Hayupo mwenye kuridhia Katiba Mpya kwenye Mitano yake ya Mwanzo

"hayuko wa kuuzuia uwe baada ya 2025"

Nimenukuu huo mstari. Umeandika utadhani uko Sudan au Mali au Gabon.

Watanzania wa kwenda kudai Katiba kwa style hiyo hawapo
 
"hayuko wa kuuzuia uwe baada ya 2025"

Nimenukuu huo mstari. Umeandika utadhani uko Sudan au Mali au Gabon.

Watanzania wa kwenda kudai Katiba kwa style hiyo hawapo

Tafuta kwenye Biblia kitu kinachoitwa ukuta wa Yeriko na ulivyo angushwa. Yakobo 5:17-18
 
"hayuko wa kuuzuia uwe baada ya 2025"

Nimenukuu huo mstari. Umeandika utadhani uko Sudan au Mali au Gabon.

Watanzania wa kwenda kudai Katiba kwa style hiyo hawapo

Mkuu mawazo kama yako yalishajadiliwa sana humu. Uzi huu unahusika:

Katiba Mpya: Ukweli Usiosemeka

Unasomeka kuwa:

1. Wadai katiba ni wastaarabu wasiotaka kutumia nguvu au makabiliano yoyote ya kuhusisha nguvu.

2. Wadai katiba wako tayari kususia chaguzi zote bila ya kuwa na tume huru au katiba mpya.

Zama zimebadilika:

Rais Samia, akili za kuambiwa changanya na za kwako
 
Sijawahi kuikubali Katiba Pendekezwa,ninaposhauri kuwa ifanyiwe maboresho maana yake yaingizwe/yarudishwe mawazo ya wananchi ambayo CCM iliyaondoa wakati ule Wa Bunge la katiba.
Nimekuwa upande wa wanaounga mkono Rasimu ya Tume Mabadiliko ya Katibailiyoongozwa na Jaji Warioba.Niliumia sana tuliposhuhudia kina Sanga walipocheza sebene bungeni walipopitisha katiba Pendekezwa ya ccm.Maombi yetu yaliwapofusha ccm wakaogopa kuileta kwa wananchi.
Hata hivyo kadiri ya miaka ilivyopita na mabadiliko ya nyakati sioni ubaya kufanya maboresho ya Yale maoni.
Nakushukuru kwa hoja mujarab na jinsi unavyopigania upatikanaji Wa katiba mpya.Kwa pamoja tutaweza.
 

Katiba pendekezwa haina lenye kuzingatiwa:



Pa kuanzia ni tume ya Warioba kama msingi.
 
Amani iwe juu yenu.

Leo nimesikitishwa sana na hoja za wenyeviti vya uvccm wilaya za Kinondoni, Ubungo na kigamboni kwa hoja zao tatu zifuatazo:

1. Wanaccm hawa wanaipinga Katiba mpya kwa nguvu kubwa sana as if anayeitaka katiba ni mpinzani wao tu, bila kujua katiba ni Mali ya Mwananchi na sio chama fulani. Dunia ya sasa kupinga mabadiliko ya katiba ili kuendana na wakati wa sasa unahitaji kuwa na akili ngumu sana. KATIBA MPYA ILITAKIWA NDIO IWE AJENDA YAO TANGU NA MAPEMA SEMA WALICHELEWA SANA.

2. Wanaccm kutaka katiba mpya iwe kwanza kwenye ilani yao ya chama ndio wafanye mabadiliko au kuandika mpya inakupa picha ya uwezo wao wa akili. Leo nimeona AIBU mwenyekiti uvccm kusema katiba mpya haipo kwenye ilani yao ya chama INASIKITISHA SANA. NI VILE TU WANANCHI NAO HAWAJITAMBUI.

3. Kwa Dunia ya sasa kujinadi kwenye uchaguzi kwamba umejenga madarasa, barabara, hospitali na vituo vya afya inahitajika roho ngumu sana kwa kweli mana hivyo vitu hata wakoloni walifanya na bado tuliwaondoa. Tanzania ya sasa sio ya wajinga wa miaka ile ya 2010 kurudi nyuma.

