Hapa kwetu TZ siku hizi kuna watu wengi wanaitwa Dr. somebody au Prof. somebody. Lakini ukienda kwenye strong journals duniani huwakuti kabisa majina yao katika articles. Hivi huwa wanapata hizo PhDs na uProf. vipi? Yani mtu anajiita Prof halafu anakaa miaka hajafanya publication? hata wanafunzi wa masters tu amewakosa ili waweze kuproduce papers! Inabidi tuchunguze au nako huko vyuoni kuna ufisadi wa kuinuana tu na kupeana u prof kwa reports za hapa na pale na vijiconference vya morogoro, arusha na dar?
Hata hivyo mambo ya Sayansi hayana mshiko hapa JF. Ni siasa kwa kwenda mbele!!🙄
Yeah,JF haina mshiko sana kwenye Science.Siasa imezidi sana humu ndani.Hata hivyo ili ku-improve ushiriki wa watu kwenye category ya science and technology....wakuu wangevunja badala ya kuwa na science and technology tungekuwa na categories nyingi nyingi ndogo ndogo ambazo ziko very particular mfano MEDICINE,COMPUTER SCIENCE etc.....yaani maeneo ya namna au tunaweza ku-break down further ili mtu achague interest yake....
Mtazamo tu...
Hapa kwetu TZ siku hizi kuna watu wengi wanaitwa Dr. somebody au Prof. somebody. Lakini ukienda kwenye strong journals duniani huwakuti kabisa majina yao katika articles. Hivi huwa wanapata hizo PhDs na uProf. vipi? Yani mtu anajiita Prof halafu anakaa miaka hajafanya publication? hata wanafunzi wa masters tu amewakosa ili waweze kuproduce papers! Inabidi tuchunguze au nako huko vyuoni kuna ufisadi wa kuinuana tu na kupeana u prof kwa reports za hapa na pale na vijiconference vya morogoro, arusha na dar?
Mama... hilo umeligundua leo? Lipo tena kwa sana. Jaribu kuchukua majina ya walimu wako (Ma-Dr na Ma-Prof) halafu uyachape kwenye search engine za maana kama Pubmed, usishangae kukuta mtu hayumo! Kuna mwalimu wangu ana paper moja tu kwenye Pubmed!!
Hata hivyo mambo ya Sayansi hayana mshiko hapa JF. Ni siasa kwa kwenda mbele!!🙄
Kwi kwi kwi,
Nafasi ya kupenya BOT kama wewe mwanasayansi utaipata wapi? Hata hiyo ya kufundisha tu huipati hata kama uwezo unao kama wewe sio ndiyo mzee! Kamulize Prof Baregu!
Wakati wenzenu wanagawana keki mil 30, 50, 100, nyie mnagawana mmba kwa ajili ya kukuna kichwa, eti sayansi!
Hadhi Tz itarudi pale wasomi watakapoona nafasi yao na kuacha kuwabeba wanasiasa kwa mbeleko. Wajisikie huru kusimama popote sio ndani ya ccm tu, na hapo ndipo wanapoweza kuwa na nguvu ya kuanisha pumba na mchele uko wapi! Hatujiulizi ni kwanini wanasiasa uchwara wana nguvu ya kupindukia?
very funny...Professor Majimarefu,Professor Vulata(RIP),Dr Remmy Ongala...hawana research papers
habari ndiyo hiyo! katika nchi za wenzetu mtu anakuwa Dr. lkn sio prof. kwani unaweza kuwa Dr. kwa kusomea degree tu (baada ya masters), baada ya hapo kama hujafanya mambo ya risachi zaidi wewe utabakkia Dr. fulani tu...ukifanya risachi na ukafanikiwa ku publish 'journals', kuhudhuria international conferences ndio wanaangalia namna ya kukupandisha kwenda assnt prof, assoc prof na prof. hatua hizi zote ni mpaka uwe na uzoefu kazini na publication za maana. lkn bongo sivyo...kamati zinakaa tu na kuamua aaah fulani sasa ni Prof teh teh teh teh...huko vyuoni kuna ufisadi wa kuinuana tu na kupeana u prof kwa reports za hapa na pale na vijiconference vya morogoro, arusha na dar
.................. Baraza la mawaziri tu lina maprofesa kibao na PhD za kumwaga (ingawa nyingine ni za kichina). Hapa hatutoki kabisa. Tumetumbukia kwenye matope!!
mzee, nimelazimika kuchangia baada ya kuona hilo nililokoleza wino! hujatembea wewe!!!!!!!, ukifika china na kuona maendeleo waliyopata kwa miaka 60 ya uhuru wao, hutadharau tena elimu yao na wala hutasaga bidhaa za china kwa greda eti "feki".
