Hebu nishaurini ktk hili jamani

TAITUZA

Member
Joined
May 2, 2011
Posts
94
Reaction score
34
Jamani mimi ni kijana, bado sijaoa ila niko ktk mchakato wa kumtafuta mke,wiki iliyopita jioni nilikuwa natembea natokea kazini narudi nyumbani,ikatokea tukapishana na dada mmoja, baada ya kama hatua tano tu toka tupishane likanijia tu wazo la kugeuka nyuma. Sikuwa na nia ya kumuangalia yeye bali ilitokea tu, kwa kuwa kwa wakati huo nilikuwa na mawazo mengi ya kazini. Cha ajabu nilipogeuka tu macho yakakutana akatabasamu, nikapuuzia nikageuka mbele nikatembea kama hatua saba hv, nilipogeuka tena naye akawa alishageuka kunitazama, tukajikuta wote tunatabasamu. Nikapuuzia tena, baada ya kutembea tena kama hatua kumi zaidi, nikageuka tena safari hii mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza yeye akafuatia, tukajikuta wote tumesimama, tunatabasamu wote tena. Hatukuongea chochote kila mtu akaendelea na safari yake,na kwakuwa mimi nilishafika kwenye kona hatukuweza kuonana tena. Toka siku hiyo sura ya huyo binti huwa inanijia na kujikuta natabasammu peke yangu, kwa upande wangu najihisi nimempenda. Swali langu ni hivi kuangaliana kwa aina hii humaanisha wote tumependana?
 

Mara ya pili na tatu mbona hukusema kama na kugeuka huko kulitokea tu laaaaaaa!

Mmetamaniana na sio KUPENDANA. Kupenda ni zao la kutamani kwanza.....

Unataka ushauri wa nini na huenda hamtaonana tena? Maana hujasema kama anakaa kitaani kwako.........
 
Du! we can't tell that for sure, so I'd say the answer is Maybe! Ila from all the turning she did, there seems to be a possibility that she was attracted to you but again, thats only speculation!......................................! Na wewe since you had a chance to find out the real deal, why did you blow it???
 
Sijui anapoishi,ila huenda tukaonana cku yeyote,c unajua milima haikutani/
mabinti changieni hapa jamani
 
mmmh,au nikuwa mimi jamani?{natania}some times inatokea,kuna attraction fulani,ila kama hamtoonana tena,inakuwa imetoka hiyo.lakini kama mkionana tena kwa mara ya 2 hapo hamtotabasamu tena ila mtapenda mjuane zaidi
 
Kaka, Mambo haya hutokea!, hio inaitwa (Chemistry), yaani hisia zenu ziliumana kama magnet hivi.

Chukulia rahisi, kama ilikuwa Riziki yako, utampata tena kama hukumpata tena......AWEZAKUWA ALIKUWA JINI!!!!!!!
 
Mlitamaniana tu. Mpotezee kama hakuna uwezekano wa kuonana tena. Ila kama ni riziki yako kuna siku mtakutana. Usijijazie mawazo kwa mambo ya kubahatisha.
 

You blew it!!
Ulitakiwa usimame na umtokee, sasa wewe umepuuza hilo. Unaweza kumwona tena au unaweza usijemwona tena. You blew that chance, mkuu!! Move on
 
Shukuru kwa kutomtokea.... jini alikuwa anataka kukuteka!!!
 
Cku zote striker wa ukweli huwa harembi kwenye kumi na nane sasa ww umeremba halafu unataka usaidiweje?
Mfano umeona fuko la hela limedodoshwa je utakaa ukilikodolea macho mpaka uambiwe okota?
Sometimes kaka unatakiwa kuwa na maamuzi ya haraka hatakama unajaribu kiutani vile.
 
Inawezekana Ulikutana na Jini linalokunyemelea
 

ndugu jini mahaba hilo na kutoka mpaka ufunge na kukesha kwa maombi litakutokea mpaka umrudie mungu mbaya lilitaman likakupenda kweli!1watchout sio wote wanaotembea ni binadamu kwa upendo nenda makanisa a kiroho mwisho wa siku litakuwa linafanya na wewe mapenzi na mbaya ujui wapi maana kuna ya kila sehemu ni ukikuta mwanaume loh@@uchelwi vidole juu mtoto wa mwenzetu bila haya kila ukisikia wimo wajua taarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…