Hawa ni wanandoa wawili vijana wanaoishi pamoja though hawana mtoto,bwana ni konda kwenye magari makubwa na bibi ni mama wa nyumbani tuu.Sasa soma kidogo moja ya maongezi yao asubuhi moja;
Bibi: naomba hela ya matumizi ya leo,kila kitu kimeisha ndani.
Bwana:mimi sina hela
Bibi:sasa kama huna hela unadhani mimi nitakula nini leo na wewe ukienda kazini unakula hukohuko?
Bwana:nishakwambia sina hela,kama unaona mimi huwa nakula kazini twende na wewe ukale huko kazini.
Bibi:lakini jana umekuja umelewa,sasa kama huna hela hiyo ya kunywea umepata wapi?
Bwana:we mwanamke acha kunisumbua,nitakuchenjia sasa hivi ohooo
Bibi:mi bora unichenjie lakini lazima uniachie hela ya matumizi.
Bwana:we mshenzi kweli,unajua hela inavyotafutwa,SI UENDE UKATO*** HIYO K***A YAKO ILI UPATE HELA YA KULA.
Bibi:anakuwa mpole huku machozi yanamtoka.
Baada ya mume kuondoka kwenda kazini,bibi huku nyuma kweli na yeye akajiremba safari huyo kutafuta pesa kwa njia aliyoambiwa na mumewe.
MY TAKE:
Hivi ndivyo maisha ya ndoa yalivyo jamani?kama watu hamko tayari kuoa kwann uharakie?na kama umemchoka mwenzakao si umuambie ukweli tuu kuliko vituko na dharau zote hizi kwa mwenzio.