[quote="Miss Judith, post: 1508021"]mpendwa chapa nalo jr, nashukuru kwa kunielewa. imeandikwa kuwa mwenye haki wangu ataishi kwa imani, so kwa kuwa umekiri kuwa nawe ni mkristo, nakusihi uendelee kuishi kwa imani.
kumtegemea Mungu sio kuipeleka akili yako likizo. kumbuka hata akili yako ni kipawa cha Mungu. tatizo watu hudhani kwamba wakiwa waangalifu sana na vigezo ndo watapata wenzi wa maisha wazuri na wanaomatch nao. lakini hekima ya Mungu si sawa na ya kibinadamu. Mungu aliweza kuyafanya hata mawe yaliyokataliwa na waashi kuwa mawe makuu ya pembeni. kumsubiri Mungu akupe mchumba siyo kufunga macho yako na kungoja uguswe bega kuwa uyu hapa mchumba, hapana. nami naishi katika jamii yangu na nasafiri mara kadhaa kwa mwaka nje ya nchi na napata fursa za kukutana na watu wa jamii mbalimbali. kote huko naweza kupata mwenza wa maisha. muhimu niwe seheme ya jamiii na nichangamane nao huku nikijiweka wazi haiba na tabia yangu yangu bila kificho. hekima ya Mungu ndiyo itakayoniongoza kufanya uamuzi siku hiyo ikifika. kumbuka nimesema kuwa nikiangalia pande zote naona maelfu ya wachumba wazuri walio tayari na huo si uongo, hivyo ashukuriwe Mungu anayetustahilisha haya yote na siye twapaswa kusema amina siku na saa ikifika.
sualal kuwa kila ndoa ina matatizo sio jambo la kuogopa. hata nje ya ndoa nako kuna matatizo, muhimu ujue msaada wako watoka wapi wakati wa matatizo, ukitegemea dunia ndio ikupe msaada, utaangamia vilivile na maarifa yako hayo. jiulize ndoa ngapi zimevurugika na maarifa yaliyopatikana mfano katika ulingo wa beijing? maazimio ya beijing si mabaya, bali kuyafuata bila kumpa Mungu nafasi yake. hapa jamvini watu wanaongelea mambo ya magari, pesa, kazi nzuri, elimu, umbo la mwili, sura, umri nk kama vigezo, wamesahau kuwa hayo ni mambo ya kupita tu, na ukitumia akili peke yake wawezza kutumbukia humo na mwisho ndoa yenye majuto kwani aliyechaguliwa kwa hivyo vigezo naye hutegemea hivyo vigezo viongoze ndoa yake na mwisho vigezo hivyohivyo vitageuka kero na hata kukuvunjia hiyo ndoa yako. tafakari hapo ndugu yangu