Uchaguzi 2020 Hebu tuambizane ukweli, Magufuli anatumia kigezo gani kusema atashinda Uchaguzi?

Uchaguzi 2020 Hebu tuambizane ukweli, Magufuli anatumia kigezo gani kusema atashinda Uchaguzi?

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,419
Mgombea urais wa CCM, Magufuli anadai kwenye kampeni kuwa atashinda Uchaguzi. Je, anatumia kigezo gani?

Kwenye mikutano yake ya kampeni anawaambia wananchi kuwa wamletee Diwani na Wabunge wa CCM eti yeye atashinda tu, Je, anatumia kigezo gani?

Anadiriki kuwaambia kuwa wasipochagua wabunge wa CCM hatawaletea maendeleo. Je, maendeleo yana vyama?

KWA UPANDE WA WATUMISHI; Akiwa huko Musoma alidiriki kusema kuwa hajamaliza muda wake wa uraisi hivyo atawaongezea mshahara watumishi kabla hajatoka madarakani, je anaongeza mwezi Oktoba? Ana uhakika gani kama atashinda Oktoba hii?

Kama hajamaliza muda wake, kwanini anapiga kampeni?
 
Kwani bado mnaamini mnatoboa hahaaa
Endeleeni na drama zenu,Magu ndio news!
Na mnajua vizuri hamshindi.
 
Kila mwenyekiti wa mtaa anapewa pesa kwa watu wa mtaa wake na wanalazimishwa kwenda kwenye mikutano kwa malipo ya 5,000 kwa kichwa. Usafiri unakuwepo, kablawhujaingia kwenye usafiri unapewa t-shirt na kofia.

muwape taarifa mapema wabebe hotpots za viazi vitamu na maji ya kunywa.
 
Mama yangu jana kala elfu 30 na bado kaniambia kura ni Kwa Lissu.
 
Anatuma kigezo alichosema katibu mkuu wa ccm.

Vyombo vya Dola.
 
Back
Top Bottom