia tu sawa na wale ambao hawajasoma.
Katika miradi yote mradi utakaotutia umaskini vizazi na vizazi ni huo wa Stiglers Gorge. Bila kuzingatia sababu za WWF kuhusu kuvuruga ecosystems na World Heritage site kuna sababu 3 za nguvu kwa nini Stiglers Gorge ni wastage of money kwa nchi ya Tanzania; (1) Maji yapatayo 36% yaliyokuwapo mwaka 1980 wakati feasibility study ilifanyika sasa hivi hayapo (2) Umeme wa kutegemea maji siyo wa kuaminika kwenye karne hii kutokana na mabadiliko ya tabia nchi (3) Hata Mtera na Kihansi zilipojengwa miaka ya 1980s na 1990s tuliambiwa zingekuwa ni suluhisho la umeme lakini zimeahindwa. Lakini tunaambiwa bwawa linajaa matope hivyo hata kimo cha maji kinakuwa kidogo.
(4) Kuna ongezeko kubwa la watu wanaoishi pembezoni mwa mto unakoanzia na unakopita hivyo basi kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu kama kilimo na mifugo.

Kweli Baba wa Taifa ndiye muasisi na mbunifu wa mradi wa Stiglers Gorge lakini hata kama angekuwa hai kufika leo angebadili mawazo ya utekelezaji kwa vile alikuwa ana shaurika.

Tutajenga Stigler Gorge kwa bei mara 3 ya hiyo wanayoitaja na hatuwezi kupata hizo Megawati 2100. Tutaendelea kulipa mkopo kutoka kwa nchi wahisani tulizokopa vizazi na vizazi.
Huyu Mbweha Bado ana ujuha huu!?
 
Humu watu hushabikia kama mazuzu tu.

Mradi unapeta kwa sasa wanataka maua apewe huyu at aliukuta upo 30% ila ungebuma hizi nyuzi ndiyo zingekuwa rejea.
Liliwaka jua kali mwaka jana 2023 wakasema sababu ya kuharibu mazingira kwenye JKNHP kule Selous mloka.
Hawajui climatology ya nchi yao ukame hutokea miaka miwili mfululizo mwaka wa tatu inakuja mfuata nyingi sana. Ni recurring events.
 
Huyu ndiye aliyesema hivi karibuni tu, haya yalisemwa miaka mingi ila yalionekana maneno ya wapinzani tu, sasa hivi mpaka CCM wenyewe wanakubali.

Jiwe hahitaji mtu wa kumchafua, alikuwa anajichafua mwenyewe hata kwa kauli zake za waziwazi.

Tatizo Tanzania ni nchi ya low standards.
Duh! Sawa mzee
 
Nani ame-fail kati yako na Magufuli?
Muda ndiyo mwalimu mzuri.
Tuweke akiba ya maneno.
 
Hii ni Ile ya rusumo ila ya rufiji ya meg wat 2160 ndo trillion 6
Nilikua nasema Rufiji katumia hizo tuko sawa. Na alitumia wakandarasi wa kiafrika, probably aliona ndio wanaweza kwa bei tajwa.

Ila nchi inachekesha bana, vimegawati miambili tunaomba mkopo ila Elf 2, tunachukua domestic revenue.
 
Sijui ilianza sukari, uhakiki, kodi za hovyo, makinikia, mbaazi, korosho, ndege vyote hivyo Rais wetu anashindwa vibaya sana na hii ni kutokana na one man show.

Ngoja niwapeni kuhusu mbaazi. Aliyekuwa msambazaji mkuu wa zao hilo kule kwa wahindi alikuwa Yusuph Manji. Serikali ikampiga stop kisha waziri wa kilimo akaenda huko kudai kuwa sasa atakayekuwa msambazaji mkuu wa mbaazi kwao ni serikali ya Tanzania badala ya Yusuph Manji. Akajibiwa kama ni hivyo basi hata hizo mbaazi zenu hatuzitaki tena. Soko likaenda shimoni.

Kaenda kwenye makinikia kisha sasa wanatoa kinyemela kupeleka Japan kusafisha. Matokeo yake mategemeo yao yamekuwa sifuri na imekuja hasara ya kufa mtu.

Rais Magufuli amefeli kila jambo. Sasa kuna mradi mmoja huko nyanda za juu wa umeme unaojulikana kama Stiglers Gorge. Huu mradi kwanza huo umeme tunaoambiwa kuwa tutapata hautofikia hata nusu yake. Mradi ukikamilika pamoja na kutumia fedha nyingi sana za ndani (maana nje tumenyimwa) utaenda kuwa msiba kwa mazingira, hasara ya mradi husika na hatimaye utatuletea umeme wa kusuasua. Tusubiri tuone! Wapi amewahi kufanikiwa? Mbona wenzake wote hawakuthubutu kuugusa? Si ulikuwepo? Haya tuone ila hajawahi kufanikiwa.

Ngoja niishie hapo maana mtu unaweza kula kifungo cha maisha jela kutokana na uhochezi na hakimu akapewa "promosheni" mchana peupeeee! Mambo ni vululu vululu ukiugusa utawala na dola ni kifungo cha kufa mtu.
Mwisho wa siku umeonekana mjinga
 
Back
Top Bottom