Mkuu
Pascal Mayalla !
Nimefarijika kuona mabandiko yako na nimeyapitia yote.
Tatizo kuu la nchi yetu ni Unafiki na Ubinafsi.
Magufuli alikuwa amezungukwa nao kuanzia Ikulu mpaka Msoga na huko Ma-wizarani.
Na same thing is going on round the time currently.
Sasa hapo ndio utaelewa ni kwa nini CCM haitaki watu wenye big thinking capabilities.
Ni kwa sababu ya kundi dogo la wasio na upeo bali waliojaa tamaa kuweza kuipenya CCM na hatimae kukaa kwenye "inner cycle core" ya CCM na hatimae kufanikiwa kuunda "Party Cartel's" na kisha kwa "Syndicate" hiyohiyo wameweka watu wao watiifu kule serikalini na hatimae wamekuwa ni "State Capture"
Watu wazuri na wazalendo ndani ya chama na serkali wametishwa na kutishika.
Ukiona unagombea na kukatwa jina au kunyimwa kura na "wajumbe" basi elewa si maamuzi yao bali ni maamuzi ya hao "State Captures" kwa jofu ya kwamba ongezeko la wajanja na waelewa ndani ya chama.
Kutawaamsha wengi waliolala ndani ya chama bila kuujua mchezo unaoendelea.
Na matokeo ya CCM kubagua watu wenye upeo na hoja,imepelekea CCM kukosa viongozi wenye weledi na uelewa.
Sasa kuanzia huko U-VCCM mpaka Jumuia za wazazi na wanawake.kuna ombwe kubwa la uongozi na hakuna yeyote aliyeweza kuvaa viatu vikamtosha.
Hapo sijaongelea hawa makatibu wa uenezi wa CCM na katibu mkuu sampuli ya Chongolo!
Hapo ni wazi tegemeo kuu la CCM kwenye chaguzi ni Dola na Dollars $.
Sio hoja wala ushawishi kwa wapiga kura.
Jumatatu njema!