Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,153
- 3,800
Nimesikiliza sera mbalimbali za vyama vyetu kuelekea uchaguzi Mkuu 2020.
Kuna watu wanaaminishwa huku vijijini kuwa ukichagua mpinzani kutatokea vita.
Pia nimesikia baadhi ya redio na Tvs na kauli hata za viongozi wa juu kutoa mifano kama ya Rwanda, Libya, Misri nk kuwa ndiyo picha ya matokeo ya kuchagua upinzani. Historia haionyeshi hata chembe kuwa vurugu za nchi hizo chimbuko ni wao kuchagua upinzani bali ni madhaifu ya watawala wa wakati huo katika mambo ya kidini,ukabila,chuki nkHili limenisikitisha sana hasa unaposikiliza sera za vyama vya upinzani wanavyohubiri amani.
Ninachokiona zaidi ni hofu iliyotanda kwa waliojichotea mali tiyari hasa security ya mali zao hasa zile za kifisadi.
Kuna watu nchi hii wamepata mali bila kutumia njia za haki! Hivyo, akitokeza mwenye sera za mrengo wa kudai haki,lazima hofu itande kwa mdhulumaji!
Nimeona majirani zetu Malawi wakichagua upinzani,sijaona vurugu.
Mwl. Nyerere kwangu nilimuona kama mpinzani mahiri anayeweza kutumika kuekezea dhana ya upinzani katika medani za siasa, uhuru na maendeleo. Alipenda sana kutumia neno " mapinduzi". Hili neno kwa viongozi wa leo hawalitumii sana sijajua wanahofia nini au ni kutokuelewa mapinduzi inamaanisha nini.
Hivyo, mpinzani wa kisiasa na au kisera namuona kama mwanamapinduzi tuu na siyo muasi