Hayati Magufuli aliwezaje kukopa kwa Wazungu ikiwa aliharibu uhusiano na nchi za Ulaya?

Hayati Magufuli aliwezaje kukopa kwa Wazungu ikiwa aliharibu uhusiano na nchi za Ulaya?

Magufuli alikuwa anakopa zaidi pesa kutoka benki za kibiashara ambapo riba huwa kubwa na huko hawana tatizo na mkopaji, maana ni suala la kibiashara na sio kisiasa.

Jamaa pamoja na kuandika kote na kutoa wasifu wake kielimu hakulijua hili?!

Kazi ipo...
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Mkuu sang'udi, Kama uwezo upo ni sahihi kabisa, na sina tatizo kupata kiongozi mwenye uthubutu wa kiwango hicho na kwa hilo 👏👏👍👍 kwa JPM(RIP)

Nitaandika kwa urefu ila tafadhali kama hutojali soma ili uelewe hoja yangu.

Pamoja na hayo aliyofanya, biashara hazikupaswa zifungwe, account za wafanyabiashara hazikupaswa zifungwe, mishahara kwa kiasi fulani ilipaswa iongezwe, huduma za uuzaji mazao hazikupaswa kuondolewa kwa wafanya biashara na kufanya ni state business na mengine mengi.

Nasema hivi kwasababu hivi ndivyo vitu vinavyomwezesha raia wa kawaida kufanya maendeleo binafsi na kurithisha vizazi vya mbele wakati yeye akiendelea kupokea pension ya uraisi na kushuhudia vizazi vyake vikifurahia urithi alioacha na akiendelea kupokea sifa za treni na ndege alizoacha.

NITAKUPA MFANO HAI WA MAMBO YALIYOTOKEA CHINI YA SERIKALI YA JPM:

Wote tunajua sheria zetu wakati mwingine huwa zinakuwa na mapungufu ya kuzitekeleza, mfano sheria za kuwataka wenye kampuni za consultancy wajisajili na VAT na waandae mahesabu bila kujali uwezo wa mtaji.

Kama mtu ana kakampuni kake ka sheria, kameajiri watu 5, sheria inamtaka aandae mahesabu kila mwaka na ajiunge VAT. Gharama ya kuandaa mahesabu si chini ya Tsh 500,000 mpaka 1,000,000 nje ya gharama za uhasibu, gharama ya kufile VAT si chini ya 50,000 mpaka 100,000 kila mwezi.

Sasa huyu mwenye kakampuni hakuwa akifile hesabu za mwisho kwa kutokujua au kwa kupuuza kwa sababu ya gharama za ukaguzi na uhasibu, na akawa anaenda kufanya makadirio kila mwaka kisha analipa kodi anaendelea na biashara kama presumptive tax payers wanavyofanya ilihali yeye ni corporate.

Sasa serikali kwa sababu ina marejesho ya mkopo wa reli ikatumia sheria ya kutokupeleka hesabu TRA ya adhabu ya Tsh 225,000 kila mwezi, na ikatumia sheria ya kutoa assessment kukadiria kodi ambayo huenda ingepatikana kwa kufanya examination of books of accounts.

Ikachukua % ya turnover ya miaka 5 ikaiita profit ikacharge penalty na interest kila mwezi ikapata makisio ya kodi ikajumlisha na zile 225,000 kila mwezi za miaka 5 na kumtaka mfanya biashara alipe plus interest each month for 5 years na kuzuia akaunti yake ya biashara huenda yenye pesa za wateja ikimlazimisha kodi ilipwe, mfanyabiashara akashindwa, biashara ikafungwa. Ukumbuke kwa huo mfumo uliotumika inaweza kuja hata kodi ya M40-M50, pesa ambayo mfanya biashara huyo hajawahi kuota kuishika kwa pamoja.

Kisheria raisi alikuwa sahihi na atakuwa alipata rejesho, ila katika uhalisia aliwanyima raia wake haki ya kufanya maendeleo binafsi kwa kuchukua mishahara yao huenda ya miaka 10 mbele ambayo wangelipwa kama angetumia busara na hako kakampuni kakaendelea kuwepo.

Sawa atapeleka rejesho ila, wale watu 5 ambao mshahara wao ameuchukua? Watoto wao mbeleni itakuwa vipi watakapokuta baba zao walilipia treni ila hawana pa kulala?

