Hayati Magufuli anapaswa kupewa Heshima ya Baba wa Pili wa Taifa la Tanzania

Habari za wakati huu, ni matumaini yangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.

Tukirejea kwenye mada, aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Magufuli alikuwa ni kiongozi wa namna yake
LaBDA Apewe Ubaba wa Kambo!
 
Nadhani kuna baadhi ya watu hawajaelewa vizuri mada hii.
Mada hii haimaanishi kwamba marais wengine waliopita hawajafanya lolote, isipokuwa JPM amefanya mambo ya pekee zaidi ambayo watangulizi wake walishindwa.

Kumbukeni mzee Mwinyi alikiri wazi kwamba JPM alikuwa ni wa pekee zaidi hata kuliko yeye.
Baadhi ya mambo ya pekee yaliyoshindikana huko nyuma ni:-
1. Ujenzi wa Bwawa la umeme la Mwl Nyerere.
2. Ikulu kuhamia Dodoma.
3.Ujenzi wa SGR nk.
 
Habari za wakati huu, ni matumaini yangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.

Tukirejea kwenye mada, aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Magufuli alikuwa ni kiongozi wa namna yake na kwa wakati muafaka ambao amekaa madarakani amefanya vitu vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeleta mageuzi na mabadiliko makubwa kiuwajibikaji, kiuchumi na kijamii na kuwa chachu kubwa kwa ustawi wa kimaendeleo wa Taifa la Tanzania.
Hilo litatekelezwa tu ni suala la muda tu kulingana na mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi yatakayotokea ndani ya miaka kumi ijayo.
 
Habari za wakati huu, ni matumaini yangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.

Tukirejea kwenye mada, aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Magufuli alikuwa ni kiongozi wa namna yake na kwa wakati muafaka ambao amekaa madarakani amefanya vitu vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeleta mageuzi na mabadiliko makubwa kiuwajibikaji, kiuchumi na kijamii na kuwa chachu kubwa kwa ustawi wa kimaendeleo wa Taifa la Tanzania.

Hakika hakuna asie na makosa, nami nakiri kuna mahali ambako aliyumba lakini bado haiondoi uhalisia na ukweli kuwa alifanya hivyo kwa dhamira kuu ya kutetea na kupigania maslahi mapana ya Taifa letu sema kuna sehemu matokeo hayakuwa chanya japo lengo lake lilikuwa jema.

Tukijaribu kuweka katika mizani yale Mazuri na mabaya, kwa hakika mazuri ni mengi sana na mfumo wa utawala wake umejenga msingi imara kwa viongozi wengi waliopo sasa na watakaokuja baadae.

Inawezekana sio wote, ila wengi wetu ni mashahidi na tumeshuhudia mageuzi makubwa kwenye kuleta mabadiliko ya uwajibikaji serikalini, kuzuia rushwa na udanganyifu, Mfumo usio na upendeleo katika kutoa ajira, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu yenye kuleta tija kiuchumi kama Bwawa la Nyerere na Reli ya SGR, Umeme vijijini, Uboreshaji wa huduma za Afya, Ongezeko la ukusanywaji wa kodi, uboreshaji wa mikataba ya madini na gesi na vinginevyo vingi ambayo vimefanikisha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati wa chini mapema tofauti na ilivyotarajiwa.

Kwa hakika umefika wakati wa Hayati John Magufuli kupewa Heshima ya Baba wa pili wa Taifa la Tanzania, baada ya waasisi wa Taifa na Muungano ili kuyaenzi daima yale mema yote aliyoyafanya kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na hatotukuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani hata Korea Kaskazini wana Baba wawili wa Taifa, ila yote kwa yote neno langu sio Sheria, ni mawazo yangu tu, hivyo nawasilisha.
Tuwaulize warithi wa Ben Saanane,Azory Gwanda, Alphonse Mawazo na mamia ya wahanga walio "potea" kwenye utawala wake na mwenza Bashite Kama wanakubaliana na uharo wako
 
Mtoa hoja aigeuze hoja yake ili ipate mashiko kwa kumfanya Magufuli kuwa baba wa Taifa wa kanda ya Ziwa. Hili litakuwa powa sana kwani aliwafanyia makuu katika kipindi chake.
 
Habari za wakati huu, ni matumaini yangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.

Tukirejea kwenye mada, aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Magufuli alikuwa ni kiongozi wa namna yake na kwa wakati muafaka ambao amekaa madarakani amefanya vitu vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeleta mageuzi na mabadiliko makubwa kiuwajibikaji, kiuchumi na kijamii na kuwa chachu kubwa kwa ustawi wa kimaendeleo wa Taifa la Tanzania.

Hakika hakuna asie na makosa, nami nakiri kuna mahali ambako aliyumba lakini bado haiondoi uhalisia na ukweli kuwa alifanya hivyo kwa dhamira kuu ya kutetea na kupigania maslahi mapana ya Taifa letu sema kuna sehemu matokeo hayakuwa chanya japo lengo lake lilikuwa jema.

Tukijaribu kuweka katika mizani yale Mazuri na mabaya, kwa hakika mazuri ni mengi sana na mfumo wa utawala wake umejenga msingi imara kwa viongozi wengi waliopo sasa na watakaokuja baadae.

Inawezekana sio wote, ila wengi wetu ni mashahidi na tumeshuhudia mageuzi makubwa kwenye kuleta mabadiliko ya uwajibikaji serikalini, kuzuia rushwa na udanganyifu, Mfumo usio na upendeleo katika kutoa ajira, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu yenye kuleta tija kiuchumi kama Bwawa la Nyerere na Reli ya SGR, Umeme vijijini, Uboreshaji wa huduma za Afya, Ongezeko la ukusanywaji wa kodi, uboreshaji wa mikataba ya madini na gesi na vinginevyo vingi ambayo vimefanikisha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati wa chini mapema tofauti na ilivyotarajiwa.

Kwa hakika umefika wakati wa Hayati John Magufuli kupewa Heshima ya Baba wa pili wa Taifa la Tanzania, baada ya waasisi wa Taifa na Muungano ili kuyaenzi daima yale mema yote aliyoyafanya kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na hatotukuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani hata Korea Kaskazini wana Baba wawili wa Taifa, ila yote kwa yote neno langu sio Sheria, ni mawazo yangu tu, hivyo nawasilisha.

Kwenye ubora wake:

IMG_20220328_080556_745.jpg
 
Back
Top Bottom