Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea na kampeni yake ya kudai mabadiliko ya sheria za uchaguzi kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, kupitia kampeni yao maarufu ya "No Reforms, No Election" katika Kanda ya Kaskazini.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche ameongoza msafara wa chama hicho akihamasisha wananchi kushiriki katika kudai mazingira huru, haki na sawa ya uchaguzi.
Leo Jumanne Mei 27, 2025, akiwa njiani kuelekea Tarakea kwa ajili ya mkutano wa hadhara, msafara wa Heche ulisimamishwa na wakazi wa Mamsera, Jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro, wakitaka kumsalimia.
Leo Jumanne Mei 27, 2025, akiwa njiani kuelekea Tarakea kwa ajili ya mkutano wa hadhara, msafara wa Heche ulisimamishwa na wakazi wa Mamsera, Jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro, wakitaka kumsalimia.