china leo wanamalizia kuweka metro kwenye tu-miji tudogotudogo, tena bila msaaada wa kiufundi, wala wa kifedha toka kokote nje ya china!!! we hapo bongo tunaweza kufanya nini??? hata barabara korofi hazitengenezwi hadi tutemewe mate na wazungu!!
hata huyo sijui sarungi aliyekuwa na elimu unayoiabudu, alipokuwa moi alifanya nini? wagonjwa walikuwa hawapelekwi nje kwa matibabu ya mifupa? ndi maana alipoona hafanyi kitu akajisalimisha kwenye siasa! tafakari kidogo ndugu kabla hujaingia jamvini!
Naona unajaribu kuchukulia issue hii personal wakati mimi nimechangia kiujumla. Kama unaishi Tanzania kwa sasa utakuwa unaelewa maana mtu anaposema kitu ni cha kichina. Kama hujakutana na hilo neno basi pole na omba watu wakusaidie, badala ya kuanza mashambulizi yasiyo ya lazima. Kwani bidhaa za feki za kichina hazipo Kariakoo na kwingineko? Kama ulitaka kueleza kuwa wachina wanafanya vitu genuine basi tueleze viko wako wapi katika soko letu? Watu wanaongelea wanachokiona na siyo hadithi. Kama kwao wanatenegeneza vitu vya maana wakati sisi tunaletewa feki bado tutawaponda tu!
Mgombea Ubunge;705099]kwa sasa siko tz lakini huo msemo naufahamu, nieshawishika kutahadharisha baada ya kuona hata great thinker anaponda bidhaa za china!
labda nikuulize, kama kitu ni feki na kinafanya kazi iliyokusudiwa na kinauzwa kwa bei nafuu ili kila mtu amudu kununua, kuna madhara gani? ningefurahi kama wangefanya kazi ya kuvi-study vtu ivyo ili kuangalia namna ya kukopy technolojia rahsi badala ya kuviponda ukiwa huna kitu katika soko lako cha kujivunia!
tunapaswa kuacha kasumba ya kushabikia vitu vya ulaya kwani hata huko nako kunatoka feki.
ili utengeneze genuine unaanza na na kitu (whether feki or otherwise) kisha unaendelea kuboresha. ndivyo walivyofanya hata ulaya na wanaerndelea kufanya hivyo hadi leo. hivi vitu mnavyoita feki huwa vinatolewa kwa bei nafuu ili kila mtu amudu kununua. ndivyo ilivyo hata kwa magari yaliyotumika. wangecrash magari yote ya mitumba, wangapi dar wangekuwa na magari? achilia mbali nguo!
tuamke,tujitetee,
hao wanaocrash vitu kwa madai ni feki wamo kwenye payrol ya mafisadi na wanwasafishia njia wauze mizigo bila ushindani, kama ulikuwa hujui, habai ndiyo hiyo!
Wasomi wengi wamegeuka wanasiasa!
Sasa watu kama Prof. Msola ndio hao wameamia kwenye siasa, huo utafiti utafanywa saa ngapi?! Tatizo letu bongo ni misallocation of resources (ikiwemo rasilimali watu) na kushindwa kutofautisha politik na academics.
Utafiti wa kisayansi unahitaji kuwekeza pesa nyingi sana jambo ambalo Tz hatujalipa kipaumbele. Nadhani kama kungekuwa na tafiti za kutosha, ugonjwa kama malaria lisigekua tatizo kwa sasa!
Mimi sina ugomvi na vitu vya bei rahisi au vya kutoka china. Kwenye ile post yangu nilitumia neno kama wanavyotumia wengine (loose meaning). Hata hivyo napata shida kwa jinsi hali ilivyo sasa hapa Tz ambapo mtu unahahikikishiwa na wauzaji kuwa kitu ni genuine kumbe ni feki toka china. Hapo ndipo ugomvi unapoanzia. You pay deally to get fake stuff! Kama tungeletewa genuine kama bidhaa zinazopelekwa Ulaya na US hayo huo ugomvi usingekuwepo. Wachina kushirikiana na wahuni na mafisadi kutuibia kunaleta damage kwa pande zote mbili. Kwa hiyo Wachina hawawezi kukwepa lawama ingawa ujinga ni wetu na sisi (Watanzania) ndio tunabeba lawama kubwa!
nimekupata mkuu ..............
Hapo tuko pamoja. Ndio maana tunalalama kuwa kama siyo kutelekeza sayansi na elimu kwa ujumla tusingekuwa tunaagiza hata viberiti toka China.