Hebu taja hapa zile furaha ndogo ndogo ambazo hazitoshi kumwambia mtu ila huwa unajisikia raha

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Hivi huo msemo kumbe umetoka hapa!![emoji1][emoji1][emoji1]
 
Another feeling ni chuo, mwalimu mnoko anataka mfanye presentation siku hiyo hiyo ya ijumaa na anatabia ya kuchagua random bila kwenda kwa mtiririko wa namba.

Group lako hamjafanya kazi sababu ninyi ni group namba 12 na magroup yapo 15. Anaanza kwa kutaja group namba 8, then namba 2,then 11, then group namba 5 then wakati group namba tano linakaribia kumalizia anawaambia ataishia hapo kwa siku hiyo. Mtaonana ijumaa ijayo....

Ukizingatia ni ijumaa na vipindi huwa ni vitatu tu.... Then ticha wa kipindi kinachofuata anatuma ujumbe kuwa hata fika mtaonana wiki ijayo....

Dah... Aisee nilikuwa napitia kabisa kwa mshikaji kuchukua movies naenda room, nalala, kisha nikiamka naanza kutazama
 

Mbona unazunguuukaaa utasema umepata bikira, hapo ni zamu yako na umepatikana baada ya binti kukwama machaguo yake karudisha majeshi kwenye other alternatives.

Mwenyewe anakushangaa unavyofuata procedure rasmi unamchelewesha tu!
 
Hivi huo msemo kumbe umetoka hapa!![emoji1][emoji1][emoji1]
Sidhani ila nachojua tundu la sindano ni dogo Sana ndio maana ikawekwa kwenye huo msemo yani chansi ya wewe kujikomboa ilikuwa ni ndogo kama tundu la sindano na hiyohiyo ndo chansi ndogo ndo imekuokoa..😜
 

Badala uandae kazi unajisemea Ijumaa mbali kote huko, ghafla alhamisi hii hapa!! [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nimecheka bila kujali kuna mteja anasubiri huduma au laah,sijavunga walai...

nimecheka sanaaaa maana ndio zangu hizo,enzi hizo yni nakaaga kichokozi chokozi,Kupgana siwezi...
 
Kuna ile unatumwa nyama Buchani,Baby Pitia buchani uje na nyama nzurii

ukiwa unarudi unapitia buchani unampga muuza bucha biti zote anakukatia nyama

ukipeleka home unakabdhi wakat inakaguliwa unasikia "nyama ya leo nzuri kweli",basi

kuna kafuraha flan kanakujaga kimoyo moyo yani unajiona wewe ndio Fazaaaa sasa...
 
Nimecheka bila kujali kuna mteja anasubiri huduma au laah,sijavunga walai...

nimecheka sanaaaa maana ndio zangu hizo,enzi hizo yni nakaaga kichokozi chokozi,Kupgana siwezi...
Ngoja huyo mteja akugeuzie kibano aanze nawe ye anajua unamcheka..😜
 
Uko zako kazini simu inaita unaambiwa "nyumbani huku TV hata haiwaki mwanao kaharibu"

unawauliza wamefanyaje wanakupa maelezo wee ila huwaelewi,unawambia ngojeni nikirudi

ukirudi unaenda kukuta ni zile nyaya za AV wamechomoa wamechanganya changanya pcha haitoki

basi unachomoa nyaya unachomeka vzr halafu TV inaanza onyesha,unamsikia mwanao akienda ita kina dada

Dada Dada Dada daddiii katengeneza,Daddie wangu ni fundiiiii Njoo tuangalie "mama cocooo",Bhasi BABA

unaamka hapo unatembea unadunda unaenda zako chumbani na tabasamu huku na kule,Chumbani unakutana

na maza mjengo Anakusimulia walivyohangaika,basi na wewe unajitutumua kiume unamwambia "siku nyingine mkiharibu siwatengenezei" 😛
 
Namimi ilinitokeaga hiyo,nilimlenga jiwe jamaaa akasimamisha baiskeli akaanza nitoa mbio,kimbia kimbia

mbele kule jamaa nlimwacha distance kbsa,akatokea mzee mmoja kiherehere akanidaka,akawa ananiambia

mbona unamkimbia kaka ako? nikamwambia yule sio kaka angu anataka kunipga,akasema hawezi kukupga bwana

basi jamaa akafika mzee akasimuliwa kdg na jamaa kisha mzee akamwambia Haya mtu wko huyo hapo,Akanikabdhi

kwa yule jamaa,asee nilikula mbata hizo sema ktk purukushani nilibahatka kumng'ata akaniachia Nikatoa ndukiiii....
 
Shule zetu za boarding huwa kuna ile mnaenda kuchukua chakula,....

sasa kuna siku chakula kinakuaga kimepkwa kingi sana,basi ikitokea hivyo....

huwa prefect/mwalimu wa zamu anachagua darasa la kurudia "second",enzi hizo nipo form 1...

,chakula hadi form six washachukua Unaskia prefect anatangaza "Form 1 Secoooooond"...

mzeee tunatoka nduki huko na furaha ya ajabu kufata kipunje..Second ilikua tamu bana....

halafu utamu wa second hunoga kama kesho yake unajua kbsa shule wali haupikwi,mchana ugali usiku kande...

wazee wa second huwa wali wetu ndio tunapetea kesho,sasa ile wakati nyie mnakula wali wengine Ugali au kande bwanaweee kuna kafuraha flani unajiona unakula kitu Hamna mtu ana mudu kpata...
 
Unapika pilau lako kwenye jiko la gesi,ushaweka mchele maji ya moto

umefunikia ufanye mambo mengine,hata dk 5 haziishi unaskia gesi imelia "paa"

kuchungulia kitu kimezima yani gesi imeisha,saa iyo usiku saa 4 inaenda 5 hv

unarudi unawaza ufanyeje,mara ghafla paap Unakumbuka kwenye fridge kuna

kiporo ulikisahau,aaah unaamka unaenda unatoa poro lako unadumbukza kwenye microwave

yani wakati unakula,unajikubali kbsa wewe ni Fazaaa "mke wa nini sasa" kama i can solve my own problems...
 
CONTROLA
Umenikumbusha misosi ya boarding ile scramble for, basi mnapanga vyombo vyenu mezani kisha mnakaa pembeni kuna watu wanapakua.

Ile mnarudi kuchukua unakuta sahani yako ina chakula cha kutosha huku wengine hamna hamna, basi ile furaha yake sio ya nchi hii!! [emoji39]
 
Mgombea unaonga wajumbe Mia moja, ili wakupigie kura then unapata kura tatu na kila mjumbe anakuambia kwenye kura tatu nami nilipiga ...
Na unabaki unajiuliza katika watu 100 ni watatu gani hao walionipigia apo ndo unaanza sasa kupiga hesabu kama za mwana hisabati🤣🤪🤦🏃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…