voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,935
Vichwa vyetu watanzania baadhi vina Matatizo!Wengi wetu humu Tumeona, tunesikia na tumesoma tamko la Ubalozi wa Marekani kuhusu uwezekano wa kutokea shambulio la ugaidi hapa nchini.
View attachment 2497876
Tumesikia mwitikio wa jeshi la polisi kuhusu hatua wanazochukua dhidi ya tahadhari hiyo huku wakituhakikishia usalama na ulinzi. Lakini mimi nineona hapo kuna jambo la kutafakari kuhusu uwezo wetu katika usalama wa ndani ya nchi yetu sambamba na uhusiano wa dola na wananchi.
Iwapo taifa la nje linaweza kuchunguza na kupata uthibitisho wa kuwepo na tishio la usalama nchini na wakatoa tahadhari maana yake kuna kulegalega na kuzembea kwa vyombo vyetu vya ulinzi hususani espionage ya ndani ya nchi.
Serikali ya Tanzania imeeza kupitia viongozi waandamizi kuhusu uwekezaji mkubwa walioufanya katika kununua mitambo ya kudukua mawasiliano ya mitandaoni hususani ikiwalenga wahalifu wa mitandaoni. Hapo awali nilisema kuwa tambo za serikali zinathibitisha kuhusu kuingilia uhuru wa wananchi wake binafsi kwa sababu mifano ya waliochukuliwa hatua hata kufikishwa mahakamani ni wale waliotuhumiwa kutoa kauli ama maneno ya kuudhi dhidi ya watawala. Hatujawahi kuona ama kusikia wahalifu ambao wanafanikisha matukio ya kihalifu ama wanaotoa matishio ya usalama wetu wa ndani waking'amuliwa ama kuchukuliwa hatua.
Marekani kupitia taasisi zake za nje wamejijengea uwezo wa kuwez kupenya vihunzi vya usalama vya makundi ya kiuhalifu dhidi ya binadamu na wakaweza kutambua mipango yao na kwa nia njema kabisa wametoa tahadhari.
Watanzania wenzangu nyie ni mashahidi wa namna ambavyo serikali yetu chini ya mkoloni mweusi CCM inavyotushughulikia raia wake huku ikivunja katiba inayotoa uhuru wa maoni. Ushshidi wa hili ni namna ambavyo asilimia kubwa ya members wa JamiiForums tunatumia pen names au majina bandia ili kuficha utambulisho wetu kwa sababu ya kuhofia vyombo vya dola ambavyo vimekuwa vikitumia kodi zetu kutufanyia uhalifu badala ya kutimiza wajibu wake muhimu wa kikatiba na kisheria.
Wachache wetu tunafahamu kinachoendelea maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Msumbiji pamoja na juhudi kubwa sa serikali kudhibiti utoaji wa taarifa kwa umma. Ndugu zetu wanauawa na magaidi ambao wamejikita kaskazini mwa Msumbiji. Wahalifu hao inasemekana ni wale magaidi waliofurushwa Kibiti na Rufiji hivyo wameamua kuweka base eneo ambalo wanaamini watajiimarisha na kurudi nchini kuleta tafrani.
Tishio la ugaidi kama lilivyotolewa na ubalozi wa Marekani ni wazi kwamba hatupo salama kwa sababu taarifa ya awali ilipaswa kutolewa na vyombo vyetu na kuchukua tahadhari zote.
Tunahitaji kuona vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikitimiza wajibu wao muhimu kisheria na kikatiba kwa kutuhakikishia usalama wetu wa ndani kwa sababu uwepo wao ni muhimu kwetu na si kwa viongozi pekee.
Tufike mahala tuangalie kwa uwiano bajeti ya ulinzi wa viongozi na bajeti ya ulinzi wa umma ili kutenda yatupasayo na si kuelemea eneo moja pekee huku nchi ikiwa ktk hekaheka na matishio ya usalama
TUSIJEKUPUUZA HILI TISHIO..
Hapa unalalamikia jambo lipi hasa wewe Msanii ?
Kwanza unapaswa kuelewa kwamba,ubalozi wa Marekani umetoa tahadhari ile,kuwalenga raia wa Marekani walioko nchini Tanzania.
Na imefanya hivyo kwa sababu,Marekani ni mlengwa namba moja wa Islamic Fundamental Jihadist Groups koote Duniani.
Kwa hiyo,kila inapopata taarifa kama hizo,cha kwanza huwa ni kuwatahadharisha raia wao popote pale wanapokuwa kwa wakati husika.
Vyombo vyetu vya Usalama:
Kwa kawaida,vyombo vya usalama,kwa sababu za kiutaratibu na mifumo ya utekelezaji wake.
Huwa haviwajibiki kufanya kazi kwa matamgazo,isipokuwa pale tu.
Inapovilazimu kufanya hivyo,ili kuwaepusha wananchi kuweza kujihadhari mapema.
Huwa wanafanya hivyo,pale ambapo,jitihada zao kama vyombo husika,zimeelekea kuwa nyuma ya muda,ili kudhibiti tukio kwa 100%.
Kwa hiyo,ukimya unaokuwepo,sio kwamba wanakuwa hawajui.wanachofanya huwa ni utekelezaji wa kimya kimya!
Serikali na vyombo vyake vya ulinzi,huwa iko kazini 24×7×12.
Na pia elewa kwamba,hata huko Marekani,Pamoja na kuwa na Security na intelligence ya hali ya juu.....lakini wanashindwa kudhibiti mauaji ambayo huwa ni ya kigaidi na tunayaona kwenye Media kila siku!
Hata juzi,watu 12 wamekufa California ,baada ya kushambuliwa na mshambulixi wa kujihani aliyebeba silaha.
CIA,FBI,DNAF na wengineo wapo!
Halafu elewa kwamba waliotangaza kuhusu tahadhari ya shambulioo la Tanzanite, sio CIA.....
Ni ubalozi...kwa maana kwamba,kabla hawajatangaza,kuna mawasiliano yamefanyika baina yao na vyombo husika nchini Tanzania.
Na lazima kuna kazi inaendelea!
Kuhusu Kbiiti:
Hawa waasi walioko jimbo la kaskazini mwa Msumbiji,ndio wale waliofurushwa toka Kibiti na kukimbilia Msumbiji kupitia Mtwara!
Na mpaka leo wejikita huko.
Pia ikumbukwe Chadema iliwatetea,ikisema Tanzania inakiuka haki za Binadamu katika kuwakabili.
Tumshukuru Rais Magufuli(R.I.P)
Sababu hakujali kelele za wasakatonge wa kiharakati,yeye aliamua kutafuta usalama wa raia wa nchi yetu Tanzania.
View attachment 2498378