Hayupo mwenye kuridhia Katiba Mpya kwenye Mitano yake ya Mwanzo

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Ikumbukwe katiba iliyopo iliasisiwa kwa lengo la kuufanya utawala wa CCM kuendelea kudumu.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

Rais gani wa CCM ataafiki uwezekano wa mabadiliko ya katiba ndani ya awamu yake ya kwanza katika 2 anazopewa?

Asijipende vipi mtu huyo?

Inawezekana ni kwa mantiki hiyo kwamba sarakasi hizi za katiba mpya iwe baada ya 2025 tunaziona sasa.

Mh. Rais Samia hana haja ya katiba mpya kwenye mitano hii labda kwenye ile mitano mingine!

Ni vizuri kuujua ukweli mchungu huu ili kuukubali au kuukataa.

Kunyoa au kusuka yote si ni uamuzi mikononi mwetu?

Stefano Mengele anajua vyema.
 
Nilisoma hapajF kwamba yako mambo 72 yalipigwa chini kutoka kwenye ile Rasimu ya tume ya Mh judge Warioba ni yepi hayo? Na hiki ndicho kilicho sababishwa kuzaliwa UKAWA.
 
Nilisoma hapajF kwamba yako mambo 72 yalipigwa chini kutoka kwenye ile Rasmu ya tune ya Mh judge Warioba ni yepe hayo? Nachiki ndicho kilicho sababishwackuzaliwa UKAWA.

Kumbuka kuna katiba ya Warioba na katiba pendekezwa.

Katiba pendekezwa ni katiba ya CCM. Katiba ya Warioba ni katiba ya wananchi.

Swali lako linaeleweka vyema, lakini tulipo kujikita huko itakuwa ni kama kupoteza muda tu kwa sasa.

La msingi, tulipo tunakubali mchakato huu kuanza baada ya 2025 au la?

Baada ya hapo ndipo suala litakuja pa kuanzia ni wapi? Na tofauti zilizopo ni zipi?

Kumbuka hata ile ya Warioba nayo kuna mambo imeshapitwa nayo wakati.
 
Hatua mbili zimeshafanyika ili kufikia lengo la kurudi ikulu 2025.

1. Kuwaondoa waliokuwa wasaidizi wasumbufu kwa kuteua wengine hasa watoto wa marafiki zake.

2. Katiba Mpya isubiri, hii inakuja ili kuwapa nafasi ya kuchakachukua kwenye uchaguzi mkuu 2025 kwa kutumia mapungufu yaliyopo kwenye hii Katiba yetu hasa uwepo wa Tume feki ya uchaguzi.
 
Rais anayeitizama Tanzania zaidi ya miaka 10 tu anayoamini anapaswa kuitawala.
Mzalendo wa kweli ambaye kwake Tanzania ni kubwa kuliko maslahi yake binafsi na chama chake.
 
Hawana uzalendo. Unaosemekana uzalendo ni kwa ajili ya matumbo yao.

Ninakazia: "Hayupo rais wa CCM ataridhia katiba kubadilika kwenye awamu yake ya kwanza."

Sana sana kwenye mitano mingine na hapo kama tutakomaa kama alivyokomaliwa Mengele!
 
Mungu wa Mbinguni akitaka lake lazima liwe, huu kwenye vitabu vya Musa unaitwa upako wa mnara wa Babeli lugha gongana. Hii kama sura ya Mh Waziri flani hivi.

Hii ndio sababu wengine tuna asa kwa nia njema wanaotuongaza. Itisheni mchakato wa katiba mpya muda si rafiki kwenu. Joto la kuidai Katiba mpya litakalo anza baada ya kanuni za mikutano ya kisiasa kutoka naona iko kila dalili litakuwa gumu sana kulihimili.

Ni bora huu mchakato ukanza na kuwa controlled na tukapata katiba ya manufaa kwa kada zote za kitanzania, muda si rafiki na hayuko wa kuuzuia uwe baada ya 2025. Labda wapewe hicho wanachokiita tume Huru ya uchaguzi wadau wairidhie, nasema labda.
 
Kumbuka kuna katiba ya Warioba na katiba pendekezwa.

Katiba pendekezwa ni katiba ya CCM. Katiba ya Warioba ni katiba ya wananchi.

Swali lako linaeleweka vyema, lakini tulipo kujikita huko itakuwa ni kama kupoteza muda tu kwa sasa.

La msingi, tulipo tunakubali mchakato huu kuanza baada ya 2025 au la?

Baada ya hapo ndipo suala litakuja pa kuanzia ni wapi? Na tofauti zilizopo ni zipi?