Sasa ukute baba anahako kakampuni na mama ni mwajiriwa kwenye kahoteli kalikokuwa kanategemea vikao vya wafanyakazi wa serikali vilivyopigwa marafuku kufanyika kwenye mahoteli hako kahoteli kakafungwa huku mzee wao akiwa anacheti cha darasa la saba akaondolewa kazini akiwa na miaka 57.
Mkuu Mimi nimeshuhudia matajiri watatu wakipewa barua hizo za kodi,tajiri mmoja ambae mwaka 2018 alinunua nyumba Shanghai,China zaidi ya billioni 2 alipewa barua ya kulipa billioni 2,tajiri wa pili yeye ana kiwanda Cha plastic alinunua ghorofa Kariakoo kwa billioni 1 yeye akapewa barua ya kodi ya Milioni 600 na wa tatu yeye alikuwa na Bureau yeye alikuwa na uwezo wa kununua hata dola million 1 kwa siku,wakati wa ambush ya kukagua bureau alikutwa na dola Million 1 na sh million 800 yeye akapewa barua ya kulipa kodi million 500, Sasa nikuulize ndugu yangu kwa akili za kawaida watu awa walionewa!!??
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kama hajaelewa ana kichwa kigumu kama jiwe.
Magufuli alikuwa anakopa zaidi pesa kutoka benki za kibiashara ambapo riba huwa kubwa na huko hawana tatizo na mkopaji, maana ni suala la kibiashara na sio kisiasa.
 
Mkuu Mimi nimeshuhudia matajiri watatu wakipewa barua hizo za kodi,tajiri mmoja ambae mwaka 2018 alinunua nyumba Shanghai,China zaidi ya billioni 2 alipewa barua ya kulipa billioni 2,tajiri wa pili yeye ana kiwanda Cha plastic alinunua ghorofa Kariakoo kwa billioni 1 yeye akapewa barua ya kodi ya Milioni 600 na wa tatu yeye alikuwa na Bureau yeye alikuwa na uwezo wa kununua hata dola million 1 kwa siku,wakati wa ambush ya kukagua bureau alikutwa na dola Million 1 na sh million 800 yeye akapewa barua ya kulipa kodi million 500, Sasa nikuulize ndugu yangu kwa akili za kawaida watu awa walionewa!!??
Tafsiri ya kuonewa ni ipi? Uwezo wa mtu kufanya jambo na fedha zake unautafsiri vipi ukiuhusuisha na jukumu la kulipa kodi kisheria? Taratibu za adhabu kwa waliokwepa kodi kisheria zipo vipi? Haya maswali yote, majibu yake yatajibu swali la hawa watu walionewa?
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Magufuli alikuwa anakopa zaidi pesa kutoka benki za kibiashara ambapo riba huwa kubwa na huko hawana tatizo na mkopaji, maana ni suala la kibiashara na sio kisiasa.
1652032421382.png
 
Chumvi za kiupinzani katika siasa. Linachukuliwa jambo moja la kawaida, linakuzwa kuonekana ni vita baina ya nchi mbili.
Kizuri chajiza kibaya chajitembeza !!! Debe tupu halikosi kelele Hata muandike kwa wino wa uharo mliohara magu was incompetent prsidaaa ovaaa
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Mkuu,
Siyo kwamba hatuna uwezo wa kupambana na matatizo yetu.

Magufuli ametuonesha kwa vitendo inawezekana kabisa kujenga nchi kwa kodi zetu wenyewe, na mikopo michache sana.

Ukumbuke pia hilo deni la karibu Trillion 30 linahusisha na madeni yaliyoiva ya nyuma ambayo amepambana sana kuyalipa.

Ametufundisha inawezekana kabisa kuendesha nchi vizuri bila misaada ya mabeberu na tukapata maendeleo.

Sote tu mashahidi wa hili, na namba hazidanganyi. Si dhambi kufanya kwa kasi kubwa kama uwezo upo.
Hata uandike kwa uharo uliohara magu alikua hatoshiiiiiiii
 
Tulipopata uhuru Mwl. Julius Nyerere alitutangazia maadui watatu: maradhi, ujinga na umasikini. Awamu zote zimekuwa zikipambana nayo kwa nafasi yake bila mafanikio ya kuridhisha.

Aina ya uongozi wa Magufuli ulilenga walau kufanya mambo kwa utofauti na matokeo chanya tuliyaona ndani ya muda mfupi. JPM hakutaka kufanya kila kitu peke yake, ila alitaka walau tuwe tulipopaswa kuwa baada ya miaka 60 ya uhuru.

