Ndugu zangu Watanzania,
Niliwaambieni Sana ,niliwaeleza sana CHADEMA, niliwapa Elimu wana CHADEMA,niliwatahadhalisha wana CHADEMA kuwa kumchagua Lissu kuwa Mwenyekiti ilikuwa ni sawa na kujipiga kitanzi,ilikuwa ni kujitundika juu ya kamba na kuweka shingo ndani yake na kisha kutegua kiti chini, ilikuwa ni kujitupa katika mdomo wa mamba, ilikuwa ni kuhatarisha uhai na ustawi wa chama,Ilikuwa ni kujimwagia petroli mwili mzima na kisha kuukumbatia moto,ilikuwa ni kujivalisha mabomu.
Niliwaambieni mara nyingi sana kuwa Akili ya Lissu haiwezi kuiongoza CHADEMA hata kwa mwezi mmoja tu. Niliwaambieni ya kuwa lissu hana akili ,wala uwezo wa kuweza kuiongoza CHADEMA na kuunganisha watu. Nilisema lissu hawezi kuyaleta pamoja makundi yote yenye mitizamo tofauti na kufikiri tofauti.
Nilisema lissu siyo kiongozi ,siyo mtu wa kuongoza njia ,siyo mtu wa kuongoza kundi. Nilisema lissu hapaswi kuwa mtu wa mwisho kiuongozi na kimaamuzi. Nilisema lissu anapaswa kuwa na mtu juu yake wa kumuongoza na kumdhibiti pamoja na kumpatia maelekezo na kumtuliza . Nilisema lissu anapaswa kuongozwa njia kwa sababu yeye binafsi hana uwezo wa kujiongoza na kuongoza wenzake.
Nilisema Lissu ni mtu aliyejaa Mihemuko, ukurupukaji,jazba, utoto na ujuaji. Nilisema kuwa pamoja na kuwa Lissu ni mkubwa kiumri na umbo kubwa lakini akili yake bado ni ndogo sana na changa sana linapokuja suala la uongozi na kuongoza watu. Hana maarifa wala uwezo wa kuvunja makundi kwa wale anaotofautiana nao.
Nilisema Mdomo wa lissu hauna breki wala kiasi. Lissu aliisambaratisha na kuigawa CHADEMA kabla hata hajawa Mwenyekiti, aliumiza watu ,kujeruhi watu ,kuwapaka matope watu, kuvuruga chama na kukifedhehesha na kukitia aibu chama ambacho alikuwa anataka kuja kukiongoza baadaye. Sasa ni vipi angeongoza chama na wanachama ambao tayari alikuwa amewaumiza ,kuwajeruhi ,kuwavunjia heshima ,kuwatweza na kuwashushia heshima zao?
Angejenga vipi chama ambacho alikibomoa wakati wote wa kampeni zake? Angefanikiwa vipi wakati alikuwa amemparua na kumpaka matope kila mtu? Angesonga vipi mbele wakati alikuwa tayari amewavunja mioyo watu wengi ndani ya chama ? Angepata vipi ushirikiano wakati alifanya kampeni chafu za kuwachafua wenzake ,kuwasiriba kwa matope na kuwatolea maneno machafu na yenye kuwashushia heshima ambayo wameijenga kwa jasho ,damu na Machozi kwa miaka Mingi?
Ni vipi mbowe aliyekijenga CHADEMA kwa jasho ,Damu na machozi yasiyokatika angeweza kumuunga mkono lissu ambaye wakati wote wa kampeni zake kwa kutumia vibaraka wake wasio na mbele wala nyuma na waliokosa adabu na malezi mazuri ya mama zao walifanya kazi ya kumtukana Mheshimiwa Mbowe,kutoa tuhuma za uongo, uzushi na uchonganishi?
Hivi Lissu huyu alikuwa ni wa kumdhalilisha Mbowe kiasi kile kweli? Mbowe huyu aliyempigania Lissu kuhakikisha anakwenda Kenya kupata matibabu alikuwa ni wa kudhalilishwa na Lissu kweli? Mbowe huyu aliyetoa mali zake na pesa zake kuijenga CHADEMA na kumkaribisha lissu chamani alikuwa ni wakumtukana Mbowe kweli? Kama siyo laana ni nini ndugu zangu?
Hivi lissu ni mzima kichwani kweli? Anajitambua kweli? Anamshipa wa aibu kweli?
.ndio maana nilisema kuwa CHADEMA ilikuwa inamhitaji Mwamba Freeman Mbowe Jabali na Nguli wa Siasa za upinzani hapa Nchini kuendelea kuiongoza CHADEMA. Kwa kuwa Huyu ni kiongozi Makini,mtulivu na mwenye akili ,maarifa ,upeo na uwezo mkubwa sana wa kiuongozi.
Ndio maana CHADEMA iliendelea kustawi na kufanya vyema sana na kuwa chama imara na chenye kuaminika na watanzania wa makundi mbalimbali katika kipindi chote cha uongozi wake wa miaka 20. Alijua namna ya kupata viongozi wa kuweza kushika nafasi mbalimbali za uongozi,alijua kukuza vipaji vya vijana alijua namna ya kuwalea vijana . Na kwa hakika mikono yake ilipika viongozi wengi sana ambao leo hii wengi wao wanatumiwa na serikali yetu katika nafasi na ngazi mbalimbali za uongozi.
Ndio maana anaitwa Mwamba .na kwa hakika aliivusha CHADEMA katika nyakati zote katika milima na mabonde na chama kikabakia salama.
Sasa huyu Lissu anayechangiwa pesa ya Fomu na kushauriwa na watu wahuni wahuni na waliokosa adabu na malezi ya Mama zao aina ya SATIVA watamshauri nini lissu akapata akili na maarifa ya kuongoza chama? Watu kama Maria Sarungi waliojikatia tamaa ya Maisha watamshauri nini lissu ambaye yeye mwenyewe kichwa chake hakijatulia? Nani wa kumtuliza sasa Mihemuko yake huyo mtu?
Embu angalia wakati wa Mwamba alikuwa na watu kama akina Profesa Baregu Msomi Nguli wa Sayansi ya Siasa. Unafikiri nini kingeharibika mbele ya Mwamba huyo? Unafikiri angekosa ushauri wa namna ya kuongoza chama?
Mwamba Mbowe .Wewe endelea kuchekaa tu Maana Mungu Amelipa machozi yako.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.