Hebu tujiulize undani wa hili ‘Tishio la UGAIDI’

Mkuu juzi tu tunaskia mzee kaua watu zaidi ya kumi huko US.
Ni kweli Tanzania tuko ovyo lakin taarifa za intelligence polisi, jw au tiss sio za kuweka public hata kama wanajua tena za ugaidi.
Kama wametangaza kwanini wasipambane kuzuia waje wakutangazie wewe kuna tishio?
US anachofanya ni kwa ajili ya raia wake hapa Ila sio kuisaidia tz
 
Wajuzi wa masuala ya usalama wakikusoma hapa hawatoondoa shaka yao kwamba vyombo vyetu vya dola vinawatumia raia kama ngao.

Elewa nilichoandika lakini
 
Marekani washaanza fitna zao. Na mambumbumbu wanalichukulia serious hili suala.
 
Wajuzi wa masuala ya usalama wakikusoma hapa hawatoondoa shaka yao kwamba vyombo vyetu vya dola vinawatumia raia kama ngao.

Elewa nilichoandika lakini
Hakuna ulicho andika...
Ujuaji tu mimi nimekaa na hao ma MI naelewa sana kuhusu haya mamb o ya ugaidi.
Lengo la ugaidi ni kutengeneza hofu, kui-sabotage serikali na kupata publicity unapotanganza kwa raia kunatishio umeshafanikisha lengo lao la kwanza hofu, kama umefuatilia huko marekani na ulaya wasomi wengi akiwemo prof Jordan Peterson wa chuo cha canada wanataka hizo taarifa za watu kuwashambulia watu wengine zisiwe zinatangazwa kwa sababu hyo ni moja ya motive ya hao watu.
Unless kama wewe ni mtu wa intelligence unajua zaidi
 

Izingatiwe security alert ya beberu imetolewa siku Lissu alipowasili, Chadema wakiwa wamepanga mfululizo wa mikutano ya hadhara pamoja naye.

Ikumbukwe wale waliowahi kusema kama risasi 16 hazikumwua, basi watamchoma sindano za sumu wangalipo.

Bwana Musiba na wenziwe waliokuwa wakiyasema hadharani kuhusu kumdhuru Lissu nao wangalipo.

Wasiojulikana na genge zima lililolukuwa area D siku Ile ya tukio nao wangalipo.

Nk, nk.

Inahitaji nini zaidi kufahamu wenye roho za kumwua mtu wanaweza kuwa watu wa namna gani? Kwamba ghafla wanaweza kuwa waliacha na kustaafu sasa?

Kwani ni lini walitubu, kuokoka au hata kuslimu ili kuutafuta wokovu wa mbinguni sasa?

Ikumbukwe mikutanoni Chadema wamewahi kushambuliwa kigaidi Arusha, bila kusahau risasi za moto kinondoni zilizoondoka na yule binti asiyekuwa na hatia.

Tishio lipo, Chadema wengine kutoimarisha ulinzi msilalie mlango wazi.
 
Mkuu
Mnachokifanya ni kuwafanya raia ni mbumbumbu.

Suala la usalama kuna taarifa zinapaswa kutolewa public na zingine za kufanyiakazi.

Uhalifu unapovuja inapaswa ijulikane ili kuwajengea hofu ama kuvuruga stance ya wahalifu.

Kufichaficha mambo ndo mulemule kuwajengea hofu raia
 
Mkuranga na Rufiji ulikuwa nchini!?
 
At least umeweka point inayoleta tafakuri.
 
Itumie hiyo kama case study yako katika mambo ya ugaidi
Kupuuzwa kwa securiry alerts ndo msingi mkuu.

Siasa za kipuuzi ambazo zinawabebesha walinzi wetu majukumu yasiyo yao ni msingi mwingine.

Yapo mengi yaliyopelekea hali ile kwa sababu uvamizi wa vituo vya polisi na kuteka silaha ulifanyika mfululizo na hakukuwepo na hatua thabiti zaidi ya vitisho vya kuwachukulia hatua wahalifu....

Polisi baadhi wanashirikiana na wahalifu na hili lipo ndani yao lakini wanachukulia.kama diplomasia rafiki.

Mkuu kuna mambo tukiyasema hapa tutakumbusha machungu na madhila mengi
 
Marekani wakati mwingine ni kama abudu nondo, wanakualati kumbe wanafanya wenyewe.

October 2020 kuelekea uchaguzi mkuu alert zao kuhusu Zanzibar zilikuwapo hivi hivi. Pana watu waliuliwa na kujeruhiwa sana tu kule.

Una mashaka kuwa wali alert na kufanyiza wao wao pia ndugu?
 
Mkuu kama haujui mambo ya intelligence bora usiyagusie.
Unajua jinsi gani wnakusanya hizo taarifa za intelligence, jinsi wanavyozichambua na jinsi wanavyozishughulikia!?
 
Ninakazia:

"Tishio lipo, Chadema wengine kutoimarisha ulinzi msilalie mlango wazi."
Inawezekana tamko limelenga kuzungumzia jambo kama hili maana kwa mwenendo wa wasaidizi wa Hangaya ni kama wana mpango wa kumharibia mama apoteze uungwaji mkono na raia wake.

Hivyo kulegalega kwa usalama inawezekana ni eneo la kimkakati pia.

CHADEMA wachukue tahadhari kwa sababu wahafidhina wa CCM wamechafukwa kuona siasa inaendeshwa kwa ufasaha sasa
 
Security alert sio ya kuipuuzia...

Pia ni lazima itolewe hata wapangaji wakiiona wanajua wameshang'amuliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…