Ukweli ni kuwa tupo nyuma sana, miaka 60 ya uhuru:
• Hatuna vyanzo vya uhakika vya umeme
• Tuna mfumo na miundombinu duni ya elimu
• Hatuna miundombinu bora ya usafiri kuanzia nchi kavu, maji na hata anga
• Hatuna huduma na miundombinu bora ya afya
• Tumeshindwa hata kuhamia Dodoma
• You name them

Kama Rais Mzalendo, asingeweza kufanya mambo kwa mazoea. Tuna utajiri mwingi sana lakini sisi ni masikini sana, yote ni kwa kuwa tuna ombwe la uongozi.

Marekani na mataifa mengine wana malengo na masilahi yao. Kama wataona una-serve interests zao watakuwa na wewe, kama hauwasaidii chochote wataachana na wewe na kama utawaletea vizingiti kwenye ku-achieve interests zao watapambana na wewe. Ndiyo mfumo wa dunia ulivyo.

Rais na Mzalendo wa kweli ni yule atakayesimamia malengo ya nchi na wananchi wake.

Magufuli hakutaka tuwe wanyonge mbele ya mataifa ya kinyonyaji. Na ndio sababu he pulled us out of a handful of unfair deals and contracts. Kwamba wao wakichukua madini ya kila aina ya thamani kubwa eti watupoze kwa vyandarua na au ARVs. Yes, tunavihitaji hivyo vitu lakini not at the expense of unfair deals.

Alitaka tufaidike na kupata stahiki yetu halali. Hakufanikiwa sana, ila walau alituweka sehemu nzuri. Mambo ni mengi, ila kwa kuhitimisha, asingeweza kuepuka kukopa, lakini tumhukumu kwa kuangalia effectiveness ya hiyo mikopo.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.
Mavi kama mavi
 
Zamani
Kulikuwa na wanaTANU
Baada kukawa na WanaCCM ndani ya CCM
Kisha kukawa na wanaCCM na WANAFURSA ndani ya CCM
Awamu hii kuna wanaFURSA wengi kuliko wanaCCM ndani ya CCM
Tupoelekea wanaCCM wataisha watabaki wanaFURSA ndani ya CCM.
 
Zamani wazee walitoa kila walichonacho ili UHURU upatikane kisha hawakuwa wanaFURSA kwa kulazimisha kuwa Viongozi na wateule bali waliendelea kuwa wanaTANU
Lengo lao lilikuwa ni kupata UHURU

Kizazi cha sasa kukunwa ili wakunwe na kupapaswa wanajiunga na CCM kutafuta FURSA mbalimbali hivyo wapo tayari kufanya hata propaganda HATARISHI ili malengo yao yatimie
Wanakuwa ni wafuasi wa FURSA na sio WAFUASI wa CCM,yupo radhi amtukane marehemu apewe hela ale ashibe au apewe cheo
 
Kalinde kaburi fisi wewe

Kutukana ndio sifa ya vijana wa Chama siku hizi,wao tumbo lishibe u apate cheo atembelee vieite,nimebahatika kusimama kwenye mabega ya watu walioshiriki gwaride la nguvu wakati wa sherehe za kuundwa CCM,wakati ule msisitizo ulikuwa kwenye neno MAPINDUZI. sasa hivi sina hakika kama hata wewe ndugu yangu @⁨road master unajua kirefu cha CCM, kwa maana yake halisi, kwamba ni chama cha kusimamia MAPINDUZI ya kuwakomboa wanyonge,ni chama cha wakulima na wafanyakazi wa Tanzania walio wengi,CCM ya wakati ule ilikuwa na nahodha mahiri.CCM alikuwa akiinua kichwa chake anaona maili elfu kumi mbele.CCM alikuwa anajenga hoja na kuongoza jitihada za kuweka mikakati ya kujenga jamii iliyo sawa na inayoheshimu utu,CCM ilisimamia katika falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea.
 
Moja ya sentesi ilisema "kuvua gamba haikufanikiwa kama ilivyotarajiwa, matokeo yake tunaona kuporomoka kwa umaarufu wa CCM" hii ilikuwa 2013 baada ya CCM kuja na SERA ya KUJIVUA GAMBA, Je TULIFIKA FIKAJE KWENYE SERA YA KUJIVUA GAMBA? suluhisho la matatizo ya kujivua gamba ndio yalipelekea JOHN POMBE MAGUFULI asiye na doa kuchaguliwa kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi wa 2015
 
Back
Top Bottom