Pre GE2025 Heche amchana RC Chalamila, kisa kauli ya mjamzito anayegoma kununua gloves, adai wamejisahu kwasababu ya shibe ya kijinga

Pre GE2025 Heche amchana RC Chalamila, kisa kauli ya mjamzito anayegoma kununua gloves, adai wamejisahu kwasababu ya shibe ya kijinga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Chalamila is a liability to ccm!! Yupo hapo kwa sababu ya ukaribu wa spika Tulia na Samia! Akiwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya alimsaidia Tulia kuiba kura za ubunge na kushinda!! Baada ya kutumbuliwa Tulia ndio akaenda kumuombea msamaha aka rudisha!! Chalamila hajifunzi anarudia makosa yale yale ya kudharau wananchi kwa kauli zake za udhalilishaji! He is a liability to ccm
 
Kwa ambao mmewahi kufanya kazi mazingira ya hospitali mtakubaliana na Chalamila ila hamtakubaliana na maneno aliyotumia.

Wananchi wanapotoshwa mno na siasa. Mwanasiasa anamwambia mwananchi mzee, mtoto chini ya miaka 5 na mama mjamzito anahudumiwa bure kabisa.

Mzee anakuja hospitali, ana kitambulisho cha wazee ambacho kinacover vitu vichache akija kuambiwa vingine anatakiwa kulipia anampigia simu Diwani kulalamika.

Diwani anaside na mwananchi. Bila kukumbuka hospitali ikishindwa kujiendesha yeye diwani amechangia katika level hiyo.

So, kiukweli Chalamila alikua na ujumbe mzuri ila uchaguzi wa maneno ndiyo changamoto
 
Sisi tunasubiri matukio ndio tupate cha kusema na sio kuwa agenda zetu wenyewe
 
Sasa kutokana na hata ARVs na dawa za TB kua zinaletwa na USAID na PEPFAR ndiyo sababu Tz inazitoa bure hizi kwa waathirika. Trump ambavyo ana mpango wa kujitoa na hizi dawa zisipokuja means itabidi Serikali inunue na iweke utaratibu wa wananchi kuchangia hii huduma.

Ni wakazi wangapi wa Mpwimbwi wanajua kua dawa zinaweza kusitishwa na mbadala ni wao kuchangia? Vipimo vya Malaria na dawa vyote vilikua bure, chanjo za watoto hadi neti. Ikifika muda mbadala ni kuchangia pekee hapo sasa ndiyo moto utawaka na itabidi waambiwe ukweli
 
Kushika mimba na kujifungua siyo suala la dharura, wazazi tunapaswa kuchangia huduma za kujifungua
Serikali haitoi bure sio mnakaa serikali serikali bure bure hii serikali haitoi bure ila kupokea tu misaada inapokea bure kabisa serikali inapokea misaada ya Marekani inakula na yenyewe haihudumii wananchi sababu haitoi bure misaada ile inaenda wapi hawasemi misaada inayoletwa ikitolewa kwa mgongo wa Serikali alietoa msaada hatajwi mpaka Trump kachukia pongezi zote kwa Muheshimiwa ndio maana kuna Nchi moja ya kigeni imeona bora iende yenyewe hewani imejenga shule huko Dodoma ikasema imejenga yenyewe km msaada la sivyo bila kufanya hivyo pongezi zote zingeenda kwa Muheshimiwa
 
huyo Heche hajaelewa mkuu wa mkoa alichomekea hilo kama kuwakumbusha wanajamii mambo ya msingi kama ya kuandaa vifaa vya kujifungua,lishe ,nk mambo ambayo wazazi hupata elimu kipidi cha kiliniki ya uzazi...rai yangu asiwagombanishe wananchi na serikali sikivu na uzuri wananchi walimwelewa mkuu wa mkoa hilo liko wazi ndugu
 
Wakuu

Makamu Mwenyekiti wa Chadema (bara), John Heche amlipua RC Chalamila kwa kauli yake iliyozua gumzo kuhusu Mama Mjamzito aliyempigia simu na kumweleza changamoto ya ukosefu wa Gloves hospitali.

Soma, Pia: RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani
Ngoja kwanza,hivi mama mwenye uwezo wa kuongea na mkuu wa mkoa kwa simu yake, anaweza kukosa bima ya afya muda wa ujauzito wake? RC alaumiwe kwa kauli zake zisizolingana na utamaduni wetu.
 
UWT ni wanafiki sana,mpaka sasa wapo kimya ilhali yule RC mwingine walichachamaa mbaya!

Au ndiyo mambo ya kutumika?
 
Kushika mimba na kujifungua siyo suala la dharura, wazazi tunapaswa kuchangia huduma za kujifungua
Hizi ni kauli za shibe......

Mnaweza mkapanga mzae na mkeo katikati ya safari ya miezi tisa kukatokea changamoto za kukufanya kuwa omba omba hali ya kuwa ulijipanga......

Hebu fikiria upo katikati ya safari ya mimba mwanao anaumwa....utamuacha afe kwa kuwa hiyo akiba ni kujifungua mkeo.......

Si vyema kuyapima mambo kwa utashi wako na mazingira yako bali katika uhalisia wake.......

Laki tano ni hela ambayo watu wanaimalizia baa dakika au masaa kadhaa tu.,.lakini kwa upande mwingine hiyo ni hela ambayo mtu anafanyia jambo kubwa linaloendesha familia.......
 
Watu wana haki ya kuilaumu serikali kwa hilo kwa sababu ni wao hua wanapita huku na kule kudanganya watu hasa kipindi cha kura kwamba matibabu kwa watoto wa chini ya miaka mitano, wazee na wajawazito ni bure lakini hawaambii watu ukweli kwamba hiyo bure ina maanisha nini wanachi wanashika neno bure wakienda kwenye huduma wanasalitiwa, dharau na kejeli juu, kama wananchi wangekua wanajitambua huu ndio muda wa kufanya mabadiliko ya kweli
 
Back
Top Bottom