Hebu taja hapa zile furaha ndogo ndogo ambazo hazitoshi kumwambia mtu ila huwa unajisikia raha

Hebu taja hapa zile furaha ndogo ndogo ambazo hazitoshi kumwambia mtu ila huwa unajisikia raha

Au ile umewahi umeanika kamba imejaa halafu kumbe kuna mtu umemuwahi tu naye anafua, basi unajiona umepatia timing kinyama.
Mara ghafla kamba ikakatika..na hapo uani hakuna sakafu, ni muda tu umewafukuza watoto waliokuwa wanacheza mpira ili uanike nguo.
Unatamani iwe ni ndoto!
 
Mko na wana mnakata vyombo mfukoni una 30k unajua kabisa mmeshazidisha bill ila unaona poa tu ngoja mmwagilie roho, mangi atakuandika kwenye daftari, anatoka mtu huko anaifuta bili yote anawazungushia na tano tano kila mtu!! Mtu weweee[emoji23][emoji23]
 
kupata kitumbua kilichosumbua roho! muda mrefuu! mpaka kuishia kutukanwa, raha sana , halafu huwaga na utamu na sura ileile km ulivo wazaga kabla.
 
Pale umecheza kamech kako rough halafu ni danger zone, ile presha unapatana nayo kwa siku kadhaa huwa haielezeki, mara ghafla kuna namna unahisi hali flani ya tofauti kwenda kujichungulia unakuta wageni wamekuja.!! 😂

Ile feeling sisi hupata na maombi ya shukrani tunayosema huwa tunajua wenyewe.!!🥰
Kwamba mimba ni issue tatizi? Naanza kuamini abortion ni hatari kuliko Ukimwi siku hizi
 
Kuna demu/mtu hujamtafuta siku nyingi, siku anakutumia ujumbe unawaza lazima ataanza kulaumu tu.

Mara anasema alipoteza simu muda mrefu, na anakuomba radhi anajua ulimtafuta sana! [emoji4][emoji2957]
 
Umetoa sadaka pesa yako ya mwisho kabisa, mara paah baada ya ibada unaona 140,000/= kesho kuna kikao cha wafanyakazi wote kwa siku mbili na nauli pia.
 
Wajumbe, ni Kazi Tu au Kazi na Bata!

Haya maisha bhana fanya yote ila hakikisha unafurahia, viwango vya furaha vinatofautiana kutoka ndogo hadi zile kubwa ambazo hadi watu wengine watajionea.

Basi kwa kutambua tofauti hizo, sio vizuri kuipuuza furaha ndogo kwa kutarajia kubwa isiyo na uhakika. Unaweza kungoja milele, na hivyo utaishi bila furaha kwa sababu tu ya tamaa na mapuuza.

Nitaanza kwa mifano michache, kisha nawe utashea za kwako:

1. Umekwangua vocha ukafuta namba kadhaa, ila ukafanikiwa kubuni namba kitu ikasoma... ile feeling niaje! Enhee hiyo hiyo.

2. Ile muda umegombea daladala na ukabahatika kupata siti, unafeel aje! Tena unajikausha kama sio wewe, furahia.

3. Upo kwenye mdahalo halafu hujui kitu imeulizwa, unaona mwezeshaji ananyoosha mkono kukuelekea... ghafla jirani yako anainuka kujibu.

4. .......

5. ........

Tuendelee!

Miscellaneous happiness!!
Kuna kale kaugonjwa kale koo limawasha lakin ukitaka kuyema kohoz alitoka sasa inatokea bahat unakohoa gafla tu unashangaa kohoz limenasa afu ili hali ya koo kuwasha inapungua basi unajiona mjanja furaha kibao
 
Kuna kale kaugonjwa kale koo limawasha lakin ukitaka kuyema kohoz alitoka sasa inatokea bahat unakohoa gafla tu unashangaa kohoz limenasa afu ili hali ya koo kuwasha inapungua basi unajiona mjanja furaha kibao

[emoji1][emoji3][emoji23][emoji1487]
 
Ile unatazama movie yako halafu ghafla TV/PC imezima, kuja kuwasha ina-resume pale pale iliishia![emoji4][emoji4][emoji4]
 
Vile una arosto umekaa unatia huruma hujaboost unazunguka mitaa ya bar! unashangaa mwamba mmoja "anakwambia aisee embu agiza na ww tuko pamoja" ile feeling kabla kinywaji hujakishusha udenda ushajaa mdomoni.

#Viva Team Walevi
 
Ni pale naposubiria kwa hamu Mchuchu kutelemsha ka kufuri ka-moyo kangu, kanaenda mbio kwa furaha zote, km ananichelewesha vile, huwaga wanaweka mikono kiunoni hivi..... picha tafadhali!
 
Umeme ukikatika ghafla wakati wa Prep hasa maisha ya sec. roho swafiii tukose wote tukalale
 
Umeme umekatika kwako unahisi kama umeisha kwa kuwa zilibakia units chache na pesa hauna, unachungulia kwa jirani unaona giza pia! [emoji4][emoji4]
Na hapo ndipo unapojua kwenye msafara wa mamba na kenge wapo..😂
 
Binti niliyemtamani kwa muda mrefu kwa kumuona, ghafla naona account yake ya Instagram imekuwa suggested kwangu, namfollow ana accept, then namDM anarespond, najitambulisha naomba namba ananipatia bila hiyana.

Namualika kupata dinner ananikubalia, nakwenda mchukua tunakwenda kupata chakula, namrejesha then wakati wa kumuaga naomba kumhug ananihug kwa huba tofauti na matarijio..... Kisha namkiss kwenye shavu anatabasamu anaondoka.......

Siku inayofuata namwambia lile hug lilinimaliza i wish nipate tena, ananiambia its okay... Naenda this time hug inakuwa ndefu kidogo, but inaishia na Kiss......

The feeling is unexplainable
 
Ile upo hospitali umeshachojoa nguo mtako hadharani dokta anaminya sindano kutest inavyopitisha dawa ghafla anakuja nesi anamwambia dokta,"dokta samahani daktari mapunda kasema huyo atatumia dawa ya kumeza tu zimeshapatikana!!"
Hapo kijasho cha shukurani kinakutoka unafunika kitako chako komavu huku ukishukuru umeponea kwenye tundu la sindano..😜

Sasa usiombe ukutane na wale daktari wa kikoloni dawa iwe imepatikana au haijapatikana utachomwa ilimradi tu umeshaingia chumba Cha sindano haiwezekani uwe umeenda kutalii mule lazima sindano idungwe..😂
 
Back
Top Bottom