Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Marehemu Rais wetu mpendwa RIP Doctor Magufuli aliwahi kutabiri kuhusu Umeme na Maji alisema kuwa akiondoka matatizo yatarudi kama zamani na leo hii yamerudi tena matatizo ya Umeme na Maji kwa njia ya mgao Lohhh Aliyeturoga sisi Wa-Tanzania ameshafariki miaka mingi hatuwezi tena kupona maradhi yetu.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akinawa maji ya bombo katika eneo la Mivinjeni ambalo kuanzia usiku wa jana limeanza kupata maji kutoka mradi wa visima vya Kigamboni.
By Elizabeth Edward
Mwandishi
Mwananchi
Dar es Salaam. Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesisitiziza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) kuzingatia ratiba ya mgawo wa maji huku akibainisha uwezekano wa maji kuongezeka mto Ruvu kufuatia mvua kuanza kunyesha mkoani Morogoro.
Hata hivyo amewatahadharisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam kutumia vizuri maji wanayopata kulingana na mgawo kwa kuwa bado kuna changamoto ya upatikanaji.
Aweso amesema Dawasa ikizingatia ratiba ya mgawo itaondoa itaondoa malalamiko ya watu kukosa maji kwa kuwa bado maji yanayozalishwa ni kidogo.
Ameyasema hayo leo Jumanne Novemba 8, 2022 wakati akikagua visima vilivyofufuliwa na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Temeke ambayo yameanza kupata maji kutoka mradi wa visima wa Kigamboni uliozinduliwa wiki iliyopita.
Akizungumzia hali ilivyo kwa sasa waziri amekiri kuwa bado kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa maji huku akieleza kuwa hatua kadha zinaendelea kuwanasua wananchi katika adha hiyo.
“Tunapitia kipindi kigumu ila niwaombe wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuwa wavumilivu, maji ya Kigamboni yameshavuka na yameanza kusambaa katika maeneo ya Temeke na katikati ya mji.
“Mategemeo yetu ni kwamba yatazidi kuwafikia wananchi na kwa kiasi fulani yatapunguza adha ya maji katika maeneo ambayo yanafikiwa na maji haya kutoka Kigamboni,” amesema Aweso.
Baadhi ya wakazi wa mitaa ya Temeke wameeleza kuwa kwa takribani wiki mbili walikosa maji na yameanza kutoka usiku wa jana.
“Wiki mbili hatujapata maji ila jana usiku ndiyo tumeanza kuona maji, hatujalala usiku kucha tumechota tukijua yatakatika ila hadi sasa tunaona bado yanatoka,” amesema Suzan Majaliwa mkazi wa Kurasini.
Meneja wa Dawasa Temeke, Cosmas Makere amesema kuanzia jana maji kutoka kwenye visima vya Kigamboni yamefika katika baadhi ya maeneo wilayani Temeke.
chanzo. Aweso asisitiza Dawasa kuzingatia ratiba mgawo wa maji
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akinawa maji ya bombo katika eneo la Mivinjeni ambalo kuanzia usiku wa jana limeanza kupata maji kutoka mradi wa visima vya Kigamboni.
Aweso asisitiza Dawasa kuzingatia ratiba mgawo wa maji
Jumanne, Novemba 08, 2022By Elizabeth Edward
Mwandishi
Mwananchi
Muktasari:
Ili kuondoa malalamiko ya wananchi, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameisisitiziza Dawasa kuzingatia ratiba ya mgawo wa maji katika Jiji la Dar es Salaam huku akisema kuna uwezekano wa maji kuongezeka mto Ruvu kufuatia mvua kuanza kunyesha mkoani Morogoro.Dar es Salaam. Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesisitiziza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) kuzingatia ratiba ya mgawo wa maji huku akibainisha uwezekano wa maji kuongezeka mto Ruvu kufuatia mvua kuanza kunyesha mkoani Morogoro.