Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Sifurahishwi na ubadhirifu unaoonyeshwa kwenye ripoti za CAG wala siutetei kwa namna yoyote ile
Lakini nataka kusema tuache siasa na unafiki, ama hata ripoti za CAG zinaweza kuwa zinatolewa kisiasa kama tunazijadili kisiasa
Kuna baadhi ya watu ambao wamekosa hoja ya kutetea siasa zao zilizoigharimu sana nchi hii kwa miaka 6 , sasa wameona ripoti ya CAG ndio gia mpya ya kutetea ushetani wao
Watu hawa wanadai awamu hii ndio ripoti ya CAG imeonyesha wizi mkubwa na hakuna hatua iliyochukuliwa tofauti na miaka 5 ya kiongozi wao,
Ni vizuri kuhimiza hatua zichukuliwe lakini sio kwa siasa za kilaghai, miaka hiyo 5 ni mwaka gani ambao mtu aliwahi kufungwa kutokana na ubadhirifu wa ripoti ya CAG?