Hebu njooni tujadili hili kutoka Simba SC

Hebu njooni tujadili hili kutoka Simba SC

Huo ni uzwazwa mahabiki wa Mbumbumbu fc wanajaa uwanjani sababu timu yao ni nzuri wana uhakika wa kupata positive results kuliko negative, kusema huyo chotara ndy anawahamasisha ni uongo,mbona amekuwa msemaji wa Mbumbumbu muda mrefu hakukuwa na kuujaza uwanja?? Baada ya kuolewa na MO ndipo mashabiki wamepata hamasa ya kuingia uwanjani acha porojo
Manara anaingiza mapato na ni lazima ahamasishe.
Hivi jinsi nyinyi mlivyoingia kwa uchache vile bila Manara Pesa ingepatikanaje hapo.
Manara anaujaza uwanja kalibu kila mechi.
Hii ndio kazi yake, kama kushinda gemu shindeni nyie basi.
Watu uwanjani mnaingia chini ya sehemu ya ⅛ ya uwanja halafu mnambeza Manara.
Hivi ile nyomi ya Simba mnaichukulia vipi, inatoka hewani au.
Hongereni na Sare yenu.



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tajiri Mo mpaka Sasa hajapost chochote mpk Sasa kuhusu mechi ile ya tarehe 4! Kapigwa ganzi [emoji2][emoji2],,

Yaani inaonekana wachezaji wa Simba wanasimangwa eti kwakuwa Wanalipwa vzr na Yanga Wanalipwa vibaya! Hayo masimango yenu yatasababisha wachezaji muwahamishe kisaikolojia! .. na mfano wa hilo ni pale Yanga walipopata goli moja,, wachezaji walipagawa na kutoka kweny game,, wakapigwa la Pili yaan ndio wakachanganyikiwa zaidi [emoji1787],! Yaani wanaogopa "tutamwambia nn Tajiri Mo"..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kosa alilofanya mzamiru huwezi kutegemea makosa hayo yanafanywa na wachezaji wa timu ndogo ukija simba umekamilika na shabalala anashindwaje kumzuia mo banka mpaka analeta madhara Manula analaumiwa bure kwa sababu alikuwa mtu wa mwisho
 
HAJI MANARA ACHA KUVUKA MIPAKA, UMEWAKOSEA SANA WACHEZAJI WA SIMBA.

Na Kulingwe Msafiri
Mwanachama Simba
Matalawe Njombe

Moja kati ya mambo ambayo hunipa furaha sana katika maisha ya ulimwengu huu pamoja na changamoto zote za dunia ni Ushindi wa Simba na Arsenal.Nazipenda timu zote ila Simba naipenda zaidi.

Ni ukweli usiopingika kwamba Timu yetu ya Simba ni kati ya vilabu bora sana katika Afrika ,kwa miaka ya hivi karibuni baada ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Mohamed Dewji klabu ya Simba imekuwa katika ubora wa kuanzia nje ya uwanja mpaka ndani ya Uwanja.

Kwa aina ya wachezaji waliopo Klabu ya Simba,ni dhahiri shahiri kwamba kila mpenzi na mshabiki wa Simba anategemea matokeo mazuri kwa kila mechi.Ila Simba hii inatupa kitu cha ziada ambacho ni Burudani ya Soka ambalo ni kama la Playstation,hii hasa inatokana na kikosi kukaa muda mrefu na kuelewana.

Wasiwasi wangu ni kuanza kujiaminisha kwamba Timu yetu hii itabaki katika kiwango kile kile kwa mechi zote na kwamba hatustahili droo wala kufungwa.

Wasiwasi zaidi unaongezeka nikiona mtu kama Haji Manara ambaye kimsingi yeye ni Msemaji tu wa Timu anakwenda mbali zaidi kutoa lawama katika mambo ambayo muda mwingine ni ya kiufundi,na hata kama alitaka kutuma huo ujumbe zipo njia sahihi za kufanya hivyo kwasababu na yeye ni sehemu ya Menejimenti badala ya kuandika ujumbe ule kwa umma hali ambayo inaweza kuwaathiri sana kisaikolojia wachezaji wetu ambao tumeshawajengea confidence kubwa kupitia mashabiki.

Manara anapaswa kutambua majukumu yake,haya mengine awaachie wahusika.Kazi ya Msemaji ni kusema baada ya jambo kuchakatwa ili lije kwa matumizi ya Umma.

Manara anajisahau kana kwamba hii ni Timu binafsi na yeye ndio mwenye kuamua cha kusema bila kuangalia athari ya maneno yake katika umoja na mshikamano wa Timu kwa muda huu.Kusema kuna wachezaji hawana sifa kuichezea Simba ni kuikosea pia Kamati nzima iliyofanya scouting ya wachezaji.

Kwa mechi kama ya jana hakuna mchezaji wa kulaumiwa,tumepata matokeo kama sehemu ya mchezo.Tuliwatawala Yanga kipindi cha kwanza,wakarudi na mbinu mpya ambayo ni kuzidiana kwa mbinu za kimchezo.

Goli la Mapinduzi Balama hata ungemleta De Gea na kipa yoyote unayemjua angefungwa tu.Ni goli la kiufundi ambalo hata sisi mashabiki wa Simba tulibaki mdomo wazi.

Aishi huyu huyu ametuokoa sana Ligi ya Mabingwa kwenye kuepuka vipigo vya aibu,leo hatuoni thamani yake na kumlaumu kwa mechi moja?

Ifike wakatai sasa CEO wa Simba achore mstari wa majukumu kila mtu asimame upande wake vinginevyo tutavurugana wenyewe kwa wenyewe wakati bado tuna safari ndefu.

Manara Simba niyetu sote punguza Mdomo kws kutafuta HURUMA na Kujihami kwa Porojo zako za Kibinafsi. Simba ni yetu sote uwe na shukurani.



Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu jamaa wa njombe mwehu, eti hata ungemleta de gea angefungwa sasa de gea nae ni wa kumpeleka sehemu kweli? Au hajaangalia mpira kipindi kirefu kidogo. Aishi na bi gea ni mapacha
 
Back
Top Bottom