Jamani mimi ni kijana, bado sijaoa ila niko ktk mchakato wa kumtafuta mke,wiki iliyopita jioni nilikuwa natembea natokea kazini narudi nyumbani,ikatokea tukapishana na dada mmoja, baada ya kama hatua tano tu toka tupishane likanijia tu wazo la kugeuka nyuma. Sikuwa na nia ya kumuangalia yeye bali ilitokea tu, kwa kuwa kwa wakati huo nilikuwa na mawazo mengi ya kazini. Cha ajabu nilipogeuka tu macho yakakutana akatabasamu, nikapuuzia nikageuka mbele nikatembea kama hatua saba hv, nilipogeuka tena naye akawa alishageuka kunitazama, tukajikuta wote tunatabasamu. Nikapuuzia tena, baada ya kutembea tena kama hatua kumi zaidi, nikageuka tena safari hii mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza yeye akafuatia, tukajikuta wote tumesimama, tunatabasamu wote tena. Hatukuongea chochote kila mtu akaendelea na safari yake,na kwakuwa mimi nilishafika kwenye kona hatukuweza kuonana tena. Toka siku hiyo sura ya huyo binti huwa inanijia na kujikuta natabasammu peke yangu, kwa upande wangu najihisi nimempenda. Swali langu ni hivi kuangaliana kwa aina hii humaanisha wote tumependana?