RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
📖Mhadhara (63)✍️
Nyumba za kupanga (hasa zile ambazo zina wapangaji wengi) zina kero mbalimbali. Hebu tiririka kero mojawapo kwenye nyumba za kupanga - Natiririsha baadhi ya kero.
🔘 KERO 1:
Kuna mpangaji ambaye akiingia bafuni kuoga, akitoka lazima bafuni mkute mabaki ya dawa za kienyeji. Kila siku anaoga madawa ya kienyeji lakini hana mabadiliko yoyote ya maisha.
🔘 KERO 2:
Kuna mpangaji (nyumba yenye choo na bafu la kuchangia) ambaye akiingia bafuni kuoga utamsahau, atakaa bafuni muda mrefu utafikiri amekwenda kufa.
🔘 KERO 3:
Kuna mpangaji ambaye akiwahi kuamka asubuhi kabla ya wenzake, anafungulia redio au mziki mkubwa (nyimbo za taarabu, au dini, au bongo fleva). Mara nyingi huwa wanahisi wenzao wanazipenda nyimbo wanazopenda wao.
🔘 KERO 4:
Kuna mpangaji ambaye akigundua mpangaji mwenzake (chumba cha jirani) ameingiza mwanamke/mwanaume, hata kama alikuwa anasikiliza mziki atapunguza sauti ili asikilize kinachoendelea kwenye chumba cha mwenzake. Au atatoa jamvi akae nje ili mgeni akitoka amuone.
🔘 KERO 5:
Kuna mpangaji ambaye akiamka asubuhi anaswaka mdomo kwa nguvu na kutema makohozi, nyumba nzima wanamsikiliza yeye.
🔘 KERO 6:
Kuna mpangaji mwenye tabia ya umalaya, yaani ni lazima atembee na mwanamke/mwanaume wa mpangaji mwenzake. Ni mzuri sana wa kuigiza nidhamu kwa mashemeji zake lakini hafai.
🔘 KERO 7:
Kuna mpangaji ambaye akiazima kifaa au kitu chochote kwa mwenzake (pasi, mbuzi, jiko, mwiko, kiberiti, sufuria, n.k) harudishi mpaka mwenye kitu chake akifuate.
🔘 KERO 8:
Kuna mpangaji akigundua Bill ya umeme au maji imetoka, au ni zamu yake kulipa umeme au maji, ataanza kuchelewa kurudi nyumbani, na huamka kimya kimya asubuhi sana kisha anaondoka.
✓ HEBU TIRIRIKA KERO NYINGINE
__________
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM