Hayati Dkt. Magufuli aliwahi kusema hata CCM kulikuwa na mafisadi wakubwa

Hayati Dkt. Magufuli aliwahi kusema hata CCM kulikuwa na mafisadi wakubwa

Kijogoodi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
1,362
Reaction score
2,373
Kwa kauli alizozitoa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza jana kwenye kipindi cha Star TV Big Agenda bila shaka ni kweli kabisa ndani ya CCM kulikuwa na mafisadi ya kutisha na Magufuli aliyabananga vizuri na sasa yameanza kupata nafuu mbele ya rais Samia.

Ikumbukwe baada tu ya kuingia madarakani Magufuli alianzisha kampeni ya kurudisha mali za chama na kukifanya chama cha mapinduzi kujitegemea katika kila kitu. CCM ilitoka kukusanya millioni 5 kwa mwaka hadi kufikia billion 20.

Mali za CCM zilikuwa zimekaliwa na kutafunwa na vigogo akiwemo huyo Diallo.

Screenshot_20210710-124312.jpg
 
Mleta Uzi mbona umemuambatanisha hapo Diallo na issue ya kuchagua rais kutokea Milembe
 
mligawana majukumu tu,wale wezi yeye muuaji tena bora hata fisadi atanipa ajira. muuaji je
 
Ila kumbe Magufuli alikua anaogopwa aiseeee.....[emoji12]
Apumzike kwa amani tu yule baba

ndio sababu ataendelea kuwa rais wangu bora wa muda wote.

hawa panya wanaojifunua ndio wanathibitisha kwamba ni kweli mwamba alikuja pale kwa kazi maalum.
 
Na hilo file la Milembe analodai Dialo ni la nani!

kwa sasa kila mmoja atalopoka analojiskia,lakini watz ni watu timamu sasa.

angali kwenye corona ndio utajua hawayumbishwi na kauli mbili mbili.
 
Ila kumbe Magufuli alikua anaogopwa aiseeee.....[emoji12]
Apumzike kwa amani tu yule baba
Alafu sisi wengine wala hatukua tunamuogopa,Bali tulikua tunafurahia kazi zake kwa Jamii!!
 
Back
Top Bottom