Hayati Magufuli alikuwa smart?

Hayati Magufuli alikuwa smart?

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
5,718
Reaction score
7,784
Kwema ndugu? Kutokana na kuenea kwa baadhi ya maneno kwamba bwana yule alikuwa mshamba, katili n.k, nikaona acha nitafute ukweli juu ya haya.

Nimepitia documentaries nyingi, hapa JF na nje ya JF. Ila kuna moja imeniacha hoi. Nayo ni ya mmoja wa members humu, akidai kuwa amewahi ku interact na baadhi ya viongozi wakuu wa nchi hii, 'specifically' JK and JPM.

Nitanakili maelezo yake hapo chini:
"Kikwete mtoto wa mjini nusura aingie ikulu 1995 kama sio kuwa close na EL.japokuwa EL ndio alikuwa sponsor wake, baada ya kuukosa urais, kwa miaka kumi alijipanga kisawasawa ikiwemo kuishi low profile ili kucheza na akili za watanzania. Tulisoma shule za kayumba na watoto wake, niliwahi kupanga foleni na JK kwenye ATM za CRDB Holland House posta, niliwahi kucheza draft na JK mitaa ya Shibam nagomeni, niliwahi kunywa supu ba JK Hugo House Kinondoni, yote ni kutudanganya kuwa ni mwenzetu. Timu yake ya Urais yaani wanamrandao wangeamya hata urais wa dunia wangeuchukua. JPM mnamchukulia poa ila hakuna mtu mjanja kama yeye, kila alichokifanya au kukitamka kwa miaka 20 kabla hajawa Rais ilikuwa ni kampeni tosha, ipo siku nitaweka visa vyake jinsi alivyojipanga, JPM ni jogoo la shamba lililowika mjini"

Kwa mchango wangu juu ya hili, nachelea kusema, kwa dalili zinazoonekana na zilizoonekana, huenda ikawa kweli bwana yule alikuwa ni jogoo la shamba lililowika mjini.

Ilikuwaje akamu outsmart 'mtoto wa mjini' na kisha jina lake kupitishwa mkutano mkuu? Ilikuwaje akapewa uwaziri ilhali alijulikana kwa kuwa 'kichaa' kama wengi wanavyodai?

Haya na mengineyo yanalipa nguvu shauri la bwana yule kuwa smart.

Credits to mdukuzi
 
HUYU JAMAA "JPM" HATAKUJA KUSAHAULIKA, ATATAJWA KILA LEO NA ATAENDELEA KUSUMBIA VICHWA VYA WAHUNI NA MATAPELI WA NCHI HII HATA AKIWA KABURINI! VIZAZI VIJAVYO, VYENYE AKILI BAADA YA KUONDOKA HIVI VYA UCHAWA, VITAKUJA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWA TAIFA HILI NA KUMJENGEA SANAMU...
 
HUYU JAMAA "JPM" HATAKUJA KUSAHAULIKA, ATATAJWA KILA LEO NA ATAENDELEA KUSUMBIA VICHWA VYA WAHUNI NA MATAPELI WA NCHI HII HATA AKIWA KABURINI! VIZAZI VIJAVYO, VYENYE AKILI BAADA YA KUONDOKA HIVI VYA UCHAWA, VITAKUJA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWA TAIFA HILI NA KUMJENGEA SANAMU...
Kwa anavyotajwa, pamoja na visa kumhusu, ni wazi atadumu sana midomoni mwa watu.
 
Jamaa alikuwa ameshapangwa, akapangika na akajipanga ila akabaki kuwa simple guy asiye na makuu bali mchapa kazi.

Jiulize tu kwa nini mzee Mkapa alimpa kitabu chake cha hotuba mapema sana kabla ya 2015 tena kwa sherehe?

Maneno ya Makinda kwa Magufuli wakati wa bunge la bajeti 2015 ilikuwa kutufungua macho kuwa ndie ajaye.
 
Mwana urais hatoki mjini ama kijijini...... Anapatikana ndani ya chama haswaa akiwa kada swafi na yuakubalika na wanachama wenziwe.......Fikiria hao wote wamekuwa wabunge kwa zaidi ya miaka 15 na uwaziri ndani yake ni wazi wanaijua vyema tasnia yao na Sera za chama Chao na si u-Smart
 
Kunywa supu na huyo Kikwete hakumfanyi kuwa raisi bora kwa hapa 🇹🇿 maraisi wote wana background ya kawaida tu na social interact niswala la mda .isipokuwa tu hata huyo magufuli kuna mambo alikosea sanaaa. Huyo kikwete ndio sitaki kusema kabisa.
 
Alikuwa smart sana japo alikuwa na mapungufu yake kama wanadamu wengine
Hakua smart, mfano umetuma jasusi kuwapekua ACACIA kuna ulazima gani kumtangaza hadharani? Au unataka kumuua mgombea wa chama pinzani si umpige sumu tu why marisasi karibu 40!!

JPM hakua smart or rather alikua na akili za darasani tu ila alikosa exposure.
 
Usinambie kina Osama, Hitler, Sadam, Jeff Kennedy nao hawakuwa smart, kina Patrice lumumba?
Hata Lumumba hakua smart, huwezi eleza azma yako kabla ya kupewa kiti. Hakua politician kabisa ndio maana aliondolewq kirahisi sana
 
Back
Top Bottom