Hayati Dkt. Magufuli hakuisaidia Chato

Mkuu umeadimika sana
 
 
Unajiita doctor ila unaandika vitu kama mtoto mdogo alievaa pampas ambae hajui la kufanya!Unasema Magufuli kupenda kwao siyo kosa,unaelewa kuwa Magufuli alikuwa ni Rais wa nchi na wala siyo mwananchi wa kawaida?..
Nami nilishangaa sana kwa mwanzo huo wa mada yake.

Ilikuwa kidogo tu niishie njiani kuendelea kuisoma yote, kabla ya kuanza kuona inapoelekea mada yake.

Hata haya tunayoyaandika sasa kuhusu miradi mbadala ambayo ingewagusa watu moja kwa moja na ingekuwa ni endelevu; tunaandika juu yake baada ya kuona kwamba mhusika alikuwa hastuliwi na kelele za upendeleo wa kwao.

Ndiyo maana tukapendekeza haya tunayoyapendekeza hapa.

'In fact', kama angewekeza kwa wananchi wa wilaya ile, pengine hata makelele yasingekuwepo sana kwa upendeleo huo, na bila shaka angesifiwa sana kama maisha ya wananchi yangebadilishwa na kazi hiyo ya uwekezaji juu yao, badala ya uwekezaji kwa vitu.
 
Wilaya ya Chato iliyopo mkoani Geita ni Tanzania. Kwahivyo, itakuwa furaha ya kila mzalendo wa Tanzania kuona maendeleo ya Chato kama itakavyokuwa kwa maendeleo ya sehemu nyingine ya Tanzania...
Ivi hii tabia yakuita mali za umma majina ya watu binafsi ipo kisheria au mimi ndo sielewi wakuu??? Haya majina mfugale,sijui kijazi huwa ni kwann inakuwa majina yao viongozi wakati pesa zina wananchi walipa kodi?

Ebu acheni hii tabia viongozi tz maana sisi ambao sio viongozi majina yetu ndo yaishie kwenye vitambulisho vya nida??!!! Acheni izi mambo kama haipo kisheria pesa niza wananchi buana
 
Mkuu ukiamini yanayosemwa na nyumbu wa Ufipa, utaamini kweli Mbowe ni "mwekezaji" Dubai na Chadema ni chama kikuu cha upinzani wakati hakina mwenyekiti wa mtaa, wala diwani wala mbunge nchi nzima!!
Unajua Mkuu mimi sijawahi kufika Chato,ila nimepita hiyo barabara kuu ya Mwanza-Geita nikaishia Geita,sikufika Chato.

Sasa waliowahi kufika kule watuambie Chato palikuwa mahala pa hovyo kabla JPM hajawa Rais wakipalinganisha na Wilaya zipi (wasipalinganishe na Majiji au Manispaa).

Mfano:waseme Chato ni pa ajabu ajabu tu afadhali ya kule alikozaliwa Mkapa,Mangula,Phillip Mpango,Nimrod Mkono,Sospeter Muhongo,Rostam Aziz, n.k.
 
Msingi imara ni muhimu katika ujenzi ila endapo ukakosea msingi ata nyumba iwe nzuri vipi ipo cku itapiga creck
 
Wilaya ya Chato iliyopo mkoani Geita ni Tanzania. Kwahivyo, itakuwa furaha ya kila mzalendo wa Tanzania kuona maendeleo ya Chato kama itakavyokuwa kwa maendeleo ya sehemu nyingine ya Tanzania...
Hivi vitu vingine mnavyo shadadia utasema sehemu nyingine hamna..!! Yani ata uwanja wa mpira wa miguu nao nongwa? Au mnafikiri uo uwanja ungekuwa kama wa Benjamini?

Uwanja wenyewe sijui ulikuwa umetumia milion 200 tu mpaka ulipofikia hapo na ulikuwa una miaka kama mitatu tangia uanze kujengwa na badi zaidi ya milion 600 zinaitajika kuukamilisha alafu mnalalama tu..!!
 
Hivi umeisoma mada na kuielewa kweli?

Maanake wewe unakoroga kivyako tu.
Milioni 200 + milioni 600 = 800 milioni - uwanja wa mpira kijijini? Kuna timu gani maarufu sana hapo kijijini.

Sasa chukulia hiyo hela milioni 800 iwekezwe kwa wananchi, iwasaidie kwa mfano kulima zao la alizeti ili kuzalisha mafuta ya kula.

