Uchaguzi 2020 Hebu tufanye kashinda Lissu, nini hatma ya haya mapesa ya walipa Kodi?

Uchaguzi 2020 Hebu tufanye kashinda Lissu, nini hatma ya haya mapesa ya walipa Kodi?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Kama tujuavyo serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli imeibua miradi mingi mikubwa ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji, hii ikimaanisha kwamba tayari hii miradi imeshatumia pesa nyingi sana za walipa Kodi ambapo mgombea huyu anatoa ahadi kwamba tukimchagua tena ataimalizia.

Kwa upande mwingine ni kwamba mgombea urais kupitia chadema ndugu Lisu amekua akiiponda miradi hii na kutilia shaka uhalisia wa gharama za utekelezaji wake ingawa hasemi akiingia madarakani ataifanyaje hii miradi ili kulinda fedha ya walipakodi isiharibike bure kama ilivyoharibiwa Ile fedha ya mchakato wa katiba mpya.

Kwa uchache hii ni baadhi ya miradi ambayo tungetamani kujua hatima ya fedha zetu chini ya utawala wa mh Tundu.

1. Stiegler's
2. SGR
3. Kuhamishia serikali Dodoma
4. Ununuzi wa ndege
5. Ujenzi wa uwanja wa ndege
6. Mabadiliko ya mikataba ya madini
7. Ujenzi wa flyovers Dar
8. Ujenzi wa madaraja kama vile Busisi, Salender
Nk.
 
Hiyo ya Stieglar Gorge Dam ni ya kuachana nayo kwa sababu za kuathiri ekolojia, hiyo SGR nayo ni ya kuachana nayo kwani reli ya wakoloni ya meter gauge inakidhi mahitaji ila haina tu service.

Mpango wa kuhamia Dodoma unaweza ukaendelea ila ndege ni ya kuachana nayo kwani hata Magufuli imemshinda na ndio maana kapiga marufuku CAG asiikague ATCL.

Ujenzi wa uwanja wa ndege kama ni Dodoma sawa ila isiwe Chato tena. Mabadiliko ya mikataba ya madini hamna kitu kumbe ilikuwa ni siasa tu na kutafuta kiki kumbe mambo yako vile vile.

Ujenzi wa flyovers Dar ni sawa ila zijengwe kwa mapato yatokanayo na makusanyo ya kodi za mkoa wa Dar es Salaam chini ya mfumo wa serikali mpya ya shirikisho (Federal Republic of Tanzania).

Ujenzi wa madaraja kama umeshaanza uendelee tu. That's the way I see it.
 
Hawezi akawa rais, hivyo hakuna haja ya kuota - ukiamua kuota basi sema na - Hashim Rungwe, Lipumba, na Membe. Ila wote hawapati.
 
CCM wana hali mbaya Sana. Kwahiyo mnatafuta huruma kupitia miradi ya hovyo hiyo ili wananchi wawapigie kura?

Magufuli kitakacho muqngusha uchaguzi huu ni ubabe, daharau na kupuuza vilio vya watu kuhusu ugumu wa maisha
 
Miradi yote ya JIWE si ya kumnufaisha mwananchi wa kawaida ,miradi hiyo ni white elephants,ni miradi ya jiwe kupiga pesa kupitia MAYANGA ,MECCO na kampuni zake nyingine zisizojulikana.

Kipindi midege ya ATCL haipo ,tulikuwa tuaenda mwanza kwa laki na nusu kwa fast jet ,alivyonunua midege hewa ,akaiua Fast Jet na sasa mwanza ni zaidi ya laki 5,sasa midege yake imesaidia nini?

Miradi yote ya JIWE ni ya UPIGAJI ,ukija kujua fedha alizopiga via hiyo miradi unaweza ukazimia.
 
Umesahau ile trilion 1.5 aliyoibua CAG.

Lissu amesema cha kwanza ni katiba, mimi nakwambia kwa moto wa LISSU jamaa atajenga kweli Tanzania mpya.
 
Back
Top Bottom