Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Najua jukumu la mwanaume ni kuleta mambo chanya kwa familia yake na jamii inayomzunguka.Yameshasemwa mengi sana,lakini bado yatasemwa.MWANAUME anajulikana ndie KIONGOZI wa jamii katika hali zozote,hili halina ubishi,sasa kama kiongozi anakuwa wa hovyo hata kile anachokiongoza nacho kitakua hivyo hivyo.Ni ukweli ulio wazi jamii yetu leo ni ya hovyo,kama ni ya hovyo ni lazima kiongozi ndo ameruhusu hayo na kwa upande mwingine nae ni wa hovyo.Kuna mambo kama ukahaba,watoto wa mitaani na kukosekana uaminifu kwenye ndoa/mahusiano,ninaamini kama wanaume tungekua dhabiti,hata kungekua hakuna huu ujinga wa kudai haki sawa.Naita ujinga kwa sababu wanaume kwanza tangu mwanzo,mwanaume ndo alikua anahudumia familia alipochemka mwanamke ikabidi aende nae front line,mwanaume alipowaka tamaa alianza kumshawishi mwanamke kumpa mwili wake kwa malipo ndipo ukaibuka ukahaba,still mwanaume akashindwa kuridhika na mkewe akaenda kuanzisha nyumba ndogo(kuna wajinga wanasapoti hili)matokeo yake wanatelekeza familia maisha yanakua magumu watoto nao wanaingia mtaani tunapata watoto wa mtaani.Haya ni makosa makubwa yaliyofanywa na yanafanywa nasi leo,yapo mengi lakini hebu tuyajadili hayo leo.Najilaumu mimi kama sehemu ya wanaume na nawalaumu wenginepia kwa sababu inafahamika mwanaume pekee ndie alikua mtafuta riziki so ndie alikua anatoka nyumbani na kumuacha mwanamke,na mwanaume ndie alikua mtoa maamuzi kuanzia familia,mtaa hadi taifa,sasa tutakwepaje lawama?Sisi ndo tulioanzisha upuuzi mwingi kwa kuwa ndo tulikua na mamlaka.Wateja wa makahaba ni wanaume,wanaoanzisha nyumba ndogo ni wanaume,wanaowapa ujauzito wanafunzi ni wanaume,mambo ya hovyo tunayofanya ni mengi halafu tunayatetea,this is a shame.Unadhani unapoonesha mambo ya hovyo na tabia za hovyo,unadhani unaemuongoza atakuheshimu?Sidhani,ndo maana wanawake kudai haki sawa naita ujinga kwa kuwa kumetokana na udhaifu wetu wanaume.Hebu leo tusemezane tulikosea wapi ili tuparekebishe ili turudishe heshima yetu jamani!