Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Leo 10:15pm 07/05/2022
Kabla ya Rais Magufuli kuingia madarakani Mwaka 2015, Tanzania ilikuwa katika uchumi wa chini, ukiwa katika uchumi wa chini kabisa, sera ya taifa na lengo linapaswa kuwa kuelekea uchumi wa kati wa ngazi ya chini, hii ni hatua moja kutoka katika uchumi wa chini,adhma na ndoto ya Rais John Pombe Magufuli ilikuwa kuipeleka Tanzania uchumi wa kati,Benki ya Dunia hutazama pato la taifa kwa mfano kupitia jumla ya utajiri wa rasilimali zetu zote,Ujenzi wa miundo mbinu itayokuja kuiingizia Taifa fedha za kigeni kutokana na shughuli mbalimbali zitakazotokana na miundo mbinu hiyo na utajiri wa kifedha kugawanya na idadi ya watu wa Tanzania,
Kwa calculation zake Rais Magufuli iliwezekana, ndoto ya Rais Magufuli ilikuwa ni kuingia Uchumi wa kati,sasa ataingia vipi, Mambo mawili akataka kuyatimiza ambayo ndio yatakuwa kichocheo cha kuiingiza Tanzania katika uchumi wa kati,Mambo hayo ni Umeme wa Uhakika kutoka Bwawa la Julius Nyerere,Rufiji na Uchumi wa Viwanda,hivi viwili kwa calculation zake vingeweza kutufikisha kwenye kundi la Nchi zenye Uchumi wa Kipato cha Kati (MIC),kwa hakika aliwaza vyema na alitimiza ndoto hiyo,ili kufanikisha hilo Rais Magufuli alihimiza mambo yafuatayo,
•Ujenzi wa Viwanda nchini Tanzania,viwanda vinahitaji malighafi (kilimo, mifugo, uvuvi, madini, nk);.
• Ujenzi wa bwawa la Umeme la Rufiji litalozalisha megawatts 2,115 ikiwa sasa hivi tunatumia megawatts 1,500 Ili Sekta hizo zizalishe malighafi za kutosheleza mahitaji ya matumizi ya ndani tunahitaji Umeme wa uhakika kutoka Bwawa la Julius Nyerere kule Rufiji,viwanda, na mauzo ya nje ya nchi, lazima kuwepo miundo mbinu bora na imara (usafiri ardhini, majini na angani, maji, nishati).
• Kumudu uendeshaji na ukarabati (Operations & Maintenance) wa miundo mbinu hiyo, kunahitaji rasilimaliwatu wenye uwezo na ujuzi;
• Kupata rasilimaliwatu wa aina hiyo kunahitajika Uzalendo kwa Taifa la Tanzania,huduma bora za jamii (elimu na afya),hii kwa ujumla ilimfanya Rais Magufuli kuanza kuijenga upya Tanzania,laiti Mungu angempa maisha marefu basi watoto na wajukuu wetu wangefaidi matunda ya utekelezwaji wa ndoto za Rais Magufuli.
-Ndoto ya Rais Magufuli kuipeleka Tanzania uchumi wa kati iliwachukiza wazungu na vibaraka wao.
Nimeona nukuu kutoka kwa Wassira ikisema "Magufuli alisema hatuhitaji mikopo tunajenga kwa kutumia fedha zetu, Tanzania ni tajiri lakini yeye ndiye aliyekopa sana kuliko Marais wote,alikopa mikopo yenye riba kubwa kwa kificho kutekeleza ujenzi,deni la Taifa limepanda sana ndani ya miaka 6 ya Uongozi wake" sasa niulize swali, Serikali ya CCM ya Awamu ya tano,iliyoongozwa na Rais Magufuli,ambayo haikuwa na mahusiano mazuri na nchi zote za Ulaya iliwezaje kukopa kwa Serikali za Ulaya ambazo haina mahusiano nazo mazuri!?
-Vibaraka walivyokwenda Ulaya kuzuia mikopo isije Tanzania,kimbilio la Rais Magufuli likawa Benki ya Maendeleo ya Afrika,AFDB.
