Hebu tukumbushane tulivyosalimika katikati ya kundi la vibaka

Hebu tukumbushane tulivyosalimika katikati ya kundi la vibaka

Invinsible

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
314
Reaction score
376
Ngoja nikumbushie stori yangu niliyonusurika kukabwa na vibaka, basi bhana ilikua siku moja ya wikiendi mida ya saa tisa usiku nilikua natoka zangu kula bata, nipo kwenye gari kuelekea home sasa akili yangu ikaniambia nishuke bakhresa kisha nipande boda mpaka home,

Nilivyofika maeneo ya kagera nikashuka nikasema kwanini nipoteze hela wakati hapa na home nikitembea dk 3 simalizi nishafika, basi bana nikaanza kukata mitaa ya kuelekea home nikiwa full pamba full mkwanja, nikikatiza mitaa ya wakali wa danta, nikapita salama, sasa nimefika kidarajani nivuke nimalize, kwa mbele kama hatua kumi naona watu kama 6 hivi naangalia nyuma naona wengine wawili, wote wanakuja usawa wangu,

Sijui ujasiri niliutoa wapi bwana, nikachukua mkono wangu wa kulia nikaurudisha nyuma ya mgongo, huku nikisema kwa nguvu (nitammwaga ubongo mtu hapa akisogea hata hatua moja) huku nikipiga hatua kuwafuta, aisee walitimka vibaya hadi wengine wakawa wanaanguka kwenye mitaro,

Huku mimi bado nikiwa natetemeka tu nikiwa siamini kinachotokea mpaka nafika home, nikasali sana kwanza, maana wangenikamata na nilivyokua mbishi wangenifanya chongo kama mshikaji wangu mmoja hivi alijifanya mbabe mbele ya hawa jamaa sasa hivi ana jicho moja.
 
ilikuwa around saa6 usiku home hapakuwa mbali na hiyo bar tuliyokuwa tunalewa

kwa kujiamini na kipindi hicho kulikuwa hakuna bodaboda wenzangu wakanishauri nichukue taksi nikawabishia...njiani huku nikiwa na wenge la safari lager nikakutana na vijana wawili,na wote wakinizonga uelekeo wangu...yule mmoja alisema baada ya kunitambua ni 'braza d' halafu huku akitoa msisitizo kwa mwenzake akimwambia 'mwachemwache'

ikawa ponapona yangu,huyu aliyenikingia kifua alikuwa ni 'mwana' na hadi leo tunaonana japo bado kazamia kwenye unga
 
Japo sio watu wazuri ila kuna umuhimu wa kejenga mahusiano mazuri na wana kama hao
 
Back
Top Bottom