Raha ya uchaguzi huu ni pamoja na tunavyoelimika. Mimi leo naelimisha jambo moja tu nalo ni kanuni mpya za uchaguzi wa mwaka huu.
Kabla ya kuongelea kanuni hizo tujikumbushe siku ya kupiga kura huwa inaendaje.
Katika chaguzi zilizopita watu wakishamaliza kupiga kura kura zinaanza kuhesabiwa pale kituoni. Zoezi hili linafanyika na mawakala wa wagombea wote wanatakiwa kuwepo.
Wakala anashiriki hatua zote, kura zikihesabiwa naye anashiriki. Jumla ya kura za kila chama inaandikwa kwenye fomu, wote tume na mawakala wanaisaini yale matokeo kwenye ile fomu ikiwa na kopi za vyama vyote.
Wakala akishagawiwa kopi yake kazi inakuwa imeisha. Wakala kupewa fomu ni ushahidi kama ameibiwa au hakuibiwa. Kashinda kihalali au kashindwa kihalali.
Kituo pia kinapata kopi yake inayobandikwa pale nje kituoni.
Kazi hii huwa si ngumu kwani hesabu zenyewe ni za kujumlisha za darasa la nne. Vituo vingine kuanzia saa 11:30 huwa tayari wameshajua matokeo.
Kiukweli ni kwamba uwezo wa kumjua rais kabla ya saa 02:00 usiku upo tena ni uwezo wa kila mmoja wetu. Ukiwa na computer yako ukaenda kwenye "Microsoft excel" ukapata matokeo ya vituo vyote nchi nzima unaweza kuyajua matokeo yote kufikia saa 02:00 usiku.
Matukio haya yote yanaongozwa na sheria "Sheria ya Uchaguzi" kwa Kiingereza inaitwa "National Elections Act, [Cap. 343, R.E. 2010]".
Maadamu sasa naeleza sheria nana kwanza tuchambue uwezo wa kisheria wa Tume ya Uchaguzi. Mwenyekiti wa Tume ni Justice Semistocle Kaijage yaani alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Hata alipokuwa Mahakama Kuu mtakumbuka mwaka 2011 ndiye aliyetoa hukumu ya kuifilisi IPTL. Hivyo siyo mbabaishaji tulitarajia anajua haki ni nini na sheria ni nini za ndani na za kimataifa.
Majaji wengine ninaowasikia wako humo nao tunatarajia wanajua vizuri sheria maana maamuzi wanayotoa ni tafsiri ya walivvyokuwa mahakamani.
Sasa turejee katika "Sheria ya Uchaguzi". Sheria hii imeweka uwezo wa kutungwa kanuni za uchaguzi.
Kama tulivyoona, miaka yote mawakala hupewa kopi ya matokeo ya pale kituoni. Sasa mwaka huu kanuni inasema watapewa fomu za matokeo "KAMA ZITAKUWEPO". Hapa ndipo penye tatizo yaani kanuni imeongeza maneno "KAMA ZITAKUWEPO".
Kanuni hii ina ubatili wa kimantiki na kisheria ninaanza kimantiki kama ifuatavyo.
Mantiki ya kwanza ni hivi. Sheria au kanuni yoyote hutungwa ili kukabili tatizo. Hakuna mtanzania anayeweza kueleza kanuni hii imeongezwa kuzuia tatizo gani. Hapa maana yake wakala atahesabu kura lakini mwaka huu anaweza asipewe kopi yake ya fomu ya matokeo.
Kimantiki ni kwamba mwaka huu tume imejiandaa fomu kutokuwepo na ndiyo maana limeongezwa hilo neno "KAMA ZITAKUWEPO".
Hili ni jambo la ajabu duniani kutokea! Hata mtoto mdogo anajua kwamba ukinunua kitu halafu usipewe risiti huyo anayekunyima risiti anatengeneza mwanya wa kuiba.