USHAURI KWA CCM

1. Muache UCHAWA badala yake muwe wa kweli ili muendane na wakati na mahitaji ya sasa. Punguzeni watu wenye akili ndogo kwenye chama chenu maana wengi wenu ni empty set, mpo kutafuta fursa tu za uteuzi.

2. Ibebeni ajenda ya katiba mpya vinginevyo huwenda mambo yakawageukia mbeleni. Yule bwana mpaka kuamua kuiba uchaguzi wa 2020 aliona mbele kiza sio bure bure tu. Msaidieni Mama na vile sio MUONGO atapata tabu sana 2025.

3. RUDISHENI CHAMA MIKONONI MWA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI.

Inakera mno kuwasikiliza wanaccm wallah....

Usiku mwema.
 
Subiri uone huyu. Atalegea tu. Nguvu ya wananchi usicheze nayo. Hatuwezi kuruhusu wizi uendelee forever. Tumekwishajua kuwa anataka kubaki madarakani kwa hila, halafu tukubali? Haiwezekani.
Yumkini aliyekuwa mwenyekiti bunge la katiba leo ni rais.

Ninakazia: "Hayupo rais wa CCM ataridhia katiba kubadilika kwenye awamu yake ya kwanza."

Sana sana kwenye mitano mingine na hapo kama tutakomaa kama alivyokomaliwa Mengele!
 
Tafuta kwenye Biblia kitu kinachoitwa ukuta wa Yeriko na ulivyo angushwa. Yakobo 5:17-18
Tanzania siyo biblia wewe wacha upumbavu. Kuna wanaoamini Korani, kuna wapagani, Wahindu na wanaoamini dini za kienyeji. Utatumua vipi mstari wa kitabu chako kutoa hoja ya kisiasa?
 
Tanzania siyo biblia wewe wacha upumbavu. Kuna wanaoamini Korani, kuna wapagani, Wahindu na wanaoamini dini za kienyeji. Utatumua vipi mstari wa kitabu chako kutoa hoja ya kisiasa?

Hakuna aliye kukataza wewe kutumia mistari ya miungu ya jezebeli kujengea hoja za kisiasa. Hujaona viongozi wakisiasa wakitumia mistari ya Kitabu cha Neno la Mungu "Yesu" katika hotuba zao za kisiasa.
 
Hakuna aliye kukataza wewe kutumia mistari ya miungu ya jezebeli kujengea hoja za kisiasa. Hujaona viongozi wakisiasa wakitumia mistari ya Kitabu cha Neno la Mungu "Yesu" katika hotuba zao z kisiasa.

Ukiona hivyo ujue kaguswa. Asikupe pressure huyo. Na safari mbona kitanuka?
 
Umewaza vyema,

Ulichosahau ni kuwa aliyepo ni one term leader.
 
Umewaza vyema,

Ulichosahau ni kuwa aliyepo ni one term leader.
Ingekuwa hivyo angeweka mazingira mazuri ya kupatikana katiba mpya sasa. Kwamba kina Polepole wametupwa Cuba huko huyu anataka term ya pili na hayupo mwenye kumsimamisha!

Katiba mpya term 2 hiyo hana tatizo nayo. Si Sasa.
 
Ingekuwa hivyo angeweka mazingira mazuri ya kupatikana katiba mpya sasa. Kwamba kina Polepole wametupwa Cuba huko huyu anataka term ya pili na hayupo mwenye kumsimamisha!

Katiba mpya term 2 hiyo hana tatizo nayo. Si Sasa.
Tanzania inaingia msimu mpya na majira mapya, 2026 ndo mwaka wa KATIBA mpya kukamilika.

Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakupa Ishara juu ya Uchaguzi wa 2025.

Haitakuwa kawaida kama ulivyozoea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…