HDTV Antenna

mwenebhukabo

Member
Joined
Mar 2, 2014
Posts
24
Reaction score
11
Habarini za wakati huu wakuu

Niliona sehemu mtandaoni wanauna kadubwasha kanaitwa "HDTV Antenna" kana uwezo wa kupata idadi kubwa cha tv channels kwa kukaweka katika muelekeo fulani kama dish.Nimevutiwa kukanunua ila sina hakika kama kwa nchi ya Tanzania kanaweza fanya kazi au la.Kwa wenye uzoefu nacho naombeni tuchangie mawazo.
Asanteni.
 
Pengine hawaifahamu,natumai atakapofika anaejua atatujuza!!!
 
Mkuu hiki kidude sikielewi ila kimekaa kihuni huni sana. Mfano.

1. Wameandika 200 miles amplifier inamaana kinategemea mawimbi yawe karibu na wewe kwa Maili hizo 200 toka eneo lolote la Tanzania huzipati hizo chanell.

2. Wameandika HDTV halafu 4k view ni vitu viwili vinakinzana.

3. Vitu kama coaxial, long cable ama 360 degree reception havimake sense kwangu, na sio specs zinazokusaidia kukijua kifaa.

Na utumizi wa hilo neno Antenna inaama hakitumii satelite au internet, kwa ninavyoona mimi matapeli wapo kazini hicho kifaa hakitafanya kazi hapa nyumbani na hutaziona hizo chanell.
 
Kinauzwa shilingi elfu kumi ,nilijaribu kupitia youtube japo napo pia inaonesha ni kitu fulani hakieleweki maana hata hizo towers sijui kama zipo.kwa ajili ya udadisi nimekiagiza na kipo njiani kinakuja. Ila sina hakika kwa kweli na utendaji wake kila ninaemuuliza hafahamu.
 
😊ngoja kije mkuu
 
Kimekuja kinashika channel za startimes zote, za free kama ITV,EATV,TV1,Safari zinaonekana ila za kulipia zinakua 'scrambled'. Pengine provider pekee ni Startimes.
Ni DVB-T receiver then, Asante kwa mrejesho.
 
Kimekuja kinashika channel za startimes zote, za free kama ITV,EATV,TV1,Safari zinaonekana ila za kulipia zinakua 'scrambled'. Pengine provider pekee ni Startimes.

umenunua wapi na mimi nikinunue
 
hivyo vi antena niliewahi kufuatilia nikagundua kwanza ni antenna ya kawaida ambayo haina active compnent yoyote kwa hiyo haiwezi kung'amua signal kwenye tv isiyo na kingamuzi.

Wanasema ina amplifier/booster lakini iko separate haiji na antenna.

pili hiyo antena inaReplace tu antenna yako ya dekoda au tv yenye dekoda ndani.


Mleta mada tuambie TV yako ina InBuilt dekoda au TV ya analog?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…