Serikali hii ndiyo inayosisitiza kudai risiti kwa kila kitu kwa kukomesha wakwepa kodi. Huwezi kudhibiti wezi wa kodi halafu usidhibiti wezi wa kura ambao hawatoi risiti (fomu) ya matokeo ya uchaguzi.
Mawakala wasipopewa fomu tume itaweza kutangaza matokeo yoyote inayoyataka, Yaani inaweza kumpa mgombea mmoja asilimia 85 na mwingine asilimia 13 na mwingine 2.
Hivyo hili kosa linatakiwa kuanikwa kama lilivyoanza kuanikwa. Lengo ni kwamba kila mtu duniani na kila nchi duniani na kila taasisi duniani inayotutazama ione kinachoandaliwa kufanywa.
Mantiki ya pili ni hivi. Siku zote ushindi wa kujivunia ni ule ushindi halali. Hivi ni chama gani kinachopenda mawakala wakose fomu mwaka huu? Je, ni chama gani hakipendi matokeo yote ya kituoni tuyajue?
Hizi fomu ya matokeo ni ushahidi kwamba umeshinda kihalali au umeiba au umeibiwa. Sasa ni chama gani kimelengwa kikose ushahidi wa kuibiwa matokeo kama kitaibiwa?
Umantiki wa tatu ni wa kisheria ambao nao uko hivi.
Hii "Sheria ya Uchaguzi" imesema kila wakala atapewa fomu za matokeo. "Sheria ya Uchaguzi" ndiyo imezaa "Kanuni za Uchaguzi". Sasa mwaka huu kanuni inataka wakala kupewa fomu "KAMA ZITAKUWEPO". Sheria mama haisemi hivyo inasema lazima watapewa fomu.
Hivyo kanuni hii imekiuka "sheria mama". Je, kanuni ikienda kinyume na "sheria mama" mambo yanakuwaje"?
Jibu linatolewa na "Sheria ya Tafsiri" inayoitwa Interpretation of Laws Act, [Cap. 1, R.E. 2002]. Kifungu cha 36(1) cha hii "Sheria ya Tafsiri" kinasema hivi,
"subsidiary legislation shall not be inconsistent with the provisions of the written law under which it is made, or of any Act, and subsidiary legislation shall be void to the extent of any such inconsistency."
Sentensi hii nimeitafsiri hivi:
"ni marufuku kwa sheria ndogo kupingana na vifungu vya sheria mama iliyoiweka hiyo sheria ndogo na ikitokea ikapingana basi kifungu cha sheria ndogo kitakuwa batili na itafuatwa sheria mama inavyotaka."
Katika hili suala Kanuni za Uchaguzi ni "sheria ndogo" wakati sheria mama ni "Sheria ya Uchaguzi". Hivyo kanuni hii yenye maneno "KAMA ZITAKUWEPO" imekiuka "sheria mama" hivyo ni kanuni batili.
Sasa kanuni inapokuwa batili, kama hii, kinafanyika nini? Jibu wote sasa hivi tunalijua.
Mwezi jana tumeona sheria inasema fomu za wadhamini wa urais zinahakikiwa na tume yenyewe pale makao makuu wakati Tume ilielekeza fomu zihakikiwe na wakurugenzi mikoani.
Kwa mujibu wa kile kifungu cha 36(1) cha "Sheria ya Tafsiri" maelekezo ya tume aliyokataa Tundu Lissu yalikiuka sheria mama.
Wagombea urais walifuata maelekezo batili ya tume. Tundu Lissu ndiye alifuata sheria inavyoelekeza.
Vivyohivyo kanuni hii ya mwaka huu imekiuka sheria mama. Hivi ndivyo kanuni ya mwaka huu ilivyo batili, tena ubatili wote wa kimantiki na kisheria
Hivyo hamna namna isipokuwa mawakala wa vyama vyote watapewa fomu za matokeo ya uchaguzi pale kituoni kama miaka yote.
Fahamu, jadili, sambaza uelewa.