Hebu tuwe realistic, haya mambo yalikuwa yana nafasi enzi za ujamaa sio dunia ya sasa

Hebu tuwe realistic, haya mambo yalikuwa yana nafasi enzi za ujamaa sio dunia ya sasa

Jerlamarel

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
843
Reaction score
2,525
Katika dunia ya sasa ya kibepari ni kuwapotezea vijana muda wao maana hiko kinachofundishwa huko JKT hakina applications mtaani.

Vijana wanaenda kuchomeshwa jua miezi au mwaka ila wakirudi mtaani mazingira ya mtaani hayawapi nafasi ya kukiapply walichofundishwa.

Ni lini viongozi wetu watakuwa na mawazo na fikra zinazoendana na nyakati hizi?

“Madhumuni ya vijana kujiunga na JKT ni kuwajengea uzalendo, kuwajengea ukakamavu lakini kuwapa stadi mbalimbali ili baada ya hapo waende kujiajiri. Madhumuni si kutoa ajira kwa vijana hawa."

-Waziri Dkt. Stergomena Tax.

20220916_113245.jpg
 
Ni kweli ipo haja ya kubadilika siyo kwa hayo mafunzo ya JKT Bali Kuna mifumo mingi ya kizamani inapaswa kubadilika Ili tuendane na nini watu Mungu aliowapa wakati wa kuishi Sasa waishije Ili kuifanya dunia ieleweke na watu wake wawe wa kujitambua.

Tunahitaji viongozi watafute maono ya Hali ya juu Ili waache ligasi maana kiongozi asipoleta maono ya kuleta mabadiliko hawezi kuacha ligasi yoyote zaidi ataonekana alifanya kazi kwenye mifumo ya wenzake walioishi katika zama hizo na yeye kutembelea zama za kale zilezile kitu kitachorudisha nyuma maendeleo ya wakati huo na wakati wa baadaye.

Mifumo ya kale ya elimu inayopoteza muda ibadilishwe, mifumo ya uongozi ibadilishwe iwe mifumo ya kuteua viongozi kwa maandiko yao ya maono mapya, mifumo ya ulinzi ibadilishwe, mifumo ya afya ibadilishwe badala ya kujenga vituo vya afya vya kufanya kazi mchana basi vijengwe vituo vya afya vya kufanya kazi usiku, na mipango ya maendeleo ije kimtaa na siyo kiwilaya kitu kinachorudisha maendeleo kuwa ya kale yaani Kila mtaa upate vitu vyote muhimu kitu kitakachozslisha ajira nyingi maana ajira za kujiajili zinaanzia kwenye mtaa, Kila mtaa ukiwa na soko tayari ajira zitapatikana, stendi, mall za biashara, vituo vya polisi, hospital kubwa, shule zihesabike kimtaa kuanzia msingi mpaka chuo kikuu, hapo tutakuwa tumekwenda na wakati tuliopo Sasa.
 
Back
Top Bottom