Hebu nipeni ukweli wa hii mimba

manSniper

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2015
Posts
814
Reaction score
680
Naombeni ushauri wa hili linamsibu kaka yangu kipenzi.

Ameishi na mwanamke 4 years na yeye alikua na mtoto wa nje na huyu binti pia alikua na mtoto. Alimkuta huyu binti anatumia sindano za uzazi wa mpango alimsihi aache na akaacha.Wameshiriki tendo la ndoa miaka yote hawakupata mtoto.

Alimpeleka hospital akaangaliwa akasafishwa na kupewa matibabu ila aliendelea bila kufanikiwa. Mwaka huu mwanamke alifiwa na babu yake akaenda kwao kakaa miezi miwili, alimpigia kuwa amepata mtaalam anampa dawa za uzazi za kienyeji pia akaenda kwa docta akapewa dawa za kuvuta mayai baada ya kamaliza period.

Sasa alirudi kama mwezi umeisha juzi tumbo likawa linamsumbua kwenda kupima anasema ana mimba. Sasa jamaa anakuwa na wasiwasi juu ya hii mimba anaomba ushauri.

Hii mimba itakua kaja nayo au? Afuate njia gani kuamini kama huu ujauzito ni wake? Ushauri yupo hapa nitampa mrejesho.
 
Tokd arudi kakaa muda gani na mimba ina muda gani?!
 
Mimba ina umri gani, na tangu arudi ana muda gani?
 
Hivi ukipima ujauzito unaweza kujua umri wake? Jibu please
 
Subiri tu mtoto azaliwa apime dna. Kama hana hela afanye dna ya kienyeji!

Katoto kakilala akapige dushe kichwani kama si kake lazima kafe!

Mmmh mganga kaishafanya yake. Anasema hivi " hii dawa inabidi uwekewe kwenye papuchi na mwanaume ambae hujawahi kulala nae"

sasa si mganga nae ni mwanaume? Anaamua amuwekee yeye ili dawa aiweke vizuri. Chezea mganga wewe!
 
Watoto ni mpango wa Mungu. Ukilazimisha sana kuwapata utasaidiwa kuwapata.

Mwambie kaka yako mimi babu yenu nimesema hivyo eti.

Ila kama hili jambo linakuhusu wewe (babu sioni mantiki ya kaka aliyekuzidi umri aje akuletee hii siri ya maisha yake ya unyumba wewe dogo ambaye pia hujui cha kumshauri mpk ukaleta huku).... basi usirudie tena. Utalea wana si wako. Shauri zako
 
Hivi ukipima ujauzito unaweza kujua umri wake? Jibu please
hapo ndipo panamchanganya hv ukipima mimba hospital unaeza jua kabisa ni ya wiki ngp? miez mingp? hv vipimo vinatoka uhalisia
 
Babu shikamoo

Kwahiyo hata kama tukisingiziwa tulee tu?!
 
Babu shikamoo

Kwahiyo hata kama tukisingiziwa tulee tu?!
Swala si kusingiziwa. Swala ni kwanini usingiziwe.... unapopress sana kupata mtoto.... na mkeo akajua. Atatafuta njia yoyote ule akutimizie haja yako. Ndo hapo sasa mtakapoanza kulea watoto wa wenzenu mkidhani ni wenu.

Mpende mkeo, watoto ni majaliwa ya Mungu.
 
Asante babu
 
Hili nalo Neno!! Shikamoo😳
 
Ndio unaweza; Shida yetu kubwa bongo ni watalaamu wa kusoma hizo ultra sound - inatoaga mpaka makadirio ya uzito wa mtoto!
kwa iyo inatoa makadirio na siyo uhakika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…