Benki ya Afrika ndio ilikuwa kimbilio la Rais Magufuli,na hata mtendaji wake Mkuu alifika Chato,kuhani msiba wa rafiki yake,AfDB wamekuwa wakitoa fedha kwenye sekta za maji, nishati na nyinginezo nchini Tanzania na wameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji wa Jiji la Arusha mara baada ya kutembelea Matenki ya Maji ya Themi Hills, Ofisi ya Kanda ya AUWSA-Moshono, Kituo cha kusukuma Maji Namba 4 na Tenki la Maji la Seedfarm lenye ujazo wa lita milioni 10 mkoani Arusha,sasa wanaojua madeni ya awamu ya tano watuambie alikopa kiasi gani hapo Benki ya Afrika? na hicho alichokikopa ndio hicho wanachotuambia kikubwa!?
Vyama vya upinzani nchini Tanzania na wanaharakati wa haki za binadamu hapa nchini Tanzania na wa kimataifa walikuwa wakiweka shinikizo la kutotolewa mikopo kwa Tanzania hadi pale Tanzania itakaporuhusu wanafunzi wanaopata ujauzito waruhusiwe kuendelea na mfumo rasmi wa elimu,kiongozi wa chama upinzani cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe aliwahi kusema kuwa Benki ya Dunia haitakiwi kuikopesha Tanzania dola milioni 500 za elimu kabla ya mabadiliko ya kisera kufanyika.Kwa mujibu wa nyaraka za Benki ya Dunia, pamoja na mambo mengine, mkopo huu ulikusudiwa kwenda kusaidia upatikanaji wa elimu bora na kwa urahisi kwa wanafunzi waliokuwa wanarudi shule baada ya kuwa wamepata ujauzito. Lakini mradi huu wa elimu ulikuwa ni kupitia elimu mbadala na si katika mfumo rasmi.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt Akinumwi Adesina,alifika mara kwa mara nchini Tanzania na alimpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa aliyokuwaanaifanya kuimarisha uchumi wa Tanzania na alijadiliana mambo kadhaa na Rais Magufuli yakiwemo namna benki hiyo ilivyosaidia juhudi za maendeleo za Tanzania tangu mwaka 1971 na inavyoendelea kusaidia katika ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo,nikimnukuu katika moja ya mahojiano yake alisema
"Yote kwa yote nimemhakikishia Rais Magufuli kuwa AfDB itamuunga mkono katika mipango yake na maono yake ili tuweze kuisaidia Tanzania kukua zaidi, nimefurahi kuzungumza na Mhe. Rais na naona Tanzania ipo katika njia sahihi," alisema Dkt Adesina kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ikulu wakati wa Awamu ya tano,AfDB ilifadhili miradi ya maendeleo yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 3.457 (sawa na Shilingi Trilioni 7.78 Tanzania) zikiwemo fedha za miradi 25 zilizotolewa kuanzia mwezi Novemba, 2017 yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.986 (Shilingi Trilioni 4.47 Kitanzania).
Nimalizie kwa kuishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) kwa kutoa mikopo kwa Serikali ya Tanzania kusaidia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati iliyobuni ajira kwa Watanzania wengi na iliyotarajiwa kubuni ajira nyingi kwa Watanzania mara tu Bwawa la Julius Nyerere,Rufiji litakapoisha,ilitarajiwa tani zaidi ya laki tano za mpunga na mazao mengine kuzalishwa pembeni ya Bwawa la Umeme la Julius Nyerere pale Rufiji na tungeweza kuuza mchele (export) nje ya nchi na kuliingizia Taifa fedha za kigeni na hivyo kukuza thamani ya shilingi ya Tanzania,hivi ni kati ya vitu ambavyo viliivutia Benki ya dunia kuitangaza Tanzania kama taifa lenye kipato cha kati mnamo mwezi Julai 2020.
Mbali na uongozi thabiti wa rais Magufuli katika kudhibiti matumizi ya fedha na kukabiliana na ufujaji wake,taifa la Tanzania lilitarajiwa kuimarika kiviwanda hali ya kwamba lina karibia viwanda 60 tangu lilipojipatia Uhuru, huku uongozi wa rais Magufuli ukifanikiwa kuanzisha zaidi ya viwanda elfu nane katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake,hivi sasa nchini Tanzania tunaunganisha matinga humu nchini,tunaunganisha mabasi na kuzalisha nondo ,mabati na kadhalika,kufikia tar 01/07/2020 siku ya Jumatano,Benki ya Dunia,iliiorodhesha Tanzania katika orodha ya nchi za uchumi wa kipato cha kati,kabla ya lengo ya dira ya Taifa kuiingiza Tanzania katika uchumi wa kati mwaka 2025.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.