Kumbuka hata ile ya Warioba nayo kuna mambo imeshapitwa nayo wakati.
Rasimu ya mabadiliko ya Katiba ya Time ya Warioba na Katiba pendendekezwa vyote lazima kuna vifungu,maoni au mapendekezo yake mengine yatakuwa yameshapitwa na wakati.
Muhimu ni makubaliano miongoni mwa wananchi,tunaanzia pale alipoishia Mh.Warioba na tume yake na kuboresha zaidi kwa weledi tukiwa na sober minds.Siyo wengine hawataki wengine wanataka.Tunahitaji makubaliano zaidi kuliko kingine ili Tanzania irejee katika nafasi yake ya ukinara wa siasa za Haki na amani barani Afrika na Duniani.
Wanaokataa Katiba mpya wameidhoofisha sana nchi yetu.Tunaweza kutengeneza Katiba ya mfano kushinda wengine Ila ubishi na ubinafsi Wa wana CCM umeidumaza nchi yetu.
 
Pa kwanza ambapo ni muhimu zaidi ni lini?

Kabla au baada ya 2025. Kumtegemea Samia hilo tujue haipo katiba mpya. Kwa pressure ya kutosha baada ya 2025.

Kwa pressure kama iliyomkuta Stefano Mengele katiba mpya ni sasa.

Kusuka au kunyoa uamuzi ni wetu.
 
Kwa utaratibu wa desturi za CCM ambazo hazijabadilika wote tunajua panapo uzima na afya 2025 mgombea wao ni Mh Rais na Mkt Taifa SSH. Wajue kinachoenda kumkwamisha ni mchakato wa katiba mpya. Kwa hulka ya wanaCCM walivyo wako ambao watataka kumkwamwisha kwa kisingizio cha mchakato wa Katiba Mpya. Na watawafinesi wanaoidai katiba mpya. Ukweli usemwe.

Chaguo liko juu kwa Mh Rais na wanao mshauri. Aanzishe mchakato wa Katiba mpya ambao inaweza kuwa karata yake ya kumpa sifa kwa Wananchi walio wengi kumchagua 2025. Na hata kama hakuchaguliwa atakuwa amejijengea Heshima kubwa sana kwake na uzao wake. Niliona habari mahali Rais SSH kama Mama na Bibi "Uzao"
 
Mungu wa Mbinguni akitaka lake lazima liwe, huu kwenye vitabu vya Musa unaitwa upako wa mnara wa Babeli lugha gongana. Hii kama sura ya Mh Waziri flani hivi.

Hii ndio sababu wengine tuna asa kwa nia njema wanaotuongaza. Itisheni mchakato wa katiba mpya muda si rafiki kwenu. Joto la kuidai Katiba mpya litakalo anza baada ya kanuni za mikutano ya kisiasa kutoka naona iko kila dalili litakuwa gumu sana kulihimili.

Ni bora huu mchakato ukanza na kuwa controlled na tukapata katiba ya manufaa kwa kada zote za kitanzania, muda si rafiki na hayuko wa kuuzuia uwe baada ya 2025. Labda wapewe hicho wanachokiita tume Huru ya uchaguzi wadau wairidhie, nasema labda.

Wenyewe wanasema Dua la kuku halimpati mwewe.

Ni kweli tumeanza zamani sana kuasa na bado wanatuona kama mazuzu tu:

Katiba Mpya: Heri Rais Samia akaruhusu mchakato, asisubiri mashinikizo

Ngoja tuone.
 
Ikumbukwe katiba iliyopo iliasisiwa kwa lengo la kuufanya utawala wa CCM kuendelea kudumu.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

Rais gani wa CCM ataafiki uwezekano wa mabadiliko ya katiba ndani ya awamu yake ya kwanza katika 2 anazopewa?

Asijipende vipi mtu huyo?

Inawezekana ni kwa mantiki hiyo kwamba sarakasi hizi za katiba mpya iwe baada ya 2025 tunaziona sasa.

Mh. Rais Samia hana haja ya katiba mpya kwenye mitano hii labda kwenye ile mitano mingine!

Ni vizuri kuujua ukweli mchungu huu ili kuukubali au kuukataa.

Kunyoa au kusuka yote si ni uamuzi mikononi mwetu.

Stefano Mengele anajua vyema.
Mtu safi mwenye hofu ya m/mungu anaanzaje kuogopa katiba?? Kiongozi ni mchungaji na kila mchungaji wataulizwa siku ya mwisho kwa vile vitu walivyovichunga,
.
Mtu mwizi/bandido hataweza kukubali katiba mpya
 
Back
Top Bottom