Hebu wana Simba SC tuacheni Utani, Unafiki na Uongo. Kuna anayependa kweli tukutane na Yanga SC Robo Fainali ya CAFCL?

Yanga anafungika vizuri tu ila timu nyingi zinacheza nayo kwa kufanya makosa yale yale ya kiufundi. Wakati fulani nililazimika kuleta uzi kufundisha jinsi ya kucheza nao maana niliona hayo makosa ya kiufundi yanajirudia kwa timu nyingi.
 
Ni mapenzi tuu...hahaahaha nikute live sasa hakuna anaejua naandika hivi kuhusu Simba..ndo uzuri wa kutojulikana... 😂 😂 😂 😂
Dahh..nimecheka kwakwel. Kwahiyo yakiwekwa pembeni majini, Yanga anakalia
 
Bila majini wanayotupia wachezaji wa timu pinzani yawafunge miguu wawe wazito uwanjani hawana lolote hao utopolo.
 
Kwa hio champions League ndio mbovu?
 
Vyovyote vile ulivyoelewa, lakini alichoongea ndio ukweli wenyewe, Simba hana timu ya kupishana na Yanga.
Na hakuna mwanasimba ambaye anatamani hii itokee hata mwezi wa 4 ni kama unakuja kwa kasi sana
 
Endeleeni kuvimba kichwa na hyo timu yenu mtashangazwa....
 
Binafsi nisiwafiche kwani sitaki na wala sitamami kwa sasa kwani Kiufundi kwa sasa Simba SC hatuna Kikosi thabiti cha Kucheza na Yanga SC iliyoko Relini na ya Moto kila Idara.
Ila IHEFU wana kikosi cha kucheza na UTO
 
Labda kuanzia nusu fainali huko ila kwa robo fainali ni ngumu sana team zilizomaliza makundi katika nafasi ya pili kukutana.
Kama hawawezi kukutana robo basi ujue haiwezekani hadi fainali, maana walioshika nafasi za pili kwenye group wanakaa upande mmoja na walioshika nafasi za kwanza wanakaa upande mwingine
 
Binafsi nisiwafiche kwani sitaki na wala sitamami kwa sasa kwani Kiufundi kwa sasa Simba SC hatuna Kikosi thabiti cha Kucheza na Yanga SC iliyoko Relini na ya Moto kila Idara.
Hahahahahahahahahahahahaahahahahahaha.......mkuu.uzi huu, Ulitakiwa uulete hapa siku ilee ya pakome.
Ajabu ulijificha wiki nzima.

Hahahahahhahahahahahahahahahaha.......aiseh!!!
Hapo sasa sawa kama umekubali mwenyewe.
 
Binafsi nisiwafiche kwani sitaki na wala sitamami kwa sasa kwani Kiufundi kwa sasa Simba SC hatuna Kikosi thabiti cha Kucheza na Yanga SC iliyoko Relini na ya Moto kila Idara.
hivi mnajua kuwa simba imeuzwa?
 
Unaongelea ushindi wa 6 ambao ni wa zamani namna hiyo, ushindi wa 4-1 ambao yanga ilikua inatembeza bakuli.
Mambo yamebadilika mno siku hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…