Tumezoe kwenye familia tukiulizwa anayedaiwa na Marehemu ajitokeze, anamdai Marehemu ajitokeze. Kauli hii inaungwa mkono na kampeni yakuandika husia.
Husia serikalini nikukabidhi Mali na dhamana uliyopewa kwa mrithi wako. Ni bahati mbaya kwamba Mzee wetu JPM alitwaliwa katika ulimwengu huu bila kukabidhi ofisi kwa mrithi wake.
Kwa mazingira haya yapo Mambo yaliyokuwa kwenye kumbukumbu na mengine hayakuwa kwenye kumbukumbu yalibaki vifuani mwa aliowaamini. Mambo hayo yanahusu rasilimali zetu na nchi yetu, yapo aliyokataza na akaweka sababu na yapo aliyoruhusu nakuweka sababu.
Kwa awamu mpya, katika mazingira Kama haya Ni vigumu nchi ikakabidhiwa kwenu na aliyekuwa anaiongozi ila inaweza ikakabidhiwa kwenu na waliokuwa wasaidizi wake. Hii siyo hiari ya mtu bali ni lazima, kila aliyekabidhiwa Siri na rasilimali flani kwakuaminiwa anapaswa kujitokeza na kuueleza utawala uliopo. Kushindwa kufanya hivyo nikuwahujumu wananchi.
Niwaombe mliopo madarakani, tafuteni kwa mbinu zenu zote Mali, amana na Siri za nchi ALIZOKABIDHIWA Jpm . Tafuteni mzijue, tafuteni kwa nguvu kubwa kwani mtakumbuka hata msiri mkubwa na mtendaji mkuu wa serikali iliyopita alitangulia mbele ya haki kabla ajakabidhi ofisi. Mnalojukumu lakulinganisha mlichokikuta na kilichopaswa kukutwa.
Msifanye kosa mkaamini hakuna yaliyojificha, yapo na Wapo wanaoyajua, anaweza kuwa Ni mtunza kumbukumbu masijala, anaweza kuwa mlinzi, anaweza kuwa sekretari au mtu mwingine wa chini ofisini. Msiwadharau zungumzeni nao watawapa pakuanzia ili kuepusha kusafiri gizani.
Lakini pia Wapo wakubwa wanalakutueleza. Hili kufanikisha niwaombe msiwaone waliokuwepo ofisini Kama maadui. Waoneni kam
Watumishi wengine wa umma mliowaweka ninyi. Msipokubali kujadiliana na waliokuwepo mtashindwa kuwa na mwanzo mzuri.
I propose this to be means of handing over Government affairs at this stake,ignore no one