Hebu taja hapa zile furaha ndogo ndogo ambazo hazitoshi kumwambia mtu ila huwa unajisikia raha

Hebu taja hapa zile furaha ndogo ndogo ambazo hazitoshi kumwambia mtu ila huwa unajisikia raha

Mdada anaenipita sehemu kwa nyodo na dharau bila kusalimia kumbe sehemu anayo enda haijui then anarudi kuniulizia[emoji28][emoji28]hapo ndipo furaha huja sasa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1635][emoji1635]
Iliwahi tokea daaah yule mdada nilimjibu kwa wema tyuuuh. Afu hat hakuamin eti.
 
Vile mtu hapendi fanya usafi chooni alafu amebanwa na tumbo la kuhara anakuomba umpishe aingie unajifanya Kama hujamsikia..ukishai gia toilet Kuna katabasamu fulani hivi kanakuja ka kumkomesha[emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Vile mpo kituoni hupaelewi vizuri unapoenda unamuuliza sistaduu wa pembeni yako kiustaarabu kabisa mabasi fulani yanapaki wapi alafu anajikuta hakusikii au anajibu kwa nyodo[emoji23][emoji23]..mwisho wa picha mnapanda bus moja konda anataka nauli sistaduu kaibiwa zamani Sana..alafu anakutana na maneno ya konda..[emoji23][emoji23][emoji23] Kuna katabasamu fulani hivi kanakuja hadi unatamani hata kucheka [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Inaonekana ushakuapata huu mkasa..[emoji23] umeyajua yote hayo.. wengine hukata na tamaa wanaanza kusema "Niuwe tu"[emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaah
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2296][emoji2296][emoji2296][emoji2296][emoji2296][emoji2296][emoji2296]kama nakuona kudadeki

Nilimuwasha tukio haki tena nilimuacha anakohoa....nilimuachia vumbi[emoji28][emoji28]kufika mbele nikakutana ni kikosi kazi changu nikasnza kutembea kama boss[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sasa hivi ni ni watu na familia zao aise [emoji28][emoji28]
Kumbe wee nunda uwiiiiiiiih
 
Unaingia kwenye daladala limejaa balaa, konda anafoka tu sogea nyuma upande wa pili hapo... ile unaingia tu mtu kashuka unapata siti.[emoji4]

Hapo kuna watu wamesimama mwanzo mwisho.
 
Wajumbe, ni Kazi Tu au Kazi na Bata!

Haya maisha bhana fanya yote ila hakikisha unafurahia, viwango vya furaha vinatofautiana kutoka ndogo hadi zile kubwa ambazo hadi watu wengine watajionea.

Basi kwa kutambua tofauti hizo, sio vizuri kuipuuza furaha ndogo kwa kutarajia kubwa isiyo na uhakika. Unaweza kungoja milele, na hivyo utaishi bila furaha kwa sababu tu ya tamaa na mapuuza.

Nitaanza kwa mifano michache, kisha nawe utashea za kwako:

1. Umekwangua vocha ukafuta namba kadhaa, ila ukafanikiwa kubuni namba kitu ikasoma... ile feeling niaje! Enhee hiyo hiyo.

2. Ile muda umegombea daladala na ukabahatika kupata siti, unafeel aje! Tena unajikausha kama sio wewe, furahia.

3. Upo kwenye mdahalo halafu hujui kitu imeulizwa, unaona mwezeshaji ananyoosha mkono kukuelekea... ghafla jirani yako anainuka kujibu.

4. .......

5. ........

Tuendelee!

Miscellaneous happiness!!
Nikiona maccm yameshindwa uchaguzi huwa najihisi kuwa na furaha sana moyoni
 
Uwe huna pesa halafu ghafla unasoma message mpya ya "IMETHIBITISHWA" [emoji4]
Kuna siku mwanangu, niko safari na mgonjwa. Inanilazimu kulala mahali ndipo siku ya pili niendelee na safari mfukoni nina 30,000/=. Ninajaribu kuomba msaada kutumiwa hela kwa mpesa, mtandao unasumbua hela hazihami.

Nikakaa kwenye kiti cha wateja kwenye ofisi ya mpesa. Nimevurugwa. Hela niliyonayo hairuhusu hata kula kabisa. Inatosha tu chumba na nauli keaho yake.

Mara sms kwenye simu hiyo. Ninadhani huenda washikaji tu wametuma. Ninachukua simu kinyonge nione ni nani ametuma sms. Mara siamini, nasoma sms tena na tena. Ni kutoka NMB. Kiasi cha sh. 3m kimeingizwa kwenye akaunti yako inayoishia na......

Nikatoka nduki kwenda nyumba ya kulala wageni nikachukue kadi kwenye mkoba. Siamini kabisa. Nikarudi mbio hadi kwa wakala. Ninaagiza tu kutoa 2.8m. Nasikilizia mashine itasoma? Mara muhudumu ananipa risiti. Nacheka moyoni cheko kuu. Nahesabu pesa na kutimua mbio kurudi chumbani.

Nilicheka hadi mgonjwa anachanganyikiwa.

Maisha haya, we acha tu.
 
Unaamka asubuhi hauna mia, kwenye kufukua nguo chafu ghafla buku mbili au tano hii hapa uliisahau mfukoni! [emoji4][emoji4][emoji4]
Hii ilishawahi nitokeaga hata mimi, kuna siku nimefulia nakuja kutoa jeans yangu nivae nakuta elf 20 kumbe niliiweka bahati mbaya na mimi nilishazowea kuweka kwenye wallet.... Hiyo furaha yake haikua ndogo.
 
Unaenda kwenye msiba unakuta Aliyefariki ni kibogoyo ,tena unaskia mc anasema "hakika pengo lake katika jamii halizibiki😁😄😅
 
Pale umecheza kamech kako rough halafu ni danger zone, ile presha unapatana nayo kwa siku kadhaa huwa haielezeki, mara ghafla kuna namna unahisi hali flani ya tofauti kwenda kujichungulia unakuta wageni wamekuja.!! [emoji23]

Ile feeling sisi hupata na maombi ya shukrani tunayosema huwa tunajua wenyewe.!![emoji3059]
Hahaa daahh!!!
 
Back
Top Bottom