Hayati Magufuli aliwasaidia Chadema kuchuja Vibaraka na Makamanda original

Hayati Magufuli aliwasaidia Chadema kuchuja Vibaraka na Makamanda original

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Au nasema Uwongo ndugu zangu.

Vibaraka wote wenye vinasaba vya CCM hayati Shujaa Magufuli aliwatwaa na kuwarejesha Lumumba na kuiacha Ufipa st na Makamanda original.

Sasa utakuta 2025 Chadema inaenda tena CCM kuomba mamluki wa kugombea Urais na Ubunge ili kudumisha Maridhiano

J3 Ubarikiwe sana.
 
Kwa jinsi chadema walivyo Uviko 19 wakimaliza ubunge wao wa mchongo watarudi chaman kwa kuomba samahan na watakubaliwa na kupewa majimbo ya kugombea 😂
 
Vibaraka wote wenye vinasaba vya CCM hayati Shujaa Magufuli aliwatwaa na kuwarejesha Lumumba na kuiacha Ufipa st na Makamanda original.
Ni kweli, shetani anawajua watu wake na hata wafanye juhudi gani za kujikwamua lazima watarudi tu nyumbani. Dr. Slaa alijaribu kumkimbia shetani, Lowassa alijaribu kumkimbia shetani na hata Sumaye naye alijaribu kumkimbia shetani lakini mwisho wa siku...all chickens do come back home to roost?
 
Tena kweli kila mwelevu anatamani tuwe na upinzani imara na sio vyama pinzani kujaa mandumilakuwili hapana hatuendelei
 
Yaani Kila ukiamka unaanzisha thread.

Hivi unatunza record ya thread ulizowahi anzisha? Sijawahi ona ukiziquote kama reference popote!!!

Jukwaa linadhalilishwa sana na watu aina Yako bwashee!
 
Yaani Kila ukiamka unaanzisha thread.

Hivi unatunza record ya thread ulizowahi anzisha? Sijawahi ona ukiziquote kama reference popote!!!

Jukwaa linadhalilishwa sana na watu aina Yako bwashee!!
Endelea kukariri

Tupo hapa Jamhuri kujua idadi ya Watanzania na kutoa mwelekeo wa mipango ya Serikali

Unateseka bure kabisa bavicha wewe!
 
Sio lazima hadi uhamie ccm, Zitto kabwe hayupo ccm ila anakula asali vizuri na wengine wale waliyomchukua Lowassa walikula pesa nje ya ccm.
 
Au nasema Uwongo ndugu zangu.

Vibaraka wote wenye vinasaba vya CCM hayati Shujaa Magufuli aliwatwaa na kuwarejesha Lumumba na kuiacha Ufipa st na Makamanda original.

Sasa utakuta 2025 Chadema inaenda tena CCM kuomba mamluki wa kugombea Urais na Ubunge ili kudumisha Maridhiano.

Akili za Chadema ni afadhali hata za Mwendawazimu wakati mwingine.

J3 Ubarikiwe sana.
Asante Jo kwa haraka,Ila je wewe uliangukia kundi lipi😄
 
Au nasema Uwongo ndugu zangu.

Vibaraka wote wenye vinasaba vya CCM hayati Shujaa Magufuli aliwatwaa na kuwarejesha Lumumba na kuiacha Ufipa st na Makamanda original.

Sasa utakuta 2025 Chadema inaenda tena CCM kuomba mamluki wa kugombea Urais na Ubunge ili kudumisha Maridhiano.

Akili za Chadema ni afadhali hata za Mwendawazimu wakati mwingine.

J3 Ubarikiwe sana.
Mbona unaongea kama Abunuwasi alipotaka ruhusa ya mfalme kumpiga rungu mwizi wa wali wake? Umejuaje kuwa CHADEMA wataenda kuomba mgombea toka CCM 2025? Au ndio unawashauri kinamna wasifanye hivyo? 😃
 
Au nasema Uwongo ndugu zangu.

Vibaraka wote wenye vinasaba vya CCM hayati Shujaa Magufuli aliwatwaa na kuwarejesha Lumumba na kuiacha Ufipa st na Makamanda original.

Sasa utakuta 2025 Chadema inaenda tena CCM kuomba mamluki wa kugombea Urais na Ubunge ili kudumisha Maridhiano.

Akili za Chadema ni afadhali hata za Mwendawazimu wakati mwingine.

J3 Ubarikiwe sana.
Kweli tupu mamluki wote hawapo
 
Ni Uwazi usiopingika kuwa Kile Alichoamini RAIS MAGUFULI hata angekuwepo leo angekiri KUSHINDWA tena HADHARANI

Baada ya UCHAGUZI wa 2015 uliokuwa na idadi ya WABUNGE wengi wa UPINZANI ulimfanya RAIS Magufuli aone Ugumu wa Kulitawala BUNGE na Kupitisha SHERIA na MISWADA Mibovu aliyoitaka .

Na ndio maana UCHAGUZI wa 2020 aliamua kwa MAKUSUDI kuuvuruga ili Awapate WABUNGE wa Ccm na kuwakata WAGOMBEA Wote wa VYAMA vya UPINZANI na UCHAFUZI huo ALIFANIKIWA.Pamoja na Mafanikio hayo bado BUNGE hilo halijafanya Chochote cha Ajabu licha ya kuwa ni Bunge la CCM.

Bunge la CCM limekuwa BUNGE linalopitisha Sheria nyingi za Maumivu kwa Wananchi kama vile Sheria ya TOZO mbalimbali ambazo zimeleta MTAFARUKU kwa Wananchi mpaka RAIS SAMIA kaingilia Kati na Kuitaka SERIKALI yake kufanya Marekebisho

Juzi tumelishuhudia BUNGE likitumia NGUVU kubwa kujadili MIKOPO ya Elimu ya Juu kwa Waombaji wachache Waliokosa Badala ya TATIZO KUBWA na ZITO la MGAO wa UMEME na MAJI unaolikumba TAIFA.

aamini bila UCHAFUZI wa UCHAGUZI wa 2020 TANZANIA tungekuwa na BUNGE ZURI la VYAMA VINGI BUNGE ambalo lingewajibika IPASAVYO kwa MASLAHI MAPANA kwa WANANCHI kuliko hili BUNGE la CCM.
 
Unaweza kudhani hayati Shujaa Magufuli alikuwa anataka kujiongezea muda wa kukaa madarakani kumbe siyo Wananchi wa Dunia ya sasa ndio wanapenda aina ile ya Viongozi

Netanyahu karudishwa na Wananchi
Lula karudishwa na Wananchi

Trump atarudi

Boris Johnson atarudi

Rip Shujaa Magufuli
 
Back
Top Bottom