Wananchi hawa wapate huduma zote zinazohitajika kuwezesha kilimo bora cha zao hilo, hela hiyo hiyo ingetosha kuweka kiwanda cha kusindika zao hilo na kupata mafuta na mashudu ya kulisha mifugo.

Mbali ya faida ya kuongeza pato la wananchi hao katika miaka miwili na kuendelea, hawa wananchi wangepata kitu cha kudumu zaidi - elimu ya kuendelea kuzalisha kwa ufanisi zao hilo mwaka hadi mwaka, hata baada ya Magufuli kuondoka!
Na uwanja huo wangeujenga wananchi wenyewe bila hata ya msaada iwapo kama kipato chao kimeongezeka kutokana na hiyo mlilioni 800.

Huo uwanja hata kama utaendelea kujengwa (sidhani), utaleta manufaa hayo ya moja kwa moja kwa wananchi wa eneo hilo?

Na kama bado huelewi...
 
Aliisaidia sana, labda kama walikuwa hawabebeki tu.
 
Mkuu ukiamini yanayosemwa na nyumbu wa Ufipa, utaamini kweli Mbowe ni "mwekezaji" Dubai na Chadema ni chama kikuu cha upinzani wakati hakina mwenyekiti wa mtaa, wala diwani wala mbunge nchi nzima!!
Mbowe ni mfanyabiashara wa kuzaliwa. Baba yake Mzazi alikuwa anakula Meza moja na Nyerere. Ingawa aliumizwa Sana 5 years ago Mungu ameshamuonesha matendo yake Makuu. Mbowe hujazaliwa kwenye Njaa na hajakulia kwenye Njaa.
 
Wapinzani wametucheleweshea sana maendeleo, ila hayo magorofa tutafugia popo msijali, mwenda zake alipenda sana chatto iwe mkoa sasa wilaya ndo najiuliza n zipi
 
Mchango Safi kabisa. Kulikuwa na haja ya Jengo Geita Airport halafu kuliita Mfugale Tower?
Hi ilikuwa cyndicate ya jiwe na jinsi walivyokuwa wanapongezana!! Kumbukeni kalemane ni ndugu ya jiwe na walikuwa njiani kujenga kiwanja cha michezo cha kimataifa hapo kijijini!
 
Wewe huijui Chato, unaifahamu kupitia vyombo vya vya Habari tu. Magufuli amefanya maendeleo makubwa sana wilayani Chato upande wa elimu.

Kiufupi safari za ndege za ATCL hazijasitishwa, bado zipo kama kawa. Sisi tunaopanda ndege tunajua.

Ungekuwa umeishi wilaya ya Chato usingeandika upuuzi huo ulioandika..Ulichoandika ni taka taka
 
Hi ilikuwa cyndicate ya jiwe na jinsi walivyokuwa wanapongezana!! Kumbukeni kalemane ni ndugu ya jiwe na walikuwa njiani kujenga kiwanja cha michezo cha kimataifa hapo kijijini!
Mmh
 

 
Anthony Dialo alishasema, jamaa alikuwa mwehu. Nguvu nyingi, akili punje ya mchele
 
Tumsameheni na tusonge mbele jamani ndio keshatangulia na yake yamemaliza. Sasa kazi kwa walio Chato na TZ kwa ujumla. Kiufupi mambo mengi hata waliohai tunauliza masuali kinyume nyume kwa mfano ivi TZ tuna wataalamu wangapi wa afya, lakini unamsikia mtu akitoka povu kanisani akiuliza kwanini wazungu hawajatengeneza chanjo ya malaria ?

Suali zuri ni kwanini wataalamu wa ndani hawajavumbua chanjo, sio wazungu. Kwa bahati wao hawasumbuliwi na malaria, I can understand that its not in their prio-list.

TZ tuna tatizo la umeme tokea napata fahamu zangu liko vile vile hadi nadhani nitaondoka duniani. Wataalamu wetu wanafanya nini ? UDSM inazalisha vilaza ?
 
Tukiwa tunaandika hapa JF, mamilioni ya fedha yanatumika kuendesha kesi ya ugaidi. Mliwahi kujiuliza kuendesha kesi kama ile inagharimu kiasi gani ? Kila mwanasheria wa serekali analipwa kiasi gani kuendesha kesi n.k. Mashahidi, maofisa, majaji.

Hii itatupiliwa mbali aidha sio muda mrefu au baada muda mfupi ujao. Kamanda wa jeshi anatafuta magaidi ndani ya madrasa - ivi ulisikia wapi gaidi akatokea huko 🙄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…