Hayati Magufuli anapaswa kupewa Heshima ya Baba wa Pili wa Taifa la Tanzania

Hayati Magufuli anapaswa kupewa Heshima ya Baba wa Pili wa Taifa la Tanzania

Du! Huwezi kulinganisha kabisa mazuri yaliyofanywa kipindi cha Mkapa na kipindi cha Kikwete katika kujali ubora wa maisha ya kila mtu hata hao ambao wanaoitwa wanyonge na hayo mamiundombinu ya Jiwe! Huwezi kabisa linganisha! Yaani huwezi!
 
Kwa hasara ile ya bilioni 60 Kwenye ATCL huku tukiaminishwa tunapata faida Napendekeza, ajengewe na sanamu kabisa ili hata vizazi vya baadae vimfahamu
Bora hata hiyo B60 kuna ile T1.5 ya CAG Prof. Assad.

Tusubiri tu labda Samia anaeweza kuwa mama wa taifa ila baba tayari tunae Nyerere.
 
Du! Huwezi kulinganisha kabisa mazuri yaliyofanywa kipindi cha Mkapa na kipindi cha Kikwete katika kujali ubora wa maisha ya kila mtu hata hao ambao wanaoitwa wanyonge na hayo mamiundombinu ya Jiwe! Huwezi kabisa linganisha! Yaani huwezi!
Magufuli alitumia siasa za kuwadanganya wanyonge kuwa yeye ni mtetezi wao kama Camoufledge. Kuwaacha wafanya kila kitu bila kufuata sheria na kuumiza wanaooitwa mashetani ili kuwafurahisha wanyonge, kumbe anawaongezea umasikini.
 
Aitwe tu Magufuli itatosha.

Watakupiga mawe, kejeli na matusi. Ila lile

lilikuwa jembe yenye haraka sana.

Nidhamu serikalini (unanijua mimi ni nani umeisha)

Umeme haukatiki tena.

Maji yapo 24/7.

Umeme unakuja mwingine mwingi. Hadi kuuza kwa nchi jirani.

Elimu bure 12 milioni watoto wamesoma bure, labda wangekuwa vibaka, malaya, majambazi. Ukimaliza secondary unaweza kujiongeza.

Mwendo kasi,terminal three.

Nchi yote barabara ziko vizuri

Alikuwa anasema tunaweza, sisi ni nchi tajiri. Katika jitihada za kuinua uwezo wa kufikiri, to change attitude, mindset.
 
Dah! Watu wamevurugwa [emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787]
 
Back
Top Bottom