Hebu tuangalie hoja hizi zilizotumika kupinga Uchunguzi wa Rais Magufuli Maabara kuu ya Taifa

Ni ya kuchukua sampuli katila fenesi ni nini?

Je ni kuonyesha kuwa hatuna co-vid nchini???
Yeye anajua kuwa ugonjwa upo na ulipo ingia nchini ni yeye ndie alitangaza na kuwaambia watu wachukue tahadhari, Sasa habari sijui za kuonyesha ugonjwa haupo hizo ni za kwako.

Lengo la kufanya huo uchunguzi ni kutaka kujiridhisha na utendaji kazi wa hivyo vifaa.
Na hilo sio kosa kwake kama mkuu wa nchi.
 
Kipindi kama hiki hutufunza mambo mengi tofauti hatayale tunayodhani si tatizo..tatizo la kwanza linaanzia kwenye timu inayomshauri Mh. Rais akiwemo huyo Prof. aliyekubali kutest covid vitu ambavyo havihusiani na kinachotakiwa kujulikana..je tatizo ni vifaa au umakini wa wapimaji..WALISHINDWA NINI KUSHAURI KWAMBA VIPIMO VICHUKULIWE KWA BINADAMU NA VIPEWE MAJINA TOFAUTI..MFANO SAMPULI ZA ALLY ZIPEWE MAJINA YA WATU 5 TOFAUTI KWA SAMPULI ZILE ZILE NK NA ZIKAPIMWE SEHEMU TOFAUTI, DAR, MZA NA ARUSHA IKIWEZEKANA PELEKA HATA NCHI JIRANI RAFIKI HALAFU LINGANISHA MATOKEO...kwa njia hiyo utakuwa kwenye nafasi nzr kufahamu dosari iko wapi..si hivyo walivyofanya, kama ni muungwana huyo prof. hata hiyo kazi alipaswa aache! huwezi kutoa ushauri dhaifu namna hii.
 
Na baada ya kuchukua sampuli.Nusu ingepelekwa maabara kuu na nyingine ipelekwe Kenya.Kisha tulibganishe majibu
 
Tumesha ambiwa kuwa wanyama kama paka na mbwa na wanyama wengine hapa Ulaya wamekutwa na coronavirus, kwa kuwa wanao wahudumia walikuwa tayari wamesha adhirika, je hizo sample zinazo tajwa hapo juu itakuwaje kama walio shughulikanazo tayari wana corona? Tangu corona ianze viongozi wengi wa kisiasa wametumia kila aina kuchukua uamuzi wa kukalia viti vya wanasayansi na kutoa maamuzi ya ugonjwa wa corona kwa kuhofia chaguzi zijazo, sababu nchi nyingi Duniani zinaingia kwenye uchaguzi siku chache zijazo.
 
Una lako jambo! Si bure, kama ni mkeo au mmeo arudishwe. Amechukuliwa tu. Khaah, si chuki hii! Hii sio hoja.
 
Hilo una uhakika nalo au unabahatisha?Mimi ninayo hapa mashine ya kupimia sukari,sampuli ni damu!Jana niliweka maji bado kikanipa reading,ina maana kuna glucose kwenye maji au kifaa ni kibovu?
Nilichogundua ni kuwa mimi ndio mjinga kuweka maji kwenye kifaa kinachopima glucose kwenye damu ya binadamu na sio kwamba kifaa ndio kibovu!
Hilo suala la visa kama hivyo lipo,ndio maana nasema tupeleke sampuli za binadamu kwa wingi kuangalia accuracy ya kifaa!Kama kina 96%,then katika watu 100 kitakosea kwa watu wa 4!So kuondoa hiyo error basi sampuli inatakiwa kupimwa walau mara 3 maana ni vigumu sana sampuli ile ile kuangukia kwenye error ya hiyo 4% kwa mara 3 mfululizo!
 
Hebu tofautisha wanasiasa na wataalam. Wanasiasa siku zote hutafuta kujijenga kisiasa tu. Kabla hujatoa hoja zako zilizokaa kishabiki ungefikiria kwanza.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, kama wameleta vipimo maalumu kwa ajili ya Corona, most likely atakuwa anazungumzia Test kits. Lakini tatizo la test kits mpaka sasa haziko well validated na ndiyo maana sehemu nyingi wamepata shida nazo na kuzikataa. Kwa idadi ya watu waliokuwa wanakuwa tested Tanzania kama walizitumia basi ilikuwa ni muhimu wafanye confirmation with WHO recommended tests.
 
Mkuu mbona tunachoshana bure, not present or not detected kwanini wakati sample sio sahihi au hili swali huliewi mkuu?? Sample sio sahihi kwenye kipimo sasa jibu kama hilo limekujaje??
Mkuu, nilikuwa najaribu kukuelewesha what it means when the test report says Negative.
 
Kama no hivo sasa kosa la Rais yeye kufanya uchunguzi ni lipi? Au wenye ruhusa ya kusema na kurudisha hivo vifaa ni hao tu wa mataifa mengine?
 
Hebu tofautisha wanasiasa na wataalam. Wanasiasa siku zote hutafuta kujijenga kisiasa tu. Kabla hujatoa hoja zako zilizokaa kishabiki ungefikiria kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni mwana sayansi au mwana siasa??
Kama wewe ni mwana sayansi basi jibu hizo hoja hapo kisayansi nikuelewe mkuu.
Mimi hapo nimeuliza kutokana na maelezo ya hao wanasayansi waliyoyaleta wakimkosoa Rais.
 
Wewe nae inabidi usome tena mada kule juu uelewe vizuri alafu uje tena mkuu.
 
What if there was a deliberate contamination to discredit our own labs??
Sasa kama kuna contamination kwenye maabara zetu, ndio nikauliza hamuoni hapo kuwa kuna uwezekano wa kuwapa watu majibu ya positive ilihali haumwi ila ni sample yake ndio ipo contaminated?
If that is true, nani anapaswa kuwajibika hapo ni wataalam wetu au Rais??
 
Mkuu unataka kunambia kuwa hawa wanasayansi maelezo waliyo yatoa kuhusiana na utendaji kazi wa hivi vifaa wametudanganya??
 
Kama no hivo sasa kosa la Rais yeye kufanya uchunguzi ni lipi? Au wenye ruhusa ya kusema na kurudisha hivo vifaa ni hao tu wa mataifa mengine?

Anyway, ngoja tusubiri tuchunguzi.
 
Wewe ndio una hoja dhaifu na si wao, kwasababu kwa mujibu wa wataalam wetu wamesema vifaa hivyo vinapima Corona na sio kitu kingine chochote, ukiweka sample tofauti kifaa hicho hakitasoma negative wala positive badala yake hakitaitambua hiyo sample yani itakuwa Unknown.

Sasa kama hilo ni kweli kwanini vilisoma positive ya papai na negative ya nanasi?

Sasa mnaanza tena kuja na sample za binadamu, we unavyodhani hao ni wajinga kiasi hicho kwamba hawajui hicho unachokisema hapo.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…