Hebu taja hapa zile furaha ndogo ndogo ambazo hazitoshi kumwambia mtu ila huwa unajisikia raha

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Wajumbe, ni Kazi Tu au Kazi na Bata!

Haya maisha bhana fanya yote ila hakikisha unafurahia, viwango vya furaha vinatofautiana kutoka ndogo hadi zile kubwa ambazo hadi watu wengine watajionea.

Basi kwa kutambua tofauti hizo, sio vizuri kuipuuza furaha ndogo kwa kutarajia kubwa isiyo na uhakika. Unaweza kungoja milele, na hivyo utaishi bila furaha kwa sababu tu ya tamaa na mapuuza.

Nitaanza kwa mifano michache, kisha nawe utashea za kwako:

1. Umekwangua vocha ukafuta namba kadhaa, ila ukafanikiwa kubuni namba kitu ikasoma... ile feeling niaje! Enhee hiyo hiyo.

2. Ile muda umegombea daladala na ukabahatika kupata siti, unafeel aje! Tena unajikausha kama sio wewe, furahia.

3. Upo kwenye mdahalo halafu hujui kitu imeulizwa, unaona mwezeshaji ananyoosha mkono kukuelekea... ghafla jirani yako anainuka kujibu.

4. .......

5. ........

Tuendelee!

Miscellaneous happiness!!
 
Kuna zile chafya sumbufu inakuja inakata inakuja inakata tena unakuta mtu hadi uwa anaganda kuipokea..😂
Ikishakupigisha zoezi hilo zaidi ya mara tano ndo inakuja sasa ukishaipiga mpk unahisi umeshinda..😅
 
Vile mtu hapendi fanya usafi chooni alafu amebanwa na tumbo la kuhara anakuomba umpishe aingie unajifanya Kama hujamsikia..ukishai gia toilet Kuna katabasamu fulani hivi kanakuja ka kumkomesha😂😂
 
Usiombe ukawa unapigana halafu kipigo kikawa kimelalia kwako then watu badala waamue ndo unasikia Kobe fulani huko inasema "Waacheni wafundishane adabu"😂
Sasa unajiuliza tufundishane adabu wakati ukijiangalia wewe jicho limeshaumuliwa halafu adui yako ndo kwanza anatoka jasho tu na kakutia kabari inaitwa "bwana wa mabwana Alfa na Omega"😂

Bahati nzuri situation kama hizo ndo wanatokeaga na wasalamia wema hapo ndo unajua kumbe malaika bado wapo duniani.. kwa ubavu nawe unajidai kuparangana ili kuuwa soo..😜
 
Vile mpo kituoni hupaelewi vizuri unapoenda unamuuliza sistaduu wa pembeni yako kiustaarabu kabisa mabasi fulani yanapaki wapi alafu anajikuta hakusikii au anajibu kwa nyodo😂😂..mwisho wa picha mnapanda bus moja konda anataka nauli sistaduu kaibiwa zamani Sana..alafu anakutana na maneno ya konda..😂😂😂 Kuna katabasamu fulani hivi kanakuja hadi unatamani hata kucheka 🤣🤣🤣🤣
 
Wajumbe, ni Kazi Tu au Kazi na Bata!

Haya maisha bhana fanya yote ila hakikisha unafurahia, viwango vya furaha vinatofautiana kutoka ndogo hadi zile kubwa ambazo hadi watu wengine watajionea.

Basi kwa kutambua tofauti hizo, sio vizuri kuipuuza furaha ndogo kwa kutarajia kubwa isiyo na uhakika. Unaweza kungoja milele, na hivyo utaishi bila furaha kwa sababu tu ya tamaa na mapuuza.

Nitaanza kwa mifano michache, kisha nawe utashea za kwako:

1. Umekwangua vocha ukafuta namba kadhaa, ila ukafanikiwa kubuni namba kitu ikasoma... ile feeling niaje! Enhee hiyo hiyo.

2. Ile muda umegombea daladala na ukabahatika kupata siti, unafeel aje! Tena unajikausha kama sio wewe, furahia.

3. Upo kwenye mdahalo halafu hujui kitu imeulizwa, unaona mwezeshaji ananyoosha mkono kukuelekea... ghafla jirani yako anainuka kujibu.

4. .......

5. ........

Tuendelee!

Miscellaneous happiness!!
Unajizuia kujamba afu bahati mbaya ushuzi unakupokonyoka unawaza bharaa lake afu bahati nzuri ulikula vichips koo ushuzi hautoi harufu heavy
 
Usiombe ukawa unapigana halafu kipigo kikawa kimelalia kwako then watu badala waamue ndo unasikia Kobe fulani huko inasema "Waacheni wafundishane adabu"😂
Sasa unajiuliza tufundishane adabu wakati ukijiangalia wewe jicho limeshaumuliwa halafu adui yako ndo kwanza anatoka jasho tu na kakutia kabari inaitwa "bwana wa mabwana Alfa na Omega"😂

Bahati nzuri situation kama hizo ndo wanatokeaga na wasalamia wema hapo ndo unajua kumbe malaika bado wapo duniani.. kwa ubavu nawe unajidai kuparangana ili kuuwa soo..😜
Umenikumbusha mbali aiseh 🤣🤣
 
Pale umecheza kamech kako rough halafu ni danger zone, ile presha unapatana nayo kwa siku kadhaa huwa haielezeki, mara ghafla kuna namna unahisi hali flani ya tofauti kwenda kujichungulia unakuta wageni wamekuja.!! 😂

Ile feeling sisi hupata na maombi ya shukrani tunayosema huwa tunajua wenyewe.!!🥰
 
Back
Top Bottom