Hayati Mkapa vs Hayati Magufuli nani akumbukwe zaidi?

Hayati Mkapa vs Hayati Magufuli nani akumbukwe zaidi?

Mbogi

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2021
Posts
803
Reaction score
997
Japokuwa mikakati ya kiutekelezaji ilitofautiana,viongozi Hawa walikuwa na itikadi zenye maono yanayokaribia kufanana hasa katika kujitegemea,kuondokana na madeni na kutumia fedha zetu za ndani.

Hivyo basi tupitie japo kwa uchache mafanikio yao katika kulijenga taifa letu nawe mchangiaji unaweza kuongeza mafanikio utakayoyakumbuka.

Mkapa;
Alifanikiwa kulipa kiasi kikubwa Kati ya deni la dola billion 7 na tukawa hautudaiwi kwa maana ya kuanza kutumia fedha zetu.

Kuna msemo usio rasmi, asamehewaye kikubwa hukumbuka zaidi, na asamehewaye kidogo hukumbuka kidogo. Mkapa alituwezesha kulipa na kusamehewa deni kubwa ni wazi kuwa tutakumbuka zaidi.

Aliweza kutengeneza mifumo mipya ya kisekta katika kusimamia uchumi na huduma za jamii, mifumo hiyo inatumika hadi sasa, mfano; tra,nhif,ppra,ewura,sumatra,vat, ya road, takukuru, nk.

Ameacha alama kubwa Sana iliyowaondelea maumivu ya kikoloni Wananchi wote na inayoendelea hadi sasa kuwa kufuta kodi ya kichwa na kuanzisha VAT.

Kwetu wapenda soka uwanja ni alama tosha.

Magufuli;
Ameweza kumsaidia Mkapa, Kikwete na yeye pia akiwa Rais kujenga barabara,madaraja, na flyover kwa kutumia nyenzo na mifumo iliyobuniwa na mkapa kama vile tanroads.

Ameweza kujenga na kuboresha huduma za kijamii kwa kutumia nyenzo za tra, ewura, nhif, tasaf,nk

Ameweza kujenga reli sgr, bwawa, kufungua atcl nk.

Ongezea.....
 
Atakayeipa nchi Katiba mpya ya wananchi ndiye atakumbukwa zaidi.
Na hakuna na wala hatatokea,hata Mbowe Urais ukimdondokea hawezi badilisha hiyo Katiba ya Mwalimu!!
 
Wote wana mazuri na mabaya yao...

Mbele yao nyuma yetu...
 
Utawala wa Wakristo huwa ni maumivu kwa watz. Ndo maana waislamu wanaishi miaka mingi.
 
Back
